Shinyanga Kahama: Askari ajiua kwasababu ya kukosa watoto

HABARI MPYA: Askari Polisi Gideon Clement (30) wa kituo kikuu Cha Polisi Mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye lindo Benki ya Access tawi la Kahama

Marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu kwa mke wake akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto hivyo hajaona sababu ya kuendelea kuishi

Taratibu za mazishi zinaendelea

Habari zaidi...

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa na mkewe kwa muda wa miaka mitano.

"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.

Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.
 
Maafande huko ktk vyuo vya mafunzo wasipewe mafunzo ya kikAtili na kutothamini utu..
Badala yake waeleweshwe thamani na maana ya uhai. Kwamb Yeye ni ni mlinzi wa amani kwa maisha yake na raia wengine...
CCM inachowafanya Ni kuwafundishA ukatili tu dhidi ya kupambana na upinzani...
Mwishowe wanajimaliza wenyewe...
Ccm mnabeba lawamA katika hili na hamuwezi kukwepa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom