Sheria ya salamu ya "Shikamoo"

Sheria ya salamu ya "Shikamoo"

Huku tunavyoishi ni nadra kukuta mtu akusalimie bila kukuanbia assalam alayqum, nikajikuta mazoea yamejengeka kiasi sion maana ya shikamoo, lakin wengine usipowapa shikamoo ukawapa assalam alayqum wanaona huwaheshim na kuwadharau

Binafsi siwez kusalimia kwa mbali labda nipunge mkono mtu yule ajue nimepa ishara tu ya salam
Napendaga sana kutumia Assalam aleykum.....lakn Mara nyingi nikiwa kwetu Tanga ndo salam yetu afu fresh tu....Ila huku kusini mmmhhh....ni shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah niko tanga na hiki usemacho huku ndio utamadun kiasi nimezoea,sasa wengine ukiwaambia hiyo salam wanakuona unewadharau wanataka shikamoo wakat haina mana
 
Kumbe tupo wengi, niliazimia kutotumia hii salaam na nilianzia nyumbani kwa wazee nashukuru walinielewa
Umeamkaje
Umeshindaje
Habari etc
(Kutegemeana na mahusiano na rika)
Niliwahi kuchumbia Mwanza... Eti kisa mchumba wangu ni mdogo ndio nalazimishwa kumwamkia kaka yake katoto kadogo hakalingani hata na mdogo wangu wa 3!

Nikamwambia huyo aliyewaletea hiyo shikamoo aliwapa masharti kwa mdogo amwamkie mkubwa sasa nitaanzaje kukuamkia wewe mdogo wangu wa 4?

Sent from my TECNO-M3 using JamiiForums mobile app
 
Naamini mko poa humu ndani.

Leo mida ya asubuh wakati naelekea kwnye miangaiko yangu ya hapa na pale bhana, nikapita mita ya karibu na nyumba anayoishi Mzee wetu mwenye nyumba.

Sasa kikukweli alikua mbali sana kiasa cha distance ya kama mita 25 au thelathini tokea nipokua napita Mimi.

Nikaona hapa kama ni kutoa salam ili aiskie bs nipaze sauti sana ndo tuskilizane...basi nikaona sio kesi nikapita kikauzu

Sasa kumbe yeye kanichora tu.

Nimerudi sa hv geto nimemkuta nje ya nyumba yetu aliotupangisha anafanya Fanya usafi.........nikamsalimia...akanikaushia....nikarudia tena kumsalimia aiseee..

Nikashangaa Mzee kawaka "unanisalimia nin wakat asubuhi umenipita bila salam,, siku hz umekua na dharau sana, hvo vimiambili mia mbili vinakuchanganya"

Yani kwa kifupi aliongea kinoma....nikaona niingie zangu ndani tu, ile nimeshangaa sana,

Sasa sijui nyie watu wa humu ndani katika swala LA kutoa shikamoo mnakua mmejiwekea utaratibu gani.
Mana mim mtu akiwa mbali sana siwezaji kupaza sauti kumsalimia kama natangaza salam bhana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu.
Ifike mahali kengele la adha ya kuishi kwenye nyumba za waswahili lilie ubongoni mwako, kama haukuwa na wazo la kuandaa mustakabali wako, basi hiyo ni fursa, lianzishe sasa, maana haujachelewa bado.

Umiliki wa kitu chochote huanza na wazo kwanza, kisha Mungu hufungua neema zake na hakuna kitu kilichowezwa na mwenziyo, wewe kukakushinda!

Kuna dharau ama manyanyaso mengine unaweza kuyapata mtu, yakawa ndiyo mwanzo wa mabadiliko ya mfumo mzima wa maisha yako.

Hiyo umeipata ni kiashiria sahihi cha tabia ya uswahilini.

Amekuwa ni baba yako mzazi huyo anayestahili kuamkiwa hata kwa kufunguzwa ili kumjulia hali?

Unaishi kwake kwa mkataba wa kulipana kodi, si vinginevyo na shikamoo yako haikupatii taafifu ya kodi.

Huyo anataka kukupandilia kisogoni umuabudu, kwa cheo cha baba mwenyenyumba ili aendelee kukunyanyasa!

Wewe fanya mambo yako kama kawaida, usimjali na wala asikukwaze ili mradi unamlipa kodi yake.

Fuata utaratibu uliojiwekea, namna ya kuamkia mtu kwa distance inayofaa kuwasiliana.

Usimuwekee kinyongo wala asikubadilishie mfumo wa uhuru wako na epuka naye mazoea.

Hizo 'shikamoo' kila mtu anaitafsiri kichwani mwake anavyotaka yeye.

Nikupe mfano, siku moja nikiwa mtumishi wa serikali kwa hadhi ya wilaya, alifika ofisini kwangu mbabu, anayenizidi kiumri kama miaka15hivi, akanitandika shikamoo!

Sikuvumilia nikamuuliza kwanini aninyenyekee kwa salamu hiyo, wakati aliyestahili kuamkiwa ni yeye anayenizidi umri?

Yule mzee wala hakumumunya maneno, akanieleza kuwa shikamoo aliyonipiga nayo usoni si ya umri bali ni ya ofisi na madaraka niliyonayo.

Akaongeza kuwa, vinginevyo nisingekuwa na cheo pamoja na ofisi, kamwe nisingelipata hicho kionjo toka kinywani mwake!

Nilishangaa sana na kugundua kuwa salaam ya shikamoo haina tafsiri moja yenye kueleweka kama watu wengi tunavyoichukulia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana muwe mnwaamkia wakubwa wenu.Mmejitafutiza vijisentensi ili msiamkie wakubwa?Muwaamkie tu,hamna namna!Hata hivyo,kwani ukisema shikamoo muzee wangu iko mbaya gani?Narudia,there is no excuse before greeting an elder with a big shikamoo and hence your knees bent a little if at all you're a female!
 
Hahahaaa we jamaa ndo umeamua kunikaziaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu.
Ifike mahali kengele la adha ya kuishi kwenye nyumba za waswahili lilie ubongoni mwako, kama haukuwa na wazo la kuandaa mustakabali wako, basi hiyo ni fursa, lianzishe sasa, maana haujachelewa bado.

Umiliki wa kitu chochote huanza na wazo kwanza, kisha Mungu hufungua neema zake na hakuna kitu kilichowezwa na mwenziyo, wewe kukakushinda!

Kuna dharau ama manyanyaso mengine unaweza kuyapata mtu, yakawa ndiyo mwanzo wa mabadiliko ya mfumo mzima wa maisha yako.

Hiyo umeipata ni kiashiria sahihi cha tabia ya uswahilini.

Amekuwa ni baba yako mzazi huyo anayestahili kuamkiwa hata kwa kufunguzwa ili kumjulia hali?

Unaishi kwake kwa mkataba wa kulipana kodi, si vinginevyo na shikamoo yako haikupatii taafifu ya kodi.

Huyo anataka kukupandilia kisogoni umuabudu, kwa cheo cha baba mwenyenyumba ili aendelee kukunyanyasa!

Wewe fanya mambo yako kama kawaida, usimjali na wala asikukwaze ili mradi unamlipa kodi yake.

Fuata utaratibu uliojiwekea, namna ya kuamkia mtu kwa distance inayofaa kuwasiliana.

Usimuwekee kinyongo wala asikubadilishie mfumo wa uhuru wako na epuka naye mazoea.

Hizo 'shikamoo' kila mtu anaitafsiri kichwani mwake anavyotaka yeye.

Nikupe mfano, siku moja nikiwa mtumishi wa serikali kwa hadhi ya wilaya, alifika ofisini kwangu mbabu, anayenizidi kiumri kama miaka15hivi, akanitandika shikamoo!

Sikuvumilia nikamuuliza kwanini aninyenyekee kwa salamu hiyo, wakati aliyestahili kuamkiwa ni yeye anayenizidi umri?

Yule mzee wala hakumumunya maneno, akanieleza kuwa shikamoo aliyonipiga nayo usoni si ya umri bali ni ya ofisi na madaraka niliyonayo.

Akaongeza kuwa, vinginevyo nisingekuwa na cheo pamoja na ofisi, kamwe nisingelipata hicho kionjo toka kinywani mwake!

Nilishangaa sana na kugundua kuwa salaam ya shikamoo haina tafsiri moja yenye kueleweka kama watu wengi tunavyoichukulia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaaah mkuu hapa umenitemea madini mujarabu kabisa.....though tumeanza maisha mda si Mrefu but ni muhimu sana kufocus kwnye kupata makazi ya jumla yaliotengenezwa kwa jasho zetu ili tuishi kwa aman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kuchumbia Mwanza... Eti kisa mchumba wangu ni mdogo ndio nalazimishwa kumwamkia kaka yake katoto kadogo hakalingani hata na mdogo wangu wa 3!

Nikamwambia huyo aliyewaletea hiyo shikamoo aliwapa masharti kwa mdogo amwamkie mkubwa sasa nitaanzaje kukuamkia wewe mdogo wangu wa 4?

Sent from my TECNO-M3 using JamiiForums mobile app
Sasa huo ndo ukilitimba original kabisa aisee Daah...ko mpka Leo unampa shikamoo hyo mtoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah niko tanga na hiki usemacho huku ndio utamadun kiasi nimezoea,sasa wengine ukiwaambia hiyo salam wanakuona unewadharau wanataka shikamoo wakat haina mana
True....nikiwa huko huwa sionagi wa kuskia makelele ya shikamoo....ya mwendo wa A/aleykum tu....huwa najiskia faraja sana......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakua na matatzo yake huyo
Alaf kuna hizi adabu za kiislam "kutoa salam kwa sauti kubwa kwa mtu alie mbali si katika adabu" ni vyema umsogelee au utafute wakati mwingin ukutane nae ndipo mpate kupeana salamu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm mwalimu wangu chuoni alitaka hata kupigana siku moja baada ya kusalimiwa kwa kiganja na rafiki yangu....mwalimu alikua ni mwenyeji wa Songea, mngoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True....nikiwa huko huwa sionagi wa kuskia makelele ya shikamoo....ya mwendo wa A/aleykum tu....huwa najiskia faraja sana......

Sent using Jamii Forums mobile app
Zote ni salamu za kitumwa tu, zao la waarabu. Ni sawa na mtu mnaongea lugha ya kiswahili lakini asubuhi mnaamkiana "good morning" halafu mnaendelea na kiswahili chenu.

Hizi ni salamu za kitumwa na hazina maana kutumika na sisi.
 
Shikamoo ni salamu, Ila salamu siyo shikamoo unaweza mwambia mtu za asubuhi,za kuamka,za kushinda.....huwa sipendelei shikamoo naona kama utumwa Fulani hivi ni bora kumwambia mtu za SAA hizi
 
Unaelewa mana ya hili neno "assalam aleykum" kwa kiswahili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shikamoo ni salamu, Ila salamu siyo shikamoo unaweza mwambia mtu za asubuhi,za kuamka,za kushinda.....huwa sipendelei shikamoo naona kama utumwa Fulani hivi ni bora kumwambia mtu za SAA hizi
Tatzo hiki kizazi chetu kimeshaoza juu ya hii salam...sjui uanzie wap kuwaelewa kuwa hii salam sio nzuri kuitumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu.
Ifike mahali kengele la adha ya kuishi kwenye nyumba za waswahili lilie ubongoni mwako, kama haukuwa na wazo la kuandaa mustakabali wako, basi hiyo ni fursa, lianzishe sasa, maana haujachelewa bado.

Umiliki wa kitu chochote huanza na wazo kwanza, kisha Mungu hufungua neema zake na hakuna kitu kilichowezwa na mwenziyo, wewe kukakushinda!

Kuna dharau ama manyanyaso mengine unaweza kuyapata mtu, yakawa ndiyo mwanzo wa mabadiliko ya mfumo mzima wa maisha yako.

Hiyo umeipata ni kiashiria sahihi cha tabia ya uswahilini.

Amekuwa ni baba yako mzazi huyo anayestahili kuamkiwa hata kwa kufunguzwa ili kumjulia hali?

Unaishi kwake kwa mkataba wa kulipana kodi, si vinginevyo na shikamoo yako haikupatii taafifu ya kodi.

Huyo anataka kukupandilia kisogoni umuabudu, kwa cheo cha baba mwenyenyumba ili aendelee kukunyanyasa!

Wewe fanya mambo yako kama kawaida, usimjali na wala asikukwaze ili mradi unamlipa kodi yake.

Fuata utaratibu uliojiwekea, namna ya kuamkia mtu kwa distance inayofaa kuwasiliana.

Usimuwekee kinyongo wala asikubadilishie mfumo wa uhuru wako na epuka naye mazoea.

Hizo 'shikamoo' kila mtu anaitafsiri kichwani mwake anavyotaka yeye.

Nikupe mfano, siku moja nikiwa mtumishi wa serikali kwa hadhi ya wilaya, alifika ofisini kwangu mbabu, anayenizidi kiumri kama miaka15hivi, akanitandika shikamoo!

Sikuvumilia nikamuuliza kwanini aninyenyekee kwa salamu hiyo, wakati aliyestahili kuamkiwa ni yeye anayenizidi umri?

Yule mzee wala hakumumunya maneno, akanieleza kuwa shikamoo aliyonipiga nayo usoni si ya umri bali ni ya ofisi na madaraka niliyonayo.

Akaongeza kuwa, vinginevyo nisingekuwa na cheo pamoja na ofisi, kamwe nisingelipata hicho kionjo toka kinywani mwake!

Nilishangaa sana na kugundua kuwa salaam ya shikamoo haina tafsiri moja yenye kueleweka kama watu wengi tunavyoichukulia!

Sent using Jamii Forums mobile app

Umenena mkuu....
 
Unaelewa mana ya hili neno "assalam aleykum" kwa kiswahili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_20180905-091808~2.jpeg
 
Niliwahi kuchumbia Mwanza... Eti kisa mchumba wangu ni mdogo ndio nalazimishwa kumwamkia kaka yake katoto kadogo hakalingani hata na mdogo wangu wa 3!

Nikamwambia huyo aliyewaletea hiyo shikamoo aliwapa masharti kwa mdogo amwamkie mkubwa sasa nitaanzaje kukuamkia wewe mdogo wangu wa 4?

Sent from my TECNO-M3 using JamiiForums mobile app
Haaaaa mkuu serious?? Vipi walikuelewa?

mndamba kutoka Ifakara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom