SUASO
JF-Expert Member
- Oct 19, 2017
- 770
- 1,196
Safi kabisa mkuu!!!Seriously sikumwamkia wanielewe wasinielewe watajua wenyewe... Mimi sio wa jamii yao mila ni tofauti
Sent using Jamii Forums mobile app
Safi kabisa mkuu!!!Seriously sikumwamkia wanielewe wasinielewe watajua wenyewe... Mimi sio wa jamii yao mila ni tofauti
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni wazee wafuate tu, jishushe. Kikubwa zaidi msome unayemsalimia yeye ni wa namna gani, kama ni wa kumpungia mkono kwa mbali mpungie tu. Kama ni wa kumfuata jongea kwake.Naamini mko poa humu ndani.
Leo mida ya asubuh wakati naelekea kwnye miangaiko yangu ya hapa na pale bhana, nikapita mita ya karibu na nyumba anayoishi Mzee wetu mwenye nyumba.
Sasa kikukweli alikua mbali sana kiasa cha distance ya kama mita 25 au thelathini tokea nipokua napita Mimi.
Nikaona hapa kama ni kutoa salam ili aiskie bs nipaze sauti sana ndo tuskilizane...basi nikaona sio kesi nikapita kikauzu
Sasa kumbe yeye kanichora tu.
Nimerudi sa hv geto nimemkuta nje ya nyumba yetu aliotupangisha anafanya Fanya usafi.........nikamsalimia...akanikaushia....nikarudia tena kumsalimia aiseee..
Nikashangaa Mzee kawaka "unanisalimia nin wakat asubuhi umenipita bila salam,, siku hz umekua na dharau sana, hvo vimiambili mia mbili vinakuchanganya"
Yani kwa kifupi aliongea kinoma....nikaona niingie zangu ndani tu, ile nimeshangaa sana,
Sasa sijui nyie watu wa humu ndani katika swala LA kutoa shikamoo mnakua mmejiwekea utaratibu gani.
Mana mim mtu akiwa mbali sana siwezaji kupaza sauti kumsalimia kama natangaza salam bhana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tamko "shikamoo" halileti dhambi wala thawabu ni utamaduni uliyojengeka katika sisi miongoni mwa wanajamii, kwa wengine lina maana kwa wengine halina maana. Ndivyo jamii ilivyo, cha msingi ni kutambua mahala husika.Yeah niko tanga na hiki usemacho huku ndio utamadun kiasi nimezoea,sasa wengine ukiwaambia hiyo salam wanakuona unewadharau wanataka shikamoo wakat haina mana
Sidhani kama umeelewa ulochonikwot! Relax sjakwazika.Tamko "shikamoo" halileti dhambi wala thawabu ni utamaduni uliyojengeka katika sisi miongoni mwa wanajamii, kwa wengine lina maana kwa wengine halina maana. Ndivyo jamii ilivyo, cha msingi ni kutambua mahala husika.
Samahani kama nimekukwaza. Siku njema.
Ok mapungufu ni ya kwangu, siku njema.Sidhani kama umeelewa ulochonikwot! Relax sjakwazika.
sipendi MTU anisalimie "vipi hali"nahisi imekaa kiswahili swahili!!
Teh teh teh. Mkuu hilo la kuamkua shemeji yako mdogo lina ukakasi.Niliwahi kuchumbia Mwanza... Eti kisa mchumba wangu ni mdogo ndio nalazimishwa kumwamkia kaka yake katoto kadogo hakalingani hata na mdogo wangu wa 3!
Nikamwambia huyo aliyewaletea hiyo shikamoo aliwapa masharti kwa mdogo amwamkie mkubwa sasa nitaanzaje kukuamkia wewe mdogo wangu wa 4?
Sent from my TECNO-M3 using JamiiForums mobile app
Hiyo issue shikamoo,umenikumbusha kipindi hicho ndio nimekuja Mwanza, niliwakuta wazee wa kabila kisukuma wamekaa wengi wengi wanaongea story zao, mie sasa nikawaamkia "SHIKAMOONI WAZEE", wale wazee wakaniangalia kwa dharau na mshangao, na mie nikawashangaa. Wakaniita, wee binti hebu njoo hapa, nilivyofika wakanihoji "SISI UMETUONA NI TENGA LA NYANYA ETI?" nikamuuliza kwanini mzee unasema hivyo? akajibu "hivi sisi unaweza kutupatia shikamoo ya jumla kwa wote?"
Kumbe walitaka niwasalimie mmoja mmoja, tena kwa kupiga magoti, kwa mfano:
1. Shikamoo Mzee Mabula
2. Shikamoo Mzee Manoni
3. Shikamoo Mzee Mpuya
4. Shikamoo Mzee Masanja
yaani hadi wote waishe kila mmoja na shikamoo yake, tena kwa kumtaja jina!!!! (ukiwa umepiga magoti)
et matenga ya nyanya....daaahh kweli kila sehemu na taratibu zake....sasa ndo kama unawahi basi stendi ndo linakupigia honi itakuaje hizo salam mpka uzimalize!hahahahahah![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
et matenga ya nyanya....daaahh kweli kila sehemu na taratibu zake....sasa ndo kama unawahi basi stendi ndo linakupigia honi itakuaje hizo salam mpka uzimalize!
Inategemeana na mda huo ni mda gani na unaelekea wapi? Wengine mishe mishe zetu zina depend sana time....ukichelewa sekunde tu unalala njaaaKama ni wazee wafuate tu, jishushe. Kikubwa zaidi msome unayemsalimia yeye ni wa namna gani, kama ni wa kumpungia mkono kwa mbali mpungie tu. Kama ni wa kumfuata jongea kwake.
AiseeeTamko "shikamoo" halileti dhambi wala thawabu ni utamaduni uliyojengeka katika sisi miongoni mwa wanajamii, kwa wengine lina maana kwa wengine halina maana. Ndivyo jamii ilivyo, cha msingi ni kutambua mahala husika.
Samahani kama nimekukwaza. Siku njema.
Kwa nini ushangae mkuu.....hiyo ndo asili sahihi ya neno shikamoo...."nipo chini ya miguu yako" ...... Shikamoo hutegemea pande mbili, kiutamaduni wetu ni katika umri mdogo kwa mkubwa, lakin waanzilishi walimaanisha katika upande wa......yule aliekuzid cheo au maisha au anaekutawala kivyovyote vile mpe shikamooSiku Rais Magufuli akiwa Morogoro akampigia Dr. Kitila Mkumbo kwa simu huku tukisikia mazungumzo kwenye loud speakers, nakumbuka Mkumbo alimuamkia shikamoo, kuna maswali mengi nilijiuliza toka siku ile.
Nitarudi baadae kujiekezea zaidi.
Majadiliano ya namna hii ni muhimu sana kwenye jamii zetu, tusiyabeze.