Shukrani kwa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukrani kwa Kikwete

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Jan 2, 2011.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikijiuliza kwa muda, hivi ni kweli kuwa Tanzania na watu wake wote ambao ni Milioni 39.999.999 tumekubali kwa urahisi kuongozwa na mtu mmoja na kwamba kila linalokwenda mrama ni yeye pekee apokee lawama?

  Hata ukiweka mizani ukatusimamisha sisi Milioni 39,999,999 upande mmoja, na yeye upande mwingine, iweje mizani ielemee upande mmoja?

  Sasa mwaka 2005, nilijisemea labda zile asilimia 80 zilitokana na Watanzania wenye tumaini, lakini baada ya miaka mitano ya ubangaizaji wa hali ya juu, bado hata kwa kuchakachua tumempa tena nafasi nyingine ya miaka mitano aendeleze libeneke!

  Lakini najiuliza, labda nikianza kupunguza kundi la Watanzania kwenye hii mizani na labda tuseme ni Watanzania 1000 ambao ni Wanasiasa kwa mgawanyo wa kuwa Wabunge, Makatibu Wakuu, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wengine ambao wameteuliwa kazi na Rais Kikwete. Je hata nanyi mmeshindwa kulazimisha mizani ikaangukia upande wenu?

  Hakieleweki kama tutadai Kikwete ni Rais Mvivu, Mzembe, Mbangaizaji, Mfujaji, asiye Makini, asiye Wajibika, asiye Fanisi, asiye Jituma au si Mfuatiliaji na Msimamizi mzuri (angalia matumizi ya makusudi ya herufi kubwa katika hayo maneno) wa kazi hata tukamtuhumu kuwa ni Fisadi, Mla Rushwa na Mhujumu Uchumi, lakini wale walioko chini yake, hata mmoja wao asiwe maridadi na kutupa tumaini na taswira kuwa kuna tumaini.

  Nikianzia na mawaziri, wengine wamerudi kwenye Uwaziri na hata wengine kuendelea na wizara zao. Leo sielewi ni vipi bado tunaendelea kuwa na tatizo la Chakula, Umeme, Afya, Maji, Elimu, Mifugo, Uhalifu na Uchumi mbovu na waliopewa majukumu ya kuongoza Taifa na hasa vitengo hivyo bado ni wale wale au wamepewa amjukumu mapya.

  Ni kazi gani nzuri mno waliofanya mpaka wakastahili kupewa majukumu haya kwa mara nyingine?

  Tuongelee Maji, najua lengo ni kuhakikisha Tanzania nzima ina maji ikifika mwaka 2025. Sasa ikiwa Mkoa wa Dar Es Salaam ambao ndio jiji kubw, bado lina shida kubwa ya maji, iweje tuendelee kuamini kuwa Waziri,naibu waziri na Katibu Mkuu wanafanya kazi nzuri kabisa? je ufanisi wao umefanikiwa vipi kuondoa tatizo la maji Dar? Je ni kweli hawa walioko kwenye hizi nafasi ni watu mahiri na wenye uwezo wa kielimu, tija na ufanisi kufanya kazi yao bila kujali udhaifu wa mwajiri wao? kwa nini basi wao hawang'ai na kutupa Watanzania tumaini kuwa labda ni Rais pekee ambaye hana uwezo wa kuchapa kazi?

  Njoo kwenye umeme, huko nako ni vituko, kila siku umeme unakatika katika na tunasaini mikataba mipya kila tukiamka, lakini hata kuhakikisha Dar Es Salaam pekee ina umeme wa kutosha kuendesha viwanda na uzalishaji inakuwa ni vigumu, je tuna mtu mahiri na mwenye uwezo pale Wizara ya Nishati na hata Tanesco?

  Turudi kwenye miundo mbinu. Wala hakuna haja ya kwenda nje ya Mbezi Luisi, anzia pale, njoo mpaka huku Bunju, nenda Pugu na kule Mbagala. Msongamano wa magari ni mkubwa, barabara ni finyu na mbovu, hakuna mifereji ya maji machafu, hakuna a, hakuna b, hakuna c na Waziri wa miundo mbinu, pale nje ya jengo la ofisi yake Tancot house, kuna mashimo barabrarani, hakuna miundombinu mizuri na ni kero tupu.

  Je ilistahili nini huyu Waziri wa awamu ya nne sehemu ya kwanza kuteuliwa tena kuwa Waziri awamu ya nne sehemu ya pili?

  Tuje kwenye masuala ya Uchumi, Waziri wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu, Waziri wa Biashara, nao wameshindwa kabisa kulitutumua Taifa letu kiuchumi. Ile kauli yaAri, Kasi na Nguvu mpya imekuwa ni kichekesho huku matumizi yakiongezeka kila siku, thamani ya fedha ikishuka kila sekunde na ubadhirifu wa kodi ni kila nukta. Lakini hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kujiwajibisha na kumwambia Rais, kazi hii imenishinda, siwezi kuwapa Watanzania matokeo nbora na kuamsha tumaini jipya.

  Tuje Kilimo, Afya, Elimu, Mambo ya Ndani, Utawala Bora, Ardhi, Maliasili, Utumishi, Uwekezaji, TAMISEMI na hata Uwaziri Mkuu, je ni vipi tumerudishiwa watu ambao wameendelea kuonekana ni dhaifu na si fanisi hata chembe?

  Haya uje kwenye wilaya, mikoa, Taasisi, Mashirika na hata Balozi zetu, bado matokeo ni yaleyale! Je tutaendelea kudai hii ni kutokana na Kikwete kuwa na Wasifu huo, basi kila aliyepewa jukumu haoni sababu za kujituma kama Bosi hajitumi?

  Hata tukija kwenye Chama Tawala, iweje katika mchakato wao walikubali kuendelea kuteua na kuchagua Wagombea ambao i wachapa kazi? Je utamaduni umekolea sana kiasi kwamba leo watuhumiwa wa Uhujumu bado wanapewa nafasi kubwa na ya heshima ndani ya CCM ilhali inajulikana wazi kuwa wameelemewa na tuhuma za Uhujumu na Uzembe wa hali ya juu uliolitia Taifa hasara?

  Je hili linaashiria nini kwetu sisi Wananchi? Je nasi tumeamua kuiga tembo midhali Rais wetu ni mdhaifu na mbangaizaji, nasi tunaendeleza libeneke kwa kufuata nyayo?

  Sasa atakapoondoka madarakani Kikwete, ndipo tutaamka na kuanza kujituma na kutafuta Rais mpya katika kundi hilohilo la wale ambao wala hawajigusi kujitutumua na kuonyesha matunda ya kweli ay kazi na si porojo na mvuke wa mchemsho ambao hufifia makaa yanapopungua nguvu?

  Ninampa Shukrani Kikwete kwa kutuonyesha wazi kuwa pamoja na udhaifu wake, ni wazi hakuna mtu ndani ya kundi lake analoliongoza na hasa Chama chake CCM ambaye mwenye uwezo, utashi na ari ya kuliongoza Taifa letu kuondokana na Umasikini, Ujinga na Maradhi.

  Simlaumu Kikwete pekee ingawa yeye ndiye Alpha na Omega wa siasa na Uongozi, lakini wengine wanaojitia wanaweza kuwa Marais wa Tanzania, iweje hatuoni basi matunda bora ya kazi zenu leo hii?

  Ina maana mnataka tusubiri mpewe Urais ndipo mtuthibitishie kuwa mna uwezo?

  Kikwete alilaghai Watanzania kuwa alikuwa amejiandaa vyema kwa miaka 10 kuwa Rais, matokeo yake ni kuwa hadi leo hii inaelekea bado anajifunza kazi au haelewi nini wajibu wake.

  Jee nanyi bado mnajifunza kazi na kubahatishabahatisha?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  I got my chopsticks ready to devour this nice peace of meal for the first Sunday of the Year... delicious..
   
 3. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Rev I really missed your posts! Happy new year !!
  I have learned through the school of hardknocks politika
  Eng Nsiande
   
 4. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwalimu come again plse
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mbombo ngafu kweli kweli Rev!
   
 6. D

  Dotori JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hard core....sobering.....
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ah,sina cha kusema
   
 8. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni sawa lakini nadhani ndio maana akaitwa 'Amiri Jeshi Mkuu'
  Sidhani kama ni title tu....but hata matendo yake yanapaswa yafananie!
  Uongozi wake yeye mbovu ndio unaopelekea hata utendaji wa watu wake ukawa mbovu,
  Imagine upo nyumbani kwako una familia ya watoto kama 6 tu, wale watoto wanapokuwa na tabia za ajabu nani hulaumiwa??
  Ni baba/mama ofcourse coz wao ndio vichwa vya familia...
  The same applies to our President...
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Cha kukuuliza ni, wewe Kishoka kama raia umeifanyia lipi Jema moja Tanzania?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haya halafu utuwekee pumba zako kama kawaida, lakini angalia wenzako washaanza kukushtukia maana hivi juzi juzi tu niliona wanavyoku kandia! nikasema AlhamduliLllah yale niliyoyaona mimi zamaaani wao ndio kwanza wanayaona!
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jema nililofanya ni kukiri udhaifu wangu...je wewe?
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nimependa sentenso yako ya mwisho. Na huo ndio ukweli. Na bado anaendelea kujifunza kwa miaka mitano ijayo, tupilia mbali ahadi alizozitoa katika kampeni za mwaka huu za kufanya sijui mji gani ule uwe Dubai ya Afrika.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu ni vuvuzela wa Kikwete na uozo wa mafisadi.
   
 14. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Rev.Kishoka
  Hivi nikweli haufahamu hawa watu wamerudije madarakani? umechambua vizuri sana lakini siamini kama hili hulitambui........
   
 15. Wameiba Kura

  Wameiba Kura JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  When u have mind Pregnant people like u use mouth to command brain to talk instead of using brain to command mouth to talk. :frusty::frusty::smash::smash:
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hilo umejifanyia mwenyewe, soma swali!
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  You are very wrong, I use qwerty keyboard!
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jasusi,

  Inasikitisha kuona tuna watu wamekuwa mawaziri miaka karibu 20 wanabadilishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine, lakini hatuoni ufanisi wa kule wanakopewa majukumu. Huko majimboni, wanapewa dhamana ya kuwawakilisha wananchi kwa kisa cha kuwa Waziri na imekuwa mtindo (fashion) kwa watu kukimbilia Ubunge ili wawe mawaziri.

  Swali ni hili, je Marais wetu wanaendeleza utamaduni wa kuchagua na kuteua watu wadhaifu ili wasipigwe mapiku? Maana kama Rais anaendelea kututeuliwa mbangaizaji, je ina maana Rais anapenda wabangaizaji wasiohoji mambo au kumbishia?

  Au kwa kuwa Rais ni mbangaizaji basi akiajiri na kutgeua Wachapa kazi ataaibikia na kuanza kudoda kisiasa kwa kuwa Wananchi wataanza kutoa tukuzo na sifa kwa mchapa kazi na si mbangaizaji?

  Je Rais anaficha udhaifu wake kwa kuajiri wabangaizaji kwa gharama za kodi yetu?
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nakusifu kwa kujuwa mambo, wewe ni zumari la rev kishoka?
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa mchungaji lakini wewe kama wewe ni kati yetu kwani wewe una mpango gani wa kutilt huo mzani?
   
Loading...