Shinyanga Kahama: Askari ajiua kwasababu ya kukosa watoto

Famous peoples who never had children.
-jesus christ.
-queen Elizabert1
-isaac newton
-Queen latifa
-Angela merkar
-oprah winfrey
-valdimir Lenin
-dalai lama
-frolence nightngale
-mother Teresa
-plato
-lawlence of arabia
-
 
Bora mke angechepuka abebe ujauzito amsingizie labda jamaa angeendelea kuishi. Uaminifu wa mke nao sio mzuri.
Anyway alale anapostahili .
 
Acha kumaliza kusema mkuu,hiyo kiprotoko za polisi inafahamika kwamba jamaa hapaswi kupata heshima ya kijeshi ktk mazishi yake,kuhusu kumsafirisha hiyo hajamaanisha kuwa jeshi LA polisi linamsafirisha LA hasha

5/5
Mkuu katika statements za uzi huu, hiko kitu kimetajwa na mara nyingi nimesikia wanaojiua kusafirishwa hasa askari wa polisi!

Kamwe anayejiua au kuuawa kwa ujambazi, hastahili kusafirishwa bali huzikwa na halmashauri tena mazishi ya aibu. Hiyo mimi nimeshuhudia mara kibao tu.

Kusafirisha pekee hata bila kuzika kijeshi ni kutoa promo za kukiuka viapo kwa wengine wenye jazba na stress zao za kipumbafu.

Askari unapokabidhiwa silaha ni kwa ajili ya kujilinda mwenyewe na kulindia raia wema na mali zao.

Haitumiki kujidhuru ama kudhuru watu wengine kwa sababu zozote zile.

Kwa mfano tulipokuwa ktk vita vya Uganda na vita kuwa tete, sheria za kijeshi zilisitishwa kwa muda na viboko kutumika kama mbadala wa adhabu zote za kijeshi.

Ilikuwa ukikosea unanyang'anywa silaha unaburuzwa mboko na njemba zilizoshiba na baadae unarudishiwa silaha yako na unaendelea na maisha na hautamani kufanya lolote na silaha yako mikononi.

Sasa nafikiria kizaz kama hiki cha visasi kwa sheria za namna hiyo, wallah mnamalizana.

Nashangaa kanuni na sheria za majeshi siku hizi kwa jinsi zinavyokiukwa kwa makusudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu hutupa hii mitihani ili tuamini jinsi alivyo na uwezo japo siyo ya kuiombea maana panahitajika nguvu kubwa sana ya maombi, kufunga na kusali mara kwa mara ili Roho Mtakatifu atutegemeze ktk imani imara.
Famous peoples who never had children.
-jesus christ.
-queen Elizabert1
-isaac newton
-Queen latifa
-Angela merkar
-oprah winfrey
-valdimir Lenin
-dalai lama
-frolence nightngale
-mother Teresa
-plato
-lawlence of arabia
-

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HABARI MPYA: Askari Polisi Gideon Clement (30) wa kituo kikuu Cha Polisi Mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye lindo Benki ya Access tawi la Kahama

Marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu kwa mke wake akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto hivyo hajaona sababu ya kuendelea kuishi

Taratibu za mazishi zinaendelea

Habari zaidi...

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa na mkewe kwa muda wa miaka mitano.

"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.

Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.
so sad aiseeee
 
...Yeye mwanaume anajiua, mkewe afanyeje??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom