Sheria ya Talaka TZ ilegezwe au isilegezwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Talaka TZ ilegezwe au isilegezwe?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mzee Mwanakijiji, May 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni lazima watu wanaovunja ndoa wawe na sababu ya msingi? Kwenye State kama Michigan (US) wana kitu kinaitwa "no fault divorce" yaani haiitajiki kuwepo kosa kwenye ndoa kumfanya mtu atake divorce. Basically mtu anaweza kuwa divorce for any reason or for no reason at all. Je katika Tanzania kama hiyo inahitajika, itasaidia, au itachochea talaka?

  Hadi hivi sasa ili mtu aweze kupata talaka kuna masharti magumu na ambayo yote yanataka sababu ya kuhalalisha talaka na hata ikiwepo sababu ni lazima mfuate utaratibu wa usuluhishi n.k n.k

  Katika Tanzania hivi sasa talaka haiwezi kutolewa mpaka mahakama iridhike kuwa ndoa haiwezi kutengamaa tena na kwamba ndoa imevunjika pasipo shaka ili kuthibitisha hili sharti muhimu la kisheria, mdai talaka anapaswa kuonyesha mahakamani mambo kadhaa yanayoweza kuvunja ndoa. Si lazima aoneshe yote bali hata mojawapo likiwa na uzito ambao utaridhisha mahakama. Lakini kimsingi ni lazima kuwe na sababu ya kutosha.

  1. Talaka ya Kiislam
  2. Desertion including constructive deserttion
  3. Cruelty...hapan ni mambo mengi yanayotafsiriwakuwa ni ukatili
  4. Kubadili dini
  5.Kifungo cha muda mrefu
  6. nadhani hata ugonjwa kama kichaa

  Sasa inakuwaje pale mtu ambapo anajua kua ndoa yake kweli imefikia magogoni? Afanye nini? aendelee kusumbuka miaka nenda rudi kutafuta talaka yake?

  Maana hata kama mtu anataka kuoa au kuolewa tena anajikuta anashindwa kwa sababu hata potential wachumba wanaachia mbele ya safari kwani talaka haiji na muda unapita. Lakini ikiwekwa sheria ya kusema kuwa yeyote kati yenu anaweza kuinitiate divorce proceeding na ya kuwa at the end divorce itatolewa hata kama mwingine hataki itasaidia watu kuwa waangalifu kwani watajua hawawezi kuchezea ndoa kwani inaweza ikavunjwa wakati wowote?

  Open floor.
   
 2. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kwa shida tulizonazo hii itachochea ndoa kuvunjika hasa kwa vijana wa sasa!
   
 3. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mnh kama mmoja hajiamini,hatakuwa na amani,muda wote atakuwa na wasiwasi ataachwa wakati wowote,hii inaweza leta pressure,msongo wa mawazo lol
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Katika taasisi za kale ndoa ni mojawapo. Jamii zote duniani zilijitahidi kuhakikisha ndoa inakuwepo kwa kujua kuwa hakuna ndoa iliyo kamili kwa asilimia mia. Ni kweli kulegeza sheria kama unavyosema kutasaidia watu kuwa waangalifu, lakini kizazi cha sasa hiyo itachochea sana uvunjikaji wa ndoa. Endapo ndoa imefika'magogoni' kuna sababu zilizoifikisha hapo na kama sababu hizo hazikubaliki basi ipo nafasi kwa wakati huo kutengeneza sababu zitakazokubalika, na hii itasaidia wanaowahi potential wachumba kufikia malengo.

  Nadhani ni muhimu watu wakaelewa kwanini wanaoa na wanamuoa nani na kwa dhati gani. Itasaidia kuwa na ndoa stable,lakini watu kama wataoana kwa mtindo wa 'hollywood' mwisho utakuwa huo huo.

  Hili la kulegeza sheria, Marekani na Ulaya linawaletea matatizo sana na kila mara wamekuwa wanatunga vijisheria indirect ili kuhakikisha wanaoamua kuvunja ndoa basi iwe ni lazima na si 'ndoa for covinience'. Kuna nchi zinasema kuvunja ndoa ni mwaka mmoja baada ya ku 'separate', zingine zinaweka masharti ya ulezi n.k. ikiwa ni njia ya kuhakikisha kuwa kuvunjika kuna msingi wa maana.

  Kwa jamii yetu ambayo ndoa haiwezi kuvunjika kwa sababu mume hakuleta maua siku ya birth day, nadhani tuendelee na taratibu zetu na ikiwa ni lazima kuvunja basi na iwe hivyo. Nisingependa tuige mambo ya nje kwasababu mazingira yetu ni tofauti kabisa na nina amini sisi bado tunabeba thamani ya ndoa kuliko jamii nyingi za ulaya na marekani.
  Ama sheria za ndoa ziachwe kama zilivyo, kama yupo aliyechoka tu basi atafute sababu ambazo zipo nyingi.
   
 5. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hii nafikiri kwa tanzania itakuwa si sahihi, itapelekea watu wengi kuweka dhana kuwa ndoa ni jambo jepesi, naweza kuoa leo na kuacha kesho,suala zima la uvumilivu na kusameheana ktk maisha ya ndoa litakuwa matatani, watu wanaweza kuwapa talaka wenzi wao ili kukwepa majukumu yao ya kifamilia .....
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Lakini kwanini ionekane kana kwamba sheria inalazimisha watu wasiopatana kuendelea kuwa pamoja katika ndoa zilizoshindwa?
   
 7. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mzee mwanakijiji,
  Ndoa is an institution which was founded by God himself and since then African community has been culturally maintaining this institution very strong. Labda kabla hujaleta mjadala wa sheria za ndoa na talaka ni vizuri tena umwage hapa jamvini procedure wanazofuata hao watu kabla ya kufunga ndoa na kuona kama zina-relate na za kwetu. Hapa kwetu najua ndoa inajumisha zaidi ya wazazi wa pande zote mbili na linakuwa jambo la koo mbili kuungana na kwa hiyo watu woote hawa wanajisikia kuwa na wajibu wa kulinda ndoa tarajwa! I think for Michigan may be wako sawa since kijana na binti wanaweza kufungia ndoa popote na sidhani kama details za milolongo kama hii yetu zinahusishwa.
  Na nido maana vijana wa ndoa za makaratasi huwa wanazimudu bila madhara makubwa kwa muda kitambo kisha wanaendelea na mambo yao hapo ughaibuni wakisha pata papers
   
 8. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red mkuu
  Wengi wa hapo wamarekani hulichukulia hivyo! huu ni mtazamo wangu!
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 20, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  I am a big proponent of no-fault divorce and I think the law(s) should be eased. It is long overdue!

  Here is my rationale. After being together for so long people (couples) do grow apart and their love for each other, bond, and romance starts petering out. This is a fact though I don't mean to imply that every couple is like that. But at least the majority of them have that experience at some point in their matrimonial life together .

  That weakening of their love may push one or both husband and wife to commit adultery which is illicit in many people's eyes. So if this is the case why then cling on to a marriage that you are not wholeheartedly committed to? I see no point whatsoever.

  If you are tired with your husband or wife for whatever reason or no reason then I think you should be able to free yourself from that marriage by legal recourse. You shouldn't be required to show any evidence of breach of the marital contract by your spouse. Irreconcilable difference(s) should suffice.
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Nikikuchoka tu
  nakutumia sms tatu tu kwenye simu

  ni ttalaka tosha....

  Hiyo ndo ilivyo nchi za kiarabu...

  Na bongo iwe hivyo...
   
 12. Rangi Mbili

  Rangi Mbili Member

  #12
  May 20, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is too dangerous,
  why did you marry in the first if you knew you could end up in love-less marriage after sometime??

  African countries should not accept these kind of laws, we are still poor. At least in USA, one can afford to live as a single parent and survive well, not so in Tanzania particularly, where there is still so much dependence among 'married' families. Putting these easy-to-break laws will jeopardise our generation in the years ahead.
   
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Sheria ibaki hivyo hivyo. Ingekuwa ku divorce ni rahisi nadhani sasa hivi ningekuwa single. Na labda ningekuwa najutia hasira zangu. Niliwahi kugombana vibaya sana na hubby nikaenda kuomba ushauri kwa lawyer (friend of mine) kuhusu utaratibu wa kufuata nipate talaka yangu. Procedure alizonambia zilinifanya nigairi. Na leo hii tunaishi vizuri na tumeshasahau yaliyotokea.

  Nimejifunza kwenye marriage life talaka si kitu cha kukimbilia. Ugomvi ni wa mpito na ukiisha mahusiano yanachipua upyaaa!
   
 14. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  And that will increase population hence poverty. Maana mtu anapoacha mke au kuachika maanake anaenda kuanza upya familia. Kwa hiyo anaanza kuzaa upya. Wakati angekaa na mke mume mmoja angejizalia watoto wawili. Sasa with new wife anaongeza wengine wawili. Na wife with new husband anaongeza wengine watatu.


   
 15. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu watu waliopendana ni ngumu kuchukiana. Sheria inawapa nafasi ya kujifikiria. Unless ndoa hiyo iwe ilikuwa ya mkeka. But if there was love, sheria imeona possibility of reconcilling ipo. Na tuna ushaidi wa watu ambao wameweza kuyashinda majaribu ya ndoa na sasa ndoa zao ni mifano ya kuigwa.
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  May 20, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  This is the basic question.
  Matrimony as an institution is governed by the laws, regulations and ethics. Millions have benefited as opposed to minority who want to make use of institution as a legal organ to justify their interest.
  For those who are skeptical they should not marry in first place, instead they have to take another path which is legally recognized i.e. live as common law. The common law is the simple way of living together if the couple is uncertain.
  The couple can marry or walk away without infringement or any legal string attached.
   
 17. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280

  Kwenye issue ya kugawana mali itakuwaje? Tutafuata the same old law or will have to create a new law as well?
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  May 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Things do happen and no one can predict the future. Do you know how many people are unhappily married? It's a lot! If all of those unhappily married people would have known beforehand that their marriage would at some point sour, I doubt if many of them would have gotten married. But most people don't live their lives like that. Most people live their lives optimistically. But when things turn out to be not as they were expected people have to adapt.

  Very weak argument! So basically what you are saying is that someone should hold on to an unhappy marriage just because our society is poor? That just doesn't make sense. Most people I think would trade an unhappy marriage life for a hard but happy single-life in a heartbeat. Just think about it, who wants to live in misery?
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  May 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hakuna ubaya kuzifanyia marekebisho sheria zinazohusu ugawanaji wa mali ili mradi ugawanaji huo ni wa haki. Kama sheria zilizopo ni za haki basi hakuna ulazima wowote wa kuzibadilisha. Kwa hiyo kwa ujumla kitu cha msingi hapa ni haki tu.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  May 21, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Huyo ni wewe. Wengine wana mtazamo tofauti na wana matakwa tofauti. Ili mradi inahusu maisha yao binafsi basi sioni kwa nini sheria isiwasitiri na wao.
   
Loading...