Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Shibuda aishangaa demokrasia ya CHADEMA

Mmeshawahi kuona mtu anaenda kutangaza kugombea kwenye kambi nyingine zaidi ya ya kwake na kuomba mshhenga wake awe "adui yake"? Huyo mtu anapaswa ashughulikiwe kabla hajachafua zaidi. Kuna somo kubwa kwa CDM kupokea magamba kwa tahadhari

Tunawaambia viongozi kwamba uvumilivu wa wanachama sasa umefikia mwisho.Shibuda afukuzwe haraka iwezekanavyo...
 
Bora CDM waanze kukanyagana wenyewe kwa wenyewe.
 
Bravo Chadema leaders, mwacheni shibuda ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe mwisho wa siku wananchi watapima. Hina haja ya kumfanya lolote kwa sasa
 
" Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya kikao cha CCM tangu juzi zinasema Shibuda, ambaye alihama CCM na kujiunga CHADEMA mwaka 2010, alivishambulia vyama vya upinzani, kiasi cha kuwaacha midomo wazi Wana CCM wenyewe.

Mmoja wa vigogo wa CCM waliozungumza na gazeti hili juzi usiku alisema kwamba baadhi ya maneno aliyotumia Shibuda dhidi ya CHADEMA yalikuwa makali kiasi kwamba hata katika mikanda yao ya video wanazotumia kwa matangazo ya vyombo vyao vya habari, ilibidi wayahariri au kuyakata."

Chanzo: Tanzania daima

Hayo ndo yaliyojiri dodoma
 
Amakwelo Shibuda jembe, kila mtu ndani ya CDM anamgwaya. Mbona Slaa hamfukuzi kama anavyowafukuzaga viongozi wa kada nyingine?
 
Kule kuna Lusinde, huku kuna shibuda! Ngoma droo, tunahitaji hosp ya vichaa ya viongozi (kama vip flani hivi)
 
Amakwelo Shibuda jembe, kila mtu ndani ya CDM anamgwaya. Mbona Slaa hamfukuzi kama anavyowafukuzaga viongozi wa kada nyingine?

Wakupakatwa wanajulikana kwa uzito wa post zao.

Imany john
14/05/2013
 
habari hii ni ngumu sana na inaumiza kichwa, wanasheria mnisaidie hili, je akifukuzwa uanachama hatakua mbuge? na itasumbua chama kisheria? kama yap... hafukuzwe tu
 
Kwangu mimi Shibuda hana hadhi ya kujadiliwa kabisa. The man has's long past his expiry. Na kinachonishangaza ni kwa CCM kuendelea kumtumia kama shushushu wao ndani ya CDM! Shibuda? Sana sana BAVICHA wanaweza kufanya kazi moja once and for all, wamtangaze Shibuda ni enemy of M4C then waendelee na mambo mengine ya maana. Wapiga kura watahangika naye.
 
Huyo jamaa akigombea urais atakuwa kama hapa chini.
.
"HERI KIJANA MASKINI MWENYE HEKIMA KULIKO RAIS MPUMBAVU".
 
ubavu wa kumfukuza hamnao, jaribuni muone atakavyowavua nguo cdm.
 
Demokrasia ndani ya CDM ni kama hii tunayoishudia kwa wapiga debe wake hapa JF.
 
Kama chadema wanaamini wana kazi ya msingi mbele yao, hawana sababu za kulumbana na mhe. shibuda. wamwache aendelee kutumia haki yake ya msingi na kidemokrasia kutoa mawazo yake. haijalishi anayatolea wapi. kumwingilia kwa kigezo chochote kila ni uthibitisho wa chadema kutokuwa na focus na vile vile kuingilia kati uhuru wa mtu.
 
Amakwelo Shibuda jembe, kila mtu ndani ya CDM anamgwaya. Mbona Slaa hamfukuzi kama anavyowafukuzaga viongozi wa kada nyingine?

Shibuda akifukuzwa ni kumuongezea umaarufu, jinsi umaarufu wake unavyoporomoka hadi CCM wenyewe wanamshitukia ingawa yeye mwenyewe kwa ujinga wake anaona ni sifa.
Muda si mrefu atajikuta anaropoka kumuomba JK amteue Balozi.
 
Back
Top Bottom