Shule gani ya advance ni nzuri kwa mikoa hii?

KJ07

JF-Expert Member
Dec 17, 2021
2,242
4,992
Salaam wakuu,

Natumai nyinyi ni wazima wa afya na wale wenye changamoto mbalimbali za kiafya basi Mungu awape ponyo.

Niko katika utafiti wa shule gani ya advance ni nzuri kwa michepuo ya sayansi ambayo ni girls school.

Mapendeko yangu ni kwa mikoa isiyo ya baridi kali mfano dodoma, pwani,mwanza n.k

Natanguliza shukrani wakuu.
 
japo hujasema ya private au ya serikali?
dodoma = msalato
mwanza= bwiru girls
moro= Dakawa high school
 
Dodoma, kuna Dodoma sekondari. Msalato siyo kwa kuingia bila hodi! Kule ni kwa wale watoto vipanga.
 
Dodoma, kuna Dodoma sekondari. Msalato siyo kwa kuingia bila hodi! Kule ni kwa wale watoto vipanga.
DODOMA SEC hakuna shule hapo!!!


DODOMA ukiondoa Msalato ambayo ni Special, sizani kama kuna shule nzuri kwa girls hasa Sciences


Kama MWANZA nenda Nganza Girls au Bwiru Girls ila kwangu Nganza ndio Bora zaidi
 
Back
Top Bottom