KERO Shirika la Umeme Zanzibar mnatukwaza kukata umeme mara kwa mara maeneo ya Kwahani na mnajua kuna Kituo cha Afya, Ziwani Police Health Center

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mkazi wa Zanzibar katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Mjini.

Kero yangu ni kwa Shirika la umeme Zanzibar (ZECO).

Wamekuwa na muendelezo wa kukata umeme mara kwa mara maeneo ya Kwahani, ikizingatiwa sehemu hiyo kuna Kituo cha Afya, Ziwani Police Health Center kinachotoa Huduma za jamii kwa wakazi wa maeneo hayo na kupelekea Huduma kusimama kwa muda mrefu na kuwaathiri wananchi.

Tunaliomba shirika la umeme ZECO wajitahidi kurekebisha miundombinu ya maeneo hayo ili huduma ziendelee kutolewa kwa jamii.


Pia soma ~ ZECO: Changamoto ya umeme Zanzibar inachangiwa na miundombinu ya kusafirisha umeme, kuna mpango wa kuweka njia kutoka Bara
 
DAH KITUO CHA AFYA HAKINA GENERATOR, MBONA HII NI HATARI ENDAPO KITAPOKEA MGONJWA MAHUTUTI USIKU NA UMEME KUKATIKA?
 
Shakuru maana umeme wenyewe mnapewa bure na watanganyika
 
DAH KITUO CHA AFYA HAKINA GENERATOR, MBONA HII NI HATARI ENDAPO KITAPOKEA MGONJWA MAHUTUTI USIKU NA UMEME KUKATIKA?
Umeambiwa ni Bima ya Afya kwa Wote itakapokua tofauti na watu kuanza kukunja ndita kwamba kinachosemwa na kinachofanyika sio sawa ndio hapo wahuni wanaingia na mitutu barabarani wanaanza kuua watu mmoja mmoja
 
Kama wiki imepita nilisikia, umeme unakatika katika maeneo mengi ya Ugunja si Kwahani tu,
Na hii huenda inachangawi na wanasiasa wakati wa kampeini za uchaguzi, utakuta wanatumia vituo vingi vya kuuza mafuta kutoa mafuta bure kwa ajili ya magari, pikipiki, vyombo vya moto vya aina mbali ili watu waende kwenye mikutano yao ya Kampeni.
Uchaguzi sasa ulishapita,
Zeco wanakata umeme kila siku katika mitaa mbali mbali ya Ugunja utadhani kuna mgao, ili tu wenye Generator wanunue mafuta, na mahoteli hawana namna lazima Generator ziwake
 
Mlea mada kila eneo lenye changamoto ni mkazi wa eneo hilo. Achunguzwe.
 
Mwinyi mitano tena,uzuri bara na visiwani pote Kuna CCM,ni suala la kubadilishana milio tu
 
Hivi lile deni la kipindi kile mlilimaliza?

KAZI NA MTUTU WA BUNDUKI, TUNASONGA MBELE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…