Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,202
- 25,526
sasa kwa kesi kama hii unawasaidiaje?wakienda mahakamani wanaweza kupeana talaka?
Nitafute Mkuu tuongee na kuelewana
sasa kwa kesi kama hii unawasaidiaje?wakienda mahakamani wanaweza kupeana talaka?
Asante mkuu.
Mahakama ya mwanzo imetengua ndoa. Nataka kukata rufaa. Ndoa imetenguliwa Iringa. Ninayemkatia rufaa yupo kigoma
1.Rufaa nikate katika mahakama gain?
2.Rufaa nikate pale nilipo Mimi au alipo mkatiwa rufaa au mkoa wowote?
Karibu
Nitafute Mkuu tuongee na kuelewana
Kwa mfano nimeoa, ila mke kanikuta na kila kitu nikaishi nae miaka 5, hatuna watoto kwa bahati mbaya tukaachana je mali alizo zikuta tutagawana?
Kama ni mali zako binafsi,haziwezi kuwa machumo ya ndoa. Hivyobasi,hazitagawanywa. Lakini,hakikisha zinakuwa kweli mali zako binafsi kwa kutunza nyaraka za uthibitisho wa hilo.
Petro,Kuna mke na mume walioishi kwa miaka 15 bila ndoa rasmi lakini hawakubahatika kupata mtoto. Mke aligundulika Ana tatizo na miaka 5 iliyopita akamruhusu mume kuzaa kwingineko.Swali je hao watoto (ni wawili) watakuwa na haki yoyote ya kurithi Mali za Baba Yao ambazo alichuma na mke mkubwa?
As ante mkuu. Ni kwamba Mimi naishi iringa.Mdai ambaye anaishi kigoma alifungua kesi mkoa nilipo yaani Iringa. Sasa ndo nauliza nikitaka kukataa rufaa, niende mahakama ipi maana baada ya mahakama ya mwanzo zinafuata za wilaya, mkazi, mkoa na mahakama kuu?Mkuu Polisi ningefurahi kujua ilikuwaje shauri la mwanzo lilisikilizwa Iringa. .
Mkuu daughter, kwakuwa hakuna ndoa,nayaona mahusiano hayo kama ya kimkataba zaidi. Makubaliano yao yataamua.Lakini,naomba kujua kama huyo wa pili alizaa naye alimuoa au la na kama ana mali naye zozote.
Mkuu jMali, kiufupi,hata ndani ya ndoa,wanandoa wanaruhusiwa chini ya kifungu cha 56 cha Sheria ya Ndoa,kumiliki mali binafsi. Kwahiyo, hata baada ya kuachana,mgawanyo wa machumo utajikita kwenye mali za pamoja tu na zile binafsi kuelekea sehemu stahiki.
As ante mkuu. Ni kwamba Mimi naishi iringa.Mdai ambaye anaishi kigoma alifungua kesi mkoa nilipo yaani Iringa. Sasa ndo nauliza nikitaka kukataa rufaa, niende mahakama ipi maana baada ya mahakama ya mwanzo zinafuata za wilaya, mkazi, mkoa na mahakama kuu?
Pili kwa kuwa mkatiwa rufaa yupo kigoma, je ni sheria nikakate rufaa huko au naweza kuamua popote pale?
Asante
Ni nini kikifanyika ndio ndoa inakuwa imevunjika rasmi?
umeoa mwanamke akakuta unaboma halafu mkaliendeleza kulijenga na kumaliza na kuhamia baadae ukaiandika kama mali ya mtoto mliyezaa nae je mkiachana ataiuza ampokonye mtoto
Mkuu Polisi,kwanza hakuna Mahakama ya Mkoa katika Mahakama za Tanzania. Mahakama zilizopo ni: Mahakama ya Mwanzo,Mahakama ya Wilaya,Mahakama ya Hakimu Mkazi,Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Pili, rufani hiyo lazima iende Mahakama ya Wilaya ilipo Mahakama ya Mwanzo iliyotengua ndoa.
asante sana, kuna ile habari ya kusema mwanamke anachangia mali za mume, kwa kutimiza majukumu ya "house wife" kupika, kufua etc, sasa kwa mfano nikiwa na holding company inayomiliki mali zangu kabla hatujaoana, je, kwenye talaka inaweza kusemwa kuwa mke alishiriki katika ukuaji wa kampuni hii toka tumeoana mpaka tunaachana kwa sababu tu alikuwa ananipikia n.k?
Umekaa na mwanamke miaka miwili bila kumlipia mahali baadae akafariki sheria itasemaje hapoIkitolewa na Mahakama Amri ya Talaka
hakumuowa kwa ndoa ila pia wana baadhi ya Mali za pamoja