Shibuda: CHADEMA nifukuzeni muone!

Poleni mnaoumizwa vichwa na mpuuzi kama Shibuda na bado mnabishana na FF, Vtz na wengine.

Hivi mnamfahamu shibuda!?, yeye sebule zake ni kwenye Pombe awe dar awe Maswa, sasa unategemea nini hapo!?

Lengo la Chadema lilitimia kwa kulipata Jimbo la Maswa, wakati ukifika atawekwa mtu mwafaka maswa kisha kazi, soo issue ya Shibuda ni kumzarau tu.
 
Siku zaja , wakati utatimu........., nadhani asifukuzwe, CHADEMA waendelee kumtizama ili aendelee kubwabwaja ili siku ya siku Shibuda atakuwa amesimama kama bua la mahindi, tujipe muda juu ya huyu mtu. N akama tutavuka salama hakika tutakuwa salama zaidi kuliko mwanzo.
 
nakumbuka wakati wa uchaguzi mwaka jana chadema ilionywa na baadhi ya watu humu kuhusu kuchukua mabaki ya vyama vingine. Kama kawaida wale mashabiki ambao hawaangalii mbele wa kureason wakatetea. Kuna baadhi ya members walionya specifically kuhusu shibuda lakini wale fuata upepo wakamuita shibuda "kamanda", "mpiganaji", "mwanamapinduzi" nk. Leo hii watu hao hao wamemgeuka kitu kinacho thibitisha kwamba humu ndani kuna wengi tu ni bendera fuata upepo na hawana uwezo wa kupingana na wengi ao uwezo wa kufikiria wenyewe.

Anyway ishu ya shibuda chadema ilijikoroga yenyewe. Sasa tuone watakavyo deal na hii ishu. Ila ukweli ni kwamba kuna watu walisema shibuda ni shushushu na kama anatishia kwamba wakimfukuza chadema watakiona inawezekana kasha tengeneza profile kubwa kuhusu chadema tayari kulitumia dhidi yao.
hawa jamaaa wali alibu pale mwanzoni kuto sikiliza ushauri lakini hii itakuwa challenge kwa 2015
 
Akifananisha chama hicho na utelezi wa mlenda.
Aonya kamati kuu iliyojadili haina ubavu kumtimua.
Atamba wakithubutu hilo wataona cha mtema kuni.
Adai kukataa posho ni sera za chama kilichoshinda.
Adaiwa kukutana na madiwani,Arusha wapanga siri.

Source gazeti la taifa letu:ijumaa julai 22- julai 28
www.ippmedia.com

wanyantuzu hamanazo
 
jamani chama sio familia kua baba ataamua na watot wafuate.chama kina kanuni, sheria na taratibu zake moja ya hizo ni misimamo ya kchama
(pamoja na kua kuna mawazo binfsi) lakini inapofikiwa maamuzi kua chakufanyika ni kitu fulani basi wanachama wote watafuatatu, la sivyo wao waukane uanachama wao.hivyo ndivyo ilivyo kwa CHADEMA na SHIBUDA, kama chama kimeamua kua posho zifutwe kama msimao wao, akaja mmoja akapinga huyo yupo kinyume na chama.kwa hyo anapoteza sifa ya uanachama kwa kukatisha nia juhudi za chama.
Hapa CHADEMA wafuatetu njia zilizo sahihi na watamtimua na hatofanya lolote.
 
Madiwani walishaambiwa waombe radhi. Ila Shibuda afukuzwe tu hana msaada kabisa katika chama. Naungo mkono hoja!
 
Kiburi alicho nacho Shibuda si cha kawaida ni dalili kuna walio nyuma ya pazia wanaompa ubavu.
Yanayojilia Arusha Shibuda amejidhihirisha kwa ndiye chachu.

Kwa mwendo huu huyu samaki aliyeoza atazidi kuozesha samaki wote ndani ya tenga.
Hakuna khofu ya kupoteza jimbo zaidi ya kulinda amani, umoja na utulivu ndani ya Chama.

Mchelea mwana mwisho hulia
 
kimsingi hata mimi simkubali huyu bwana kibuda.

lakini pia mimi nina amini 100% kuwa chadema ni system.

let the system do the job.
 
Nipo na wewe Mkuu 100%! Yaani asipofukuzwa atajiona wa maana sana. Huyu alishaonyesha toka mwanzo yupo the magambaz
 
huu ndo uCCM watu wanafanya ujia mnawaangalia, et mnauvumilivu!! mnavumilia upuuzi??
mtu kafanaya ujinga mpanish hapohapo ili kuondoa chances za watu kufanya upumbavu!!
tatizo la CCM wote au wengi wao ni wachafu kwa namna moja au nyingine kwa hyo hakuna wa kumpanish mwingine
kwa sababu watatibuana.
 
Kiburi alicho nacho Shibuda si cha kawaida ni dalili kuna walio nyuma ya pazia wanaompa ubavu.
Yanayojilia Arusha Shibuda amejidhihirisha kwa ndiye chachu.

Kwa mwendo huu huyu samaki aliyeoza atazidi kuozesha samaki wote ndani ya tenga.
Hakuna khofu ya kupoteza jimbo zaidi ya kulinda amani, umoja na utulivu ndani ya Chama.

Mchelea mwana mwisho hulia
 
Kiburi alicho nacho Shibuda si cha kawaida ni dalili kuna walio nyuma ya pazia wanaompa ubavu.
Yanayojilia Arusha Shibuda amejidhihirisha kwa ndiye chachu.

Kwa mwendo huu huyu samaki aliyeoza atazidi kuozesha samaki wote ndani ya tenga.
Hakuna khofu ya kupoteza jimbo zaidi ya kulinda amani, umoja na utulivu ndani ya Chama.

Mchelea mwana mwisho hulia
Tundu Lissu uko wapi?
Mbowe, Zitto, Mnyika, sugu, Marando.
Chama chetu tunakijenga kwa damu zetu kila kukicha muondoeni huyu kichaa haraka.
 
Uzuri watanzania tunajua,na dunia inajua kwa hiyo anajikaanga mwenyewe hana jipya ,maneno atakayo watukana viongozi wa chadema na chadema ni yaleyale yameongelewa toka 1995 aishie mbali
 
CDM habembelezwi mtu, kuleana ni sera ya CCM na ndiyo imefanya mpaka leo tuko gizani. Fukuza mamluki hawa na njaa zao wapeleke kwa wajinga wenzao huko magamba.
 
Kiburi alicho nacho Shibuda si cha kawaida ni dalili kuna walio nyuma ya pazia wanaompa ubavu.
Yanayojilia Arusha Shibuda amejidhihirisha kwa ndiye chachu.

Kwa mwendo huu huyu samaki aliyeoza atazidi kuozesha samaki wote ndani ya tenga.
Hakuna khofu ya kupoteza jimbo zaidi ya kulinda amani, umoja na utulivu ndani ya Chama.

Mchelea mwana mwisho hulia

Mwacheni Shibuda awafunde siasa nyie watoto wadogo, Shibuda kwa siasa hakuna anae mzidi pale cdm !
 
Back
Top Bottom