Shibuda amshambulia Tundu Lissu bungeni

Shibuda amshambulia Tundu Lissu bungeni

Mawazo mfilisi. Kajipange kwanza wewe bongo lala. Umbea jamii forum una degrade status ya jukwaa.
 
Shibuda ni janga kubwa kwenye kambi ya ukombozi wa Taifa letu. bora arudi magambani ili mwisho wa siku wafe maji wote na yeye akiwemo.

Arudi alikotoka hata leo, jimbo letu atuachie tumpe mwingine.
 
Shibuda ni mwanasiasa mkongwe mwenye makeke licha ya kua na umri mkubwa lakini bado anaonesha kua na nguvu kama vijana bungeni.Anatofauti kubwa na wanasiasa wengi ambao mara nyingi wanaendeshwa na misukumo ya vyama,siasa ama mabwana zao,shibuda husimamia haki hata kama chama chake hakipendi yeye kufanya anachofanya,mifano ni mingi lakini hili la jana mh lisu kutoa mifano yenye kutukana ni mojawapo.Binafsi namfananisha mh shibuda kama mesi kwani kokote lazma ang'are.CCM walipo mchakachua lakini kupitia CDM ameweza kutetea kiti chake.Naamini hata akihamia CCJ lazma atashinda na kurudi mjengoni.Hawa ndio aina ya wanasiasa tunao wahitaji nchini licha ya watu wasio na mapenzi mema kuwachukia kwa sababu zao binafsi.Hongera sana Mh shibuda

CDM ndio mwisho wake wa kung'ara,labda arudi Gambani apewe ubalozi kabla ya 2015.
 
akili za kushikiwa utazijua, yaani mwanaJF kutokota katika zero degree ni aibu sana.

Kuwa mwanaJF ni zaidi ya form six ya kata bana!!=

funguka vizuri hujaeleweka.
 
Mawazo mfilisi. Kajipange kwanza wewe bongo lala. Umbea jamii forum una degrade status ya jukwaa.

Hujaeleweka,unachangia mada au unarumbana na nani kwa sababu hakuna uliyem-quote.jipange upya halafu uje.
 
Shibuda ni shabiki na mpenzi mkubwa wa Kiswahili. Kwa upeo wa Lisu kwenye Kiswahili, neno 'tvko' ni kali zaidi ya neno 'uchi'. Hivyo akaamuwa kutumia neno 'uchi' badala ya 'tvko'. Sasa inabidi Shibuda atueleze, ni neno gani mbadala kupunguza ukali wa neno 'tvko'. Wazee wetu wanajuwa tafsida zote, lakini waliacha maneno makali kwenye methali zetu kwa sababu za msingi kabisa. Pale mtu anapotaka kufikisha strong message hayo maneno hayanabudi kutumika. Si makosa. Kama Lisu angeitumia hiyo methali kama ilivyo ''nguo ya kuazima haisitiri matvko'' nadhani angekuwa safe side zaidi. Pia tunaweza kujadili kama dhana ya Lisu ni sahihi, kwamba neno 'uchi' laweza punguza ukali wa neno 'tvko'.
 
kaka usishangae hizi ndizo kazi alizotumwa aje awafanyie hawa jamaa wa chadema
 
shibuda ni mamuluki hakuna ambaye halifahamu hili na chadema wanatakiwa walifahamu hili otherwise atakuja kuleta matatizo hapo baadye
 
Ni kawaida ya Magamba kudandia hoja zisizowahusu.Gamba linakuwasha wewe.

Wewe gwanda litakua linakubana ni bora ukae kimya.Lazma wewe utakua ni yule ambaye matusi ndio kiunganishi haiwezekani mtu atoe matusi bungeni umtetee kisa mwana chama mwenzio,huo ni ujuha!
 
Wewe gwanda litakua linakubana ni bora ukae kimya.Lazma wewe utakua ni yule ambaye matusi ndio kiunganishi haiwezekani mtu atoe matusi bungeni umtetee kisa mwana chama mwenzio,huo ni ujuha!

Toa taarifa BAKITA wafute methali zote zinazotamka matusi kama unaweza,Kilaza mkubwa wewe.
 
sijaona hoja hapo yakuleta hapa, swala lililokuwa mezani ni kuanzasha kamisheni ya kiswahili sasa kisa Tundu ni CHADEMA mwenzake ndo asimrekebishe......we akili yako kila kitu inawaza siasa tu
 
cdm itaangamia kama haitakubali kukosolewa ndani na nje ya chama. Hata muwa huwezi kuula tu unasikia utamu na usikutane na fundo. tafakari chukua hatua.
 
washabiki wa cdm wengi wao wanafikiri kupitia chupa ya bia kwani tundu ni malaika kila anachosema kiko sawa kurekibishana ndio demokrasia acheni dhana potofu kudhani viongozi wenu kila kati wako sawa au kwakuwa hatoki kupitia kanisa mbona mbowe kamsifia kikwete laiti angefanya zitto mngepata la kusema leo hapa jf

acha udini wewe mtz. Mwenye fikra ndogo ya chekechea.
 
sijaona hoja hapo yakuleta hapa, swala lililokuwa mezani ni kuanzasha kamisheni ya kiswahili sasa kisa Tundu ni CHADEMA mwenzake ndo asimrekebishe......we akili yako kila kitu inawaza siasa tu

Kwani aliyoongea Shibuda siyo siasa? Au aliyoongea Lissu sio siasa,shughuli iliyokuwepo bungeni sio siasa? Kama hujui siasa bora ukae kimya
 
cdm itaangamia kama haitakubali kukosolewa ndani na nje ya chama. Hata muwa huwezi kuula tu unasikia utamu na usikutane na fundo. tafakari chukua hatua.

CDM haiwezi kukataa kukosolewa ni moja kati ya njia ya kujenga chama,lakini mnaposhambuliana nyinyi kwa nyinyi inaleta makundi kama ilivyo kwa magamba hivi sasa,Kafulila anajua vizuri.Kwa mfano leo asimame Pinda na kumshambulia Bosi wake Jk hadharani sidhani kama CCM itatulia na Pinda atawajibishwa tu.
 
Back
Top Bottom