Shibuda amshambulia Tundu Lissu bungeni

Shibuda amshambulia Tundu Lissu bungeni

Acha uongo wewe wala hakuna msamiati wa nguo ya kuazima haistiri mwili! Labda huu ni wako wewe!

Sitegemei kama utayajuwa hayo, kwenu wapi?

Hata Nyota wa Kilimanjaro band kaimba hiyo, uko wapi wewe? husikilizi hata mziki? au unafikiri misamiati inaota kwenye miti?
 
Wanabodi

Kama kawaida ya John Shibuda kutaka kuonekana anajua kila kitu,amekosoa maneno yaliyosemwa na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu aliposema nguo ya kuazima haisitiri uchi.

Amesema si neno zuri kulitamka hadharani kwa sababu ni maungo ya siri ya binadamu.Shibuda ameongea hayo bungeni jioni hii akichangia hoja ya uanzishwaji wa kamisheni ya kiswahili ya afrika mashariki

My take!
Kwa nini shibuda huwa tofauti sana na ukweli wanaozungumza wabunge wenzake wa chama chake? Ana ajenda gani?
Shibuda kazidi kuwa politically Correct....neno uchi lilikuwa neno decent sana la kuelezea maeneo yote private kwa mitizamo ya jamii nyingi za kitanzania.Ghafla likafanywa kuwa na mapana madogo sana na kuwakilisha nyeti za kutolea haja,na uzazi.Shibuda alipeleka fikra kwenye zile sehemu wapendazo zitumia sana akina Malima.

Sasa siku hizi wameamua tuharamishia chumvi,tuite dawa ya mboga, kunya kukawa kujisaidia haja kubwa, uchi-utupu,zeruzeru tunaambiawa tuwaite walemavu wa ngozi, sijui na walioliw ana mba hadi ngozi kubaki na makunyanzi wataitwaje tena?

Unafikiki wetu umetupelekea kubuni maneno ya kufikirika mengi sana,halafu baadaye nayo yanakuja ktk nadharia ya uhasilia,kisha tunabuni mengine.Tunahamishwa sana kuhusu viziwi,vipovu, bubu.
 
eti hata gololi nazo zina jina tezi za kiume, Busha nalo ..jamani uswahili kazi,ndio maana akina Ponda wanakuwa kama vichaa
 
eti hata gololi nazo zina jina tezi za kiume, Busha nalo ..jamani uswahili kazi,ndio maana akina Ponda wanakuwa kama vichaa
 
Hana akili hata kidogo.huo ni msemo wa kiswahili na kama tunataka kukikuza kiswahili ni lazima tukitumie pamoja na misemo yake.
 
Ni kum-ignore tu. Anajenga mazingira ya kupokelewa na CCM maana anajua fika kuwa 2015 will not feature in CDM list! I guess

Huyu mzee anajipendekeza CCM, ni mtu wa ajabu sana, kila siku anakuwa kinyume na wenzake, mimi simsikilizagi akianza kuongea nabadilisha chanel!
 
Mbona tena kuna methali: "Nyani haoni kundule" - Iweje hiyo ya Nguo ya kuazima..........?
 
Shibuda ni ze comedy kwahiyo usimchukulie serious.

lakini mkuu unazi pembeni!.. hapo amemsahihisha au ameshambulia..?!

mtoa mada anashindwa kutofautisha kati ya kushambulia na kusahihisha....

shibuda kama mtu wa makamo mwenye busara ilibidi aseme asipo sema yeye nani atamrekibisha huyu kijana ..?
 
achana na shibuda, mental case. Yeye anawaza uchi nasikia aliwahi kuishi Zanzibar..............!!!!!!!!????????
 
Wewe acha udini kila mara akili zako ziko kwenye udini tu ndo maana mnachoma makanisa! Zitto hapa anaingiaje? wewe humjui Shibuda kuwa ni bingwa wa kuropoka? 2015 lazima ang'oke.Tumemchoka kwa kudhoofisha mapambano.
Washabiki wa CDM wengi wao wanafikiri kupitia chupa ya bia kwani Tundu ni malaika kila anachosema kiko sawa kurekibishana ndio demokrasia acheni dhana potofu kudhani viongozi wenu kila kati wako sawa au kwakuwa hatoki kupitia kanisa mbona mbowe kamsifia kikwete laiti angefanya zitto mngepata la kusema leo hapa jf
 


lakini mkuu unazi pembeni!.. hapo amemsahihisha au ameshambulia..?!

mtoa mada anashindwa kutofautisha kati ya kushambulia na kusahihisha....

shibuda kama mtu wa makamo mwenye busara ilibidi aseme asipo sema yeye nani atamrekibisha huyu kijana ..?

Shibuda alipokuwa CCM alikuwa anapingana sana na wanamagamba wenzie,Sasa yuko Chadema anapingana na wenzake, tumueleweje? Huyu ni mburula tu
 
Guys lets call spade a spade! This man doesnt fit anywhere... Neither cdm nor ccm! Akajarib cuf, sema dini kikwazo! I wish him a gud rest in wherever he go 2015....!
 
Mtu akiwa hajavaa nguo tunasema yuko UCHI, mtu akivaa vazi lisilofunika ipasavyo tunasema Amevaa UCHI, UCHI maanake ni kuangazisha sehemu isiostahili kuonekana. usipovaa shati tutasema uko UCHI, usipovaa chupi tutasema uko UCHI, UCHI sio neo gumu wala Neno baya, kulilalamikia ni kutafuta hisia za watu tu kwako.
 
kama neno uchi limeleta ukakasi kwa mswahili Shibuda katika methali hiyo je kwenye methali hii "MFICHA UCHI HAZAI' lifutwe?

Au Nyani haoni KUNDULE nayo ifutwe?
 
Kweli kabisa!

Washabiki wa CDM wengi wao wanafikiri kupitia chupa ya bia kwani Tundu ni malaika kila anachosema kiko sawa kurekibishana ndio demokrasia acheni dhana potofu kudhani viongozi wenu kila kati wako sawa au kwakuwa hatoki kupitia kanisa mbona mbowe kamsifia kikwete laiti angefanya zitto mngepata la kusema leo hapa jf
mficha uchi hazai je ni kosa pia?
 
Tatizo wana CDM hupenda kupongezwa hata kwenye makosa ukikosoa tu wewe si mwenzao wanawaza fukuza fukuza .
 
Back
Top Bottom