Shinyanga Kahama: Askari ajiua kwasababu ya kukosa watoto

Kazi ngumu,roho ngumu,maisha magumu
stress kidogo risasi
Anyway,kapumzike unapostahili askari.
 
Mmhh jamaniii mbona alijikatia tamaa mapema kiasi hicho,miaka 30 mwanaume??khaaa!!! Tunajua jinsi gani kukosa mtoto kunavyouma hasa kwa sisi wenye damu za kupenda watoto lakini sio kukatisha uhai kwasababu hiyo asee,.
Apumzike tuu penye stahili yake..Ova.
 
haya mambo ni vile tunayasema kwa mzaha, ila kejeli toka kwa jamii ukishindwa zihimili matokeo ndiyo haya.

kuna jamaa yangu alipata mtoto na demu 1 ila mtaani kukawa na utani kwamba ni baba wa kambo wa yule mtoto maana kuna baba halisi

siku moja alinambia adhima yake ya kwenda kwa mganga kupiga ramli kama mtoto si wake akate moto tu.Nilicheka sana

nikamtuliza akaaacha, leo mtoto amekua kafanana na jamaa balaa hadi ujinga wake kaufata (kila siku kesi kupiga wenzake)

ogopa sana masimango ya jamaa na ukiwa na uwezo mdg wa kuyakabiri.
 
Haijakuwa na mashiko kwa sababu hujavivaa viatu vyake,shida isikie kwa jirani yako tu usiombe ikukute.

As human beings huwa tunajisahau sana tunapoona wenzetu wameshindwa pale tuliposhinda sisi ila tujue matatizo yasiyokukuta wewe yakamkuta mwenzako siyo wote wana mioyo ya kusubiri kutafuta plan B ndo maana haya yanatokea.

RIP askari!
Pamoja na yote angalia ukatili alojifanyia yeye mwenyewe kujiua kwa kujipiga risasi ni zaidi ya kukosa mtoto naamini alikuwa hana huruma na hata yeye mwenyewe vipi hata angepata mtoto angemhurumia vipi pale ambapo angemletea maudhi na makwazo plan B yenyewe isn't a plan at all!
 
Hili suala la askari kujiua na kusafirisha maiti kwenda kuzikwa kwao limekaaje.

Hawa makamanda sasa hivi wanatumia madaraka yao vibaya, kwa kujua ama kutokujua.

Askari akifa vifo vifuatavyo; kujiua kwa njia yoyote, ama kuuawa akitekeleza uhalifu ama ujambazi, maiti yake huwa haisafirishwi.

Hicho kijeshi kinaitwa kifo cha aibu na mazishi yake hufanywa na manispaa.

Marehemu anayejiua huwa amevunja mkataba na mwajiri wake kwa kipengele cha kuacha kazi ndani ya masaa24.

Uachaji wa namna hiyo wa kazi, mfanyakazi hastahili malipo yoyote ama stahili yoyote ile.

Ninawaomba makamanda wote wa vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama wazingatie viapo vyao na waache kufanyakazi kwa mazoea.

Stahili ya kusafirisha maiti za askari na kufanya mazishi ya heshima ya kijeshi ni za wanaokufa vifo vya kawaida ama vifo vitokanavyo na kutekeleza majukumu ya kazi za kijeshi.

Hivi huyo kamanda akiulizwa ni kifungu kipi cha sheria kinachompa mamlaka ya kusafirisha maiti ya askari aliyejiua anaweza akajibu nini kwa mfano?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kumaliza kusema mkuu,hiyo kiprotoko za polisi inafahamika kwamba jamaa hapaswi kupata heshima ya kijeshi ktk mazishi yake,kuhusu kumsafirisha hiyo hajamaanisha kuwa jeshi LA polisi linamsafirisha LA hasha

5/5
 
Kuna haja ya polisi kuajili wanasaikolojia wengi ili kugundua na kudeal na matatizo ya kisaikolojia ya mapolisi

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom