Shinyanga Kahama: Askari ajiua kwasababu ya kukosa watoto

kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
6,037
2,000
Kuna jamaa yangu wa karibu alidumu ktk ndoa miaka 7 na akapata mtoto mwaka wa 8.sasa anao watoto wawili !! Maamuzi ya haraka hayajengi...jipe muda na omba ushauri .
HABARI MPYA: Askari Polisi Gideon Clement (30) wa kituo kikuu Cha Polisi Mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye lindo Benki ya Access tawi la Kahama

Marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu kwa mke wake akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto hivyo hajaona sababu ya kuendelea kuishi

Taratibu za mazishi zinaendelea

Habari zaidi...

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa na mkewe kwa muda wa miaka mitano.

"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.

Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hehemnyalu

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
706
1,000
Umesahau ile buku tano ya kusafishia viatu...
Mishahara yao mbona haina tofauti na watumishi wengine wa serikali tena wao wana faida zaidi maana hata kwenye daladala hawalipi na mapumziko (off) huwa wanapewa achilia mbali likizo ya miezi 3 kila baada ya miaka mitatu ambazo zote hizo ni fursa za kufanya shughuli zingine za kujiongezea kipato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sinyora

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
922
1,000
Kuna haja ya kuanzishwa kwa somo la Stress management kwa Askari maana tutaona na kusikia mengi. Tena afadhali amejiua mwenyewe je angetuua sisi raia wengine tena tusio na hatia

ᴵᶠ ᵀᵃⁿᶻᵃⁿⁱᵃ ʷᵃˢ ᵃ ʷᵒᵐᵃⁿ̇ ⁻ ⁱᵗ ʷᵒᵘˡᵈ ᵇᵉ ᵃ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ
nmecheka jmn wakt kuna msiba
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
6,123
2,000
HABARI MPYA: Askari Polisi Gideon Clement (30) wa kituo kikuu Cha Polisi Mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo wakati akiwa kwenye lindo Benki ya Access tawi la Kahama

Marehemu ameacha ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu kwa mke wake akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto hivyo hajaona sababu ya kuendelea kuishi

Taratibu za mazishi zinaendelea

Habari zaidi...

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa na mkewe kwa muda wa miaka mitano.

"Sababu za kujiua kwake ameeleza kwa ujumbe aliotuma kwa mke wake kwamba hana sababu za kuendelea kuishi kwa sababu hajajaliwa kupata mtoto na amekaa kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na mke wake ambaye ni mwalimu na inasemekana jana alilalamikia sana jambo hilo na alianza kuonesha dalili kwa kumtumia mkewe ujumbe wa simu akieleza kuhusu mali zake vikiwemo viwanja viko wapi",ameeleza Kamanda Abwao.

Kamanda Abwao amesema taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Muleba kwa ajili ya mazishi zinaendelea.
Wakati anajua kwa kukosa mtoto kuna wanaojiua kwa sababu ya watoto wao! Dunia uwanja wa fujo
 
Mr English

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,254
2,000
Mpumbavu huyo. Kuna mwalimu kastaafu hana mke wala mtoto. Mijihela ya pension anakula peke yake. Ye mbona hajajiua. Alijaribu kuchepuka akakosa mtoto?

Sent using my Nokia Torch
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,593
2,000
Hili suala la askari kujiua na kusafirisha maiti kwenda kuzikwa kwao limekaaje.

Hawa makamanda sasa hivi wanatumia madaraka yao vibaya, kwa kujua ama kutokujua.

Askari akifa vifo vifuatavyo; kujiua kwa njia yoyote, ama kuuawa akitekeleza uhalifu ama ujambazi, maiti yake huwa haisafirishwi.

Hicho kijeshi kinaitwa kifo cha aibu na mazishi yake hufanywa na manispaa.

Marehemu anayejiua huwa amevunja mkataba na mwajiri wake kwa kipengele cha kuacha kazi ndani ya masaa24.

Uachaji wa namna hiyo wa kazi, mfanyakazi hastahili malipo yoyote ama stahili yoyote ile.

Ninawaomba makamanda wote wa vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama wazingatie viapo vyao na waache kufanyakazi kwa mazoea.

Stahili ya kusafirisha maiti za askari na kufanya mazishi ya heshima ya kijeshi ni za wanaokufa vifo vya kawaida ama vifo vitokanavyo na kutekeleza majukumu ya kazi za kijeshi.

Hivi huyo kamanda akiulizwa ni kifungu kipi cha sheria kinachompa mamlaka ya kusafirisha maiti ya askari aliyejiua anaweza akajibu nini kwa mfano?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jul 21, 2018
90
125
Huyo alikuwa hana sababu ya msingi hasa basi tu kwa vile alikuwa na silaha mda mwingi,

nimewaza tu kama raia nao wangekuwa wanamiliki silaha isee watu wengi sana wangekuwa wanajiua maana kitaa kumejaa shida jamani.
Piere Liquid ana 40+ na hana mtoto hajatamani hata kujiua
Sababu nyepesi ingawa ndivo msiba wake ulipangika ivo rest easy mlinzi wetu wa qm
 
Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
7,141
2,000
Sababu haina mashiko...anyway mwenyezi Mungu amuweke panapostahili.
Haijakuwa na mashiko kwa sababu hujavivaa viatu vyake,shida isikie kwa jirani yako tu usiombe ikukute.

As human beings huwa tunajisahau sana tunapoona wenzetu wameshindwa pale tuliposhinda sisi ila tujue matatizo yasiyokukuta wewe yakamkuta mwenzako siyo wote wana mioyo ya kusubiri kutafuta plan B ndo maana haya yanatokea.

RIP askari!
 
Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
8,487
2,000
Haijakuwa na mashiko kwa sababu hujavivaa viatu vyake,shida isikie kwa jirani yako tu usiombe ikukute.

As human beings huwa tunajisahau sana tunapoona wenzetu wameshindwa pale tuliposhinda sisi ila tujue matatizo yasiyokukuta wewe yakamkuta mwenzako siyo wote wana mioyo ya kusubiri kutafuta plan B ndo maana haya yanatokea.

RIP askari!
Hata kama...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom