Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Asante mkuu.
Mahakama ya mwanzo imetengua ndoa. Nataka kukata rufaa. Ndoa imetenguliwa Iringa. Ninayemkatia rufaa yupo kigoma
1.Rufaa nikate katika mahakama gain?
2.Rufaa nikate pale nilipo Mimi au alipo mkatiwa rufaa au mkoa wowote?
Karibu

Mkuu Polisi ningefurahi kujua ilikuwaje shauri la mwanzo lilisikilizwa Iringa. Hatahivyo, ustaarabu wa kisheria hutaka shauri lifunguliwe pale ambapo Mkatiwa Rufani anapatikana.Hivyobasi, ingekupasa ufungue rufani Kigoma.Lakini, kwakuwa rufani yako inaelekezwa Mahakama ya Wilaya inapopatikana Mahakama ya Mwanzo iliyotoa uamuzi wa mwanzo, yakupasa ufungue rufani Mahakama ulipo,naamini ni Iringa. Ingekuwa tofauti kama ungekuwa unaelekea Mahakama Kuu.
 
Last edited by a moderator:
Petro,Kuna mke na mume walioishi kwa miaka 15 bila ndoa rasmi lakini hawakubahatika kupata mtoto. Mke aligundulika Ana tatizo na miaka 5 iliyopita akamruhusu mume kuzaa kwingineko.Swali je hao watoto (ni wawili) watakuwa na haki yoyote ya kurithi Mali za Baba Yao ambazo alichuma na mke mkubwa?
 
Mkuu daughter, kwakuwa hakuna ndoa,nayaona mahusiano hayo kama ya kimkataba zaidi. Makubaliano yao yataamua.Lakini,naomba kujua kama huyo wa pili alizaa naye alimuoa au la na kama ana mali naye zozote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Polisi ningefurahi kujua ilikuwaje shauri la mwanzo lilisikilizwa Iringa. .
As ante mkuu. Ni kwamba Mimi naishi iringa.Mdai ambaye anaishi kigoma alifungua kesi mkoa nilipo yaani Iringa. Sasa ndo nauliza nikitaka kukataa rufaa, niende mahakama ipi maana baada ya mahakama ya mwanzo zinafuata za wilaya, mkazi, mkoa na mahakama kuu?
Pili kwa kuwa mkatiwa rufaa yupo kigoma, je ni sheria nikakate rufaa huko au naweza kuamua popote pale?
Asante
 
Last edited by a moderator:
umeoa mwanamke akakuta unaboma halafu mkaliendeleza kulijenga na kumaliza na kuhamia baadae ukaiandika kama mali ya mtoto mliyezaa nae je mkiachana ataiuza ampokonye mtoto
 
Mkuu daughter, kwakuwa hakuna ndoa,nayaona mahusiano hayo kama ya kimkataba zaidi. Makubaliano yao yataamua.Lakini,naomba kujua kama huyo wa pili alizaa naye alimuoa au la na kama ana mali naye zozote.

hakumuowa kwa ndoa ila pia wana baadhi ya Mali za pamoja
 
Last edited by a moderator:
Mkuu jMali, kiufupi,hata ndani ya ndoa,wanandoa wanaruhusiwa chini ya kifungu cha 56 cha Sheria ya Ndoa,kumiliki mali binafsi. Kwahiyo, hata baada ya kuachana,mgawanyo wa machumo utajikita kwenye mali za pamoja tu na zile binafsi kuelekea sehemu stahiki.

asante sana, kuna ile habari ya kusema mwanamke anachangia mali za mume, kwa kutimiza majukumu ya "house wife" kupika, kufua etc, sasa kwa mfano nikiwa na holding company inayomiliki mali zangu kabla hatujaoana, je, kwenye talaka inaweza kusemwa kuwa mke alishiriki katika ukuaji wa kampuni hii toka tumeoana mpaka tunaachana kwa sababu tu alikuwa ananipikia n.k?
 
As ante mkuu. Ni kwamba Mimi naishi iringa.Mdai ambaye anaishi kigoma alifungua kesi mkoa nilipo yaani Iringa. Sasa ndo nauliza nikitaka kukataa rufaa, niende mahakama ipi maana baada ya mahakama ya mwanzo zinafuata za wilaya, mkazi, mkoa na mahakama kuu?
Pili kwa kuwa mkatiwa rufaa yupo kigoma, je ni sheria nikakate rufaa huko au naweza kuamua popote pale?
Asante

Mkuu Polisi,kwanza hakuna Mahakama ya Mkoa katika Mahakama za Tanzania. Mahakama zilizopo ni: Mahakama ya Mwanzo,Mahakama ya Wilaya,Mahakama ya Hakimu Mkazi,Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Pili, rufani hiyo lazima iende Mahakama ya Wilaya ilipo Mahakama ya Mwanzo iliyotengua ndoa.
 
Last edited by a moderator:
umeoa mwanamke akakuta unaboma halafu mkaliendeleza kulijenga na kumaliza na kuhamia baadae ukaiandika kama mali ya mtoto mliyezaa nae je mkiachana ataiuza ampokonye mtoto

Mkuu High Vampire,kwenye ndoa hakuna mali ya mtoto/watoto. Kuna aina mbili za mali: mali binafsi ya mwanandoa na mali ya pamoja ya wanandoa. Hivyobasi,ni busara kuepuka varangati juu ya mali kwa kuweka mali katika mifumo/aina hizo zinazotambulika kisheria.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Polisi,kwanza hakuna Mahakama ya Mkoa katika Mahakama za Tanzania. Mahakama zilizopo ni: Mahakama ya Mwanzo,Mahakama ya Wilaya,Mahakama ya Hakimu Mkazi,Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Pili, rufani hiyo lazima iende Mahakama ya Wilaya ilipo Mahakama ya Mwanzo iliyotengua ndoa.

Asante sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
asante sana, kuna ile habari ya kusema mwanamke anachangia mali za mume, kwa kutimiza majukumu ya "house wife" kupika, kufua etc, sasa kwa mfano nikiwa na holding company inayomiliki mali zangu kabla hatujaoana, je, kwenye talaka inaweza kusemwa kuwa mke alishiriki katika ukuaji wa kampuni hii toka tumeoana mpaka tunaachana kwa sababu tu alikuwa ananipikia n.k?

Mkuu sana jMali, kwanza Amri ya Talaka haibebi maelekezo mengineyo kama hayajaombwa kimahakama.Pili, mali binafsi huruhusiwa kwa wanandoa.Ni wajibu wako kutunza nyaraka za kuthibitisha kuwa mali fulani ni zako pekee.Kinyume na hapo,itahesabiwa kama ni mali ya ndoa/machumo na itagwanywa inavyopasa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom