Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

KIBONGOMKUTI

Mbona huo mlolongo mkubwa mno hivyo?!

Unaweza kukuta watu wanakuwa emotional abused kwenye ndoa wanashindwa kutoka kwa sababu hawawezi kuonyesha wazi mateso, na mmoja kati ya wana ndoa hajakubali kuwa ndoa hiyo haiwezi kuendelea tena.

Something needs to be done, kulegeza masharti hayo.

Hii haijakaa sawa

Ni kweli Gaijin wengi tuna umia/kuumizwa emotionally katika ndoa zetu ila pale unapoona mara baada ya kujaribu njia zote mbadala hakuna uwezekano wa kupata muafaka wa kunusuru ndoa. Ndo maana Sheria zinakuwepo kulinda haki za wanandoa kwa uzoefu Mahakimu/Majaji wengi huwa wanazichukulia Kesi za Ndoa hususani TALAKA kwa tahadhari kubwa ukizingintia kuwa baadhi yao pia ni wanandoa. Kuhusu emotional abuse kwa maana pana ya kisheria inaangukia katika UKATILI be it Mental or Physical. Ifahamike kuwa hakuna mwanandoa anaeamua kama ndoa ivunjike au la bali ni Mahakama ndiyo mara baada ya kuridhika hutoa Hukumu ya Kuvunja Ndoa kisheria.
 
Tatizo kubwa ni mke kabadili kabisa muelekeo kiimani kitu ambacho kinakingana na ile imani iliyokuwapo awali wakati wa kutoa kiapo cha ndoa kanisani. Licha ya kuonywa na kukatazwa mume, pia ndugu, jamaa na hata kasisi wamemshauri aondokane na hiyo imani yake mpya, bila mafanikio. Hii inaleta hali ya kutoaminiana na kuvunjika kwa amani nyumbani.

Unazungumzia KUBADILI KABISA MUELEKEO WA IMANI ........ Kama sababu ndiyo hiyo... hapo huna sababu ya kumlaumu kwa kubadilisha imani, na pia huna sababu ya kuvunja ndoa...... mfano kama ameamua kuwa mlokole shukuru Mungu, unaonaje kama angeamua kuwa mshirikina wa kutupwa ingekuwa hatari zaidi, wako wanandoa ambao mmoja wao anaamua kukata shauri kuokoka a.k.a. ULOKOLE wao wanachukulia wameikimbia dini au imani ya asili yetu, au amekimbia dini ya wazazi wetu... hakuna dini iliyosafi zaidi ya kuwajali yatima na wajane na kujikinga na dunia pasipo na mawaa...... PAMOJA NA HAYO KAMA BADO ANAENDELEA KUKUHESHIMA NA KUKUPENDA NA KUIJALI FAMILIA ENU hapo hakuna tatizo mwache aendelee na imani yake mpya mradi haikuvunjii heshima

Kuna jamaa mmoja alimfukuza mkewe kwa mambo kama hayo hayo...yan jamaa alikuwa ni dereva wa magari ya masafa marefu, basi siku moja alirudi home baada ya kutoka safari akamkuta mkewe yupo kwenye maombi ya mfululizo ya kufunga bila kula kwa siku tatu....Mume karudi home anahitaji kuhudumiwa na kupikiwa chakula ila hakuna mtu...mke yupo ndani anaroroma na kuruka ruka kwa maombi....Jamaa alimpiga kibao kimoja hapo hapo na talaka yake mkononi...
 
Mbona umpe talaka jamani?MUNGU ANACHUKIA KUACHANA,usichoke kuongea nae ili arudi RC mwambie MUNGU haangalii dhehebu hata ukiwa katoliki anabariki tu.

Hata RC kuna walokole..wanaitwa charismatic Catholic Mer Dritt watafute ili wakusaidie kukushauri...
 
Last edited by a moderator:
Unazungumzia KUBADILI KABISA MUELEKEO WA IMANI ........ Kama sababu ndiyo hiyo... hapo huna sababu ya kumlaumu kwa kubadilisha imani, na pia huna sababu ya kuvunja ndoa...... mfano kama ameamua kuwa mlokole shukuru Mungu, unaonaje kama angeamua kuwa mshirikina wa kutupwa ingekuwa hatari zaidi, wako wanandoa ambao mmoja wao anaamua kukata shauri kuokoka a.k.a. ULOKOLE wao wanachukulia wameikimbia dini au imani ya asili yetu, au amekimbia dini ya wazazi wetu... hakuna dini iliyosafi zaidi ya kuwajali yatima na wajane na kujikinga na dunia pasipo na mawaa...... PAMOJA NA HAYO KAMA BADO ANAENDELEA KUKUHESHIMA NA KUKUPENDA NA KUIJALI FAMILIA ENU hapo hakuna tatizo mwache aendelee na imani yake mpya mradi haikuvunjii heshima

Umenena vema mkuu
 
Hata RC kuna walokole..wanaitwa charismatic Catholic Mer Dritt watafute ili wakusaidie kukushauri...

Hawa "charismatic" ni tofauti kabisa na hili kundi linaloitwa "faraghani". In fact, "charismatic" wote niliozungumza nao wanawapinga kabisa hawa "faraghani". Mke ni kama karogwa. Ni balaa!
 
samehe saba mara saba kwa siku,no way mtu afanye makosa 49 kwa siku,hata muuaji,mchawi,mzinzi,je kuna upendo mkubwa kama wa kutoa maisha yako ajili ya mwingine,be strong in the spirit and in faith
 
Hawa "charismatic" ni tofauti kabisa na hili kundi linaloitwa "faraghani". In fact, "charismatic" wote niliozungumza nao wanawapinga kabisa hawa "faraghani". Mke ni kama karogwa. Ni balaa!
Pole sana jamani,sijui hawa wachungaji wanawadanganya nini?Mimi naamini uhusiano wa mtu na MUNGU ni binafsi.Sasa maombi kanisani muda wote hadi unasahau kuhudumia watoto uliowazaa huu ni ujinga huyo anahitaji kufunguliwa kifikira katekwa aisee.Jitahidi kumwelewesha kama hilo kanisa walifanikiwa kumteka,sidhani kama wewe mme wake utashindwa kumrudisha kwenye mstari.
 
Asante kwa maoni yako. Nachotaka kufahamu ni sheria imekaaje kuhusu tatizo hili. Isitoshe jee kiapo cha ndoa kilichotolewa dhehebu moja bado kitaendelea kuwa halali kama mmoja wa wanandoa baadaye aamue kujitoa kwenye dhehebu lake na kuingia dhehebu lingine?

Maelezo ya Kibongo mkuti yanatosha kwa maelezo zaidi angalia sehemu ya sheria ya ndoa hapa chini

d) Separation and Divorce (ss 99-101)
[PCh29s99]99. Right to petition for separation or divorce
Subject to the provisions of sections 77, 100 and 101, any married person may petition the court for a decree of separation or divorce on the ground that his or her marriage has broken down but no decree of divorce shall be granted unless the court is satisfied that the breakdown is irreparable.
[PCh29s100]100. Restriction on petition for divorce during first two years of marriage
(1) No person shall, without the prior leave of the court, petition for divorce before the expiry of two years from the date of the marriage which it is sought to dissolve.
(2) Leave shall not be granted to petition for divorce within two years of the marriage except where it is shown that exceptional hardship is being suffered by the person applying for such leave.
(3) An application may be made to the court under this section either before or after reference to a Board under section 101.
[PCh29s101]101. Requirement of prior reference to Board
No person shall petition for divorce unless he or she has first referred the matrimonial dispute or matter to a Board and the Board has certified that it has failed to reconcile the parties:
Provided that this requirement shall not apply in any case–
(a) where the petitioner alleges that he or she has been deserted by, and does not know the whereabouts of, his or her spouse;
(b) where the respondent is residing outside Tanzania and it is unlikely that he or she will enter the jurisdiction within the six months next ensuing after the date of the petition;
(c) where the respondent has been required to appear before the Board and has wilfully failed to attend;
(d) where the respondent is imprisoned for life or for a term of at least five years or is detained under the Preventive Detention Act * and has been so detained for a period exceeding six months;
(e) where the petitioner alleges that the respondent is suffering from an incurable mental illness;
(f) where the court is satisfied that there are extraordinary circumstances which make reference to the Board impracticable.
 
Ndoa ya kanisani (roman catholic) haivunjwi lakini hubatilishwa. Na kuna sababu nyingi tu ambazo hufanya ndoa kuwa batili. So kama wewe ni wa dhehebu hilo cha kufanya ni kwenda kwa padri wa parokia yako...mweleze tatizo lako, atamuita huyo mwenza wako atajaribu kuwasuluhisha. Akishindwa kuwasuluhisha atakupa barua unaenda nayo kwenye mahakama ya ndoa ipo kurasini kwa kardinali. Ukifika pale watajaribu kuwasuluhisha tena. Na hii process ya kuwasuluhisha hutumia muda mrefu sana. (Keep in mind that kanisa katoliki halipendi kabisa haya mambo ya talaka so watafanya kila njia kuwarudisha pamoja).

Nenda pale bookshop cathedral (karibu na saint joseph), nunua kitabu cha sheria za ndoa. humo wameeleza kila kitu kuhusu sheria za ndoa ya kikatoliki na kanuni zinazofanya ndoa ikawa batili. ukishajua ni nini hasa kinafanya ndoa kuwa batili, na kama kuna kanuni yoyote inaendana na hilo tatizo lako..ndo unasimamia kanuni hiyo kufanya ndoa yenu kuwa batili.

Mbali na hizo kanuni, hakuna njia yoyote inayoweza kufanya ndoa yenu kuwa batili.

sasa basi, baada ya hapo watawahoji pamoja na mashahidi then kesi inapelekwa kwenye mahakama kuu ya ndoa ya kanisa katoliki, ipo moshi. huko wanajadili tena kesi yenu halafu wanatoa hukumu inarudishwa dar,kama ndoa ni batili mnaambiwa na kupewa barua iliyosainiwa na kardinali pengo. baada ya hapo sasa ndo unaenda mahakama ya serikali kudai talaka, huko hakuna shida kabisa kama unakuwa tayari umeshapitia process ya kanisani na ndoa yenu imekuwa declared batili.

Shida mtakayoipata kwenye mahakama ya serikali ni endapo mtakuwa mna mali mlizochuma pamoja na endapo mna watoto wadogo wanaohitaji custody ya mzazi.

Sidhani kama nimeeleweka vizuri, nina uhakika na hizo process coz nimezishuhudia mwenyewe. ila hutakiwi kuwa na haraka maana hayo mambo ya kanisani yanatumia muda mrefu sana unaweza kukata tamaa. inaweza kuchukua hata miaka mitano.
kila la kheri.
 
Hapa wajuzi wa sheria wanahitajika. Haiingii akilini kuwa nyie wenye ndoa mmeamua kuvunja uhusiano wenu kwa sababu zenu wenyewe mlazimishwe kusuluhishwa.

Ni kupoteza muda na resources nyengine tu.

Kwa watu wanaojiandaa kuingia kwenye ndoa ni vizuri wafahamu kuwa ndoa si jambo la kukimbilia kabla ya kujipanga na kwamba hakuna majaribio ya kuoa au kuolewa.

Ndoa ni taasisi muhimu katika maisha ya mwanadamu, na kwenye ndoa imara tunapata watu imara na wenye kutimiza wajibu wao, na kwa hiyo basi tunapata taifa imara. Kutokana na msingi huu ndio maana sheria zote zinazohusu ndoa huweka utaratibu mgumu wa kuvunja ndoa ili suluhu iwe jambo la kwanza na kuvunja ndoa iwe jambo la mwisho na ambalo kama taratibu zitafuatwa halitafikiwa.

Ni vizuri ifahamike pia, kuwa ndoa ni mkataba wa aina yake, amabao condition kubwa ni kwa wanandoa kuishi pamoja kwa maisha yao yote na kwahiyo basi, kwa kuwa walikubaliana kuishi pamoja, hakuna hiari ya kuachana; ni lazima wawe na sababu za msingi, zinazokubaliwa kisheria na zinazoweza kuthibitishwa mahakamani ili waweze kuachana.

Lakini ni vizuri kujua kuwa maandiko yanasema aliyoyaunganisha Mungu mwanadamu asiyatenganishe.
 
kama ni mkatoliki, na unajua ndoa ni sakramenti, huwezi omba watu wengine wakuvunjie.

Ukiamua unaivunja mwenyewe bila msaada wa mtu yeyote maana hata padri wala papa hawana mamlaka ya kuvunja ndoa hiyo.

Kwa hiyo ndio maana hata wao huwa hawana majibu sahihi ya kuvunja ndoa maana hawana mamlaka hayo.

Ni sawa na kesi ya mauaji ulazimishe iamliwe na mahakama ya mwanzo wakati haina mamlaka hayo kisheria.
 
Na hii ina sababisha ndoa kushindwa kutumika(consumation of marriage)

Hapa umezungumza ukweli mtupu. Iweje mke aende kusali/kufanya maombi kila siku, siku saba kwa wiki? Na mbaya zaidi hata watoto hawahudumii vilivyo kama ilivyokuwa awali?
 
Kuna vitu vitaangaliwa kama
* kwanza itabidi ithibitishwe kuwa njia ya kusuluhisha imeshindika.
* kuwepo na ushahidi wa kutosha kuvunja ndoa hiyo
ikumbukwe kwamba ndoa ya kanisani ina tambulika kisheria hivyo kuivunja sheria zitafatwa
Jee, ni taratibu zipi za kufuata ili mwanandoa aliyefunga ndoa ya Kikristo kanisani aweze kuivunja ndoa hiyo kimahakama au kisheria?

Wataalamu wa Sheria tafadhali naomba mnifahamishe. Natanguliza shukrani.
 
Yaani wewe mke anaamua kuwa mlokole halafu unalialia? Cha msingi kaeni chini elewaneni? Pia ninajua kuwa kuokoka kunasababishwa na mambo mengi sana!!! Je una uhakika wewe si sababu ya mkeo kuokoka? Ulitaka awe Muislam ili akuchomee nyumba kabisa!!! Shukuru mkeo ameamua kuwa mkristu kwa ukamilifu zaidi. Cha msingi ashauriwe awe na kiasi ili asisahau familia. Na hawa wachungaji ambao hawana maadili ni kuwa na ratiba lukuki za kanisa ili mradi tu wakusanye sadaka!! Nyambafu yenu.
 
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea ndoa kuvunjika, wanandoa wanaweza kubaliana wao wenyewe kuvunja ndoa na hakuna sheria yeyote inayoweza kuwakataza. Kusema ndoa za kikristo hazivunjiki ni uongo wa kweli uliokomaa na kuota mizizi. Sina haja ya kuanzisha uzi mwingine kuhusu hili, ila sheria ya hati ya ndoa au cheti cha ndoa pamoja na pete ni ubunifu wa kibinadamu ili kuudhibiti mfumo dume wa kuwanyanyasa wanawake uliokuwa ukitekelezwa katika himaya ya "hao" wanaojiita wakristo enzi zile. (Mnisamehe kama nitawaudhi kidogo kwani mimi ni mkristo na nina ndoa iliyojaliwa watoto watatu.) Hivyo kanisa la Kirumi likaona ni vyema kuanzisha utaratibu huo wa vyeti vya ndoa na haikuruhusiwa mtu kujitengenezea cheti chake. Hivyo suala hilo likapenyezwa hadi serikalini kupitia Roman Catholic popote duniani. Haikuishia hapo Protestants (Lutheran, Waadventist/Sabato, na akina sisi wengine tukaendelea na mfumo huo)...Nguvu kubwa zaidi ikapatikana Anglican (Uingereza) wakati wanawake walipoandamana hadi kwa King James kudai haki zao za msingi, kuwa waume zao huenda katika clubs na kunywa sana scotch whisky na kuja nyumbani usiku wakiwa "basi tena" hivyo wakati hawa akina mama wakihitaji shughuli waume walikuwa wa kwanza kufika kileleni au hata wasifike kabisa na kuwaacha wake zao wakihitaji huduma. Naye King James akapitisha sheria iitwayo "Ladies First".

Back to the point, Mfumo wa vyeti hivi haubagui mtu ila una option kama ndoa ni ya wake wengi, mke mmoja, kihindi, kibudha nk. Kwa waislamu hapa dini haijatajwa ila ni hapo kwenye "wake wengi". Mnisahihishe ndg zangu kama nitakuwa nakosea. Ila waislamu wana vyeti vyao, tofauti na hivi vya kiserikali na vinakubalika.

Tatizo la mfumo dume ni kutojua maana halisi ya ndoa, au kuoa. Uchanga wa kiswahili pia unachangia katika suala hili. Kwa kiingereza hakuna neno kuolewa. Kwa kiswahili lipo kwa maana ya Mtenda(mume) na Mtendwa (Mke) ila kwa kiingereza wote ni (Watenda).

Hii ni kusema (kwa wote wawili) wameoana. Kuoana ni kupendana, kuendana, kushabihiana, kufanana, kulandana,kukubaliana, kufanana, kuoana. Kwa hiyo wawili hawa wanaoana. Haiwezekani mmoja akamuoa mwenzake. Kuoa ni mfumo dume, yaani hata kama mwenzako hataki wewe unamuoa- huo ni udikteta. Kwa kiingereza ni "married to" mfano mimi Thanda nasema, I am married to Thando (mke wangu) naye atajitambulisha hivyo I am married to Thanda.

Hakuna kusema I married Thando, naye aseme I am married by Thanda. Wote, "we are married to one another"

Pia ukuzi wa lugha unapanuka zaidi unaweza kuoa mambo mengi sana. Kwa mfano
"I will marry your ideas" au " Mr Brat has married my characteristics of not having fun during night"

Kwa hiyo wadau hapa pana mengi ya kujifunza kuhusu ndoa, ndoa ni zaidi ya watu wawili kuishi pamoja, kulala kitanda kimoja, kufanya tendo la ndoa. Ndoa ni kujifunza mengi. Vipi lile andiko katika Biblia lisema kila unayezini naye unakuwa umefunga naye ndoa? Ok kama ni hivyo basi tujiulize hadi sasa tuna ndoa ngapi?

Nawasilisha.
 
Ndoa ya kanisani (roman catholic) haivunjwi lakini hubatilishwa. Na kuna sababu nyingi tu ambazo hufanya ndoa kuwa batili. So kama wewe ni wa dhehebu hilo cha kufanya ni kwenda kwa padri wa parokia yako...mweleze tatizo lako, atamuita huyo mwenza wako atajaribu kuwasuluhisha. Akishindwa kuwasuluhisha atakupa barua unaenda nayo kwenye mahakama ya ndoa ipo kurasini kwa kardinali. Ukifika pale watajaribu kuwasuluhisha tena. Na hii process ya kuwasuluhisha hutumia muda mrefu sana. (Keep in mind that kanisa katoliki halipendi kabisa haya mambo ya talaka so watafanya kila njia kuwarudisha pamoja).

Nenda pale bookshop cathedral (karibu na saint joseph), nunua kitabu cha sheria za ndoa. humo wameeleza kila kitu kuhusu sheria za ndoa ya kikatoliki na kanuni zinazofanya ndoa ikawa batili. ukishajua ni nini hasa kinafanya ndoa kuwa batili, na kama kuna kanuni yoyote inaendana na hilo tatizo lako..ndo unasimamia kanuni hiyo kufanya ndoa yenu kuwa batili.

Mbali na hizo kanuni, hakuna njia yoyote inayoweza kufanya ndoa yenu kuwa batili.

sasa basi, baada ya hapo watawahoji pamoja na mashahidi then kesi inapelekwa kwenye mahakama kuu ya ndoa ya kanisa katoliki, ipo moshi. huko wanajadili tena kesi yenu halafu wanatoa hukumu inarudishwa dar,kama ndoa ni batili mnaambiwa na kupewa barua iliyosainiwa na kardinali pengo. baada ya hapo sasa ndo unaenda mahakama ya serikali kudai talaka, huko hakuna shida kabisa kama unakuwa tayari umeshapitia process ya kanisani na ndoa yenu imekuwa declared batili.

Shida mtakayoipata kwenye mahakama ya serikali ni endapo mtakuwa mna mali mlizochuma pamoja na endapo mna watoto wadogo wanaohitaji custody ya mzazi.

Sidhani kama nimeeleweka vizuri, nina uhakika na hizo process coz nimezishuhudia mwenyewe. ila hutakiwi kuwa na haraka maana hayo mambo ya kanisani yanatumia muda mrefu sana unaweza kukata tamaa. inaweza kuchukua hata miaka mitano.
kila la kheri.

Ndugu yangu nashukuru kwa kuniweka wazi namna hii. Nina shida ya namna hiyo na nitajitahidi kuwa mvumilivu wa kufuatilia kwa karibu nijue hatima yake. Je baada ya kubatilishwa unaruhusiwa kusimama tena kanisani kufunga ndoa nyingine ya kikatoliki???
 
Utangulizi.
Ndoa inaweza kuvunjwa na mahakama iwapo mambo haya yafuatayo yametokea kwenye ndoa husika na mmoja wa wanandoa kuchukua hatua ya kuomba mahakama ivunje ndoa hiyo.
1.kufumaniwa unazini-(walau iwe mara kwa mara)
2.ukatiri uliopitiza kwa mwenzi wako.
3.kumtenga mwenzi wako kwa kipindi kisichopungua miaka 8,aidha kwa kuhama chumba au kuhama nyumba,mji au nchi.

Sasa iwapo kati ya hayo niliyoyataja hapo juu yametokea mwanandoa anatakiwa kwanza aende kanisani kwa usuluhishi na ikishindika Mchungaji au Padri atatoa cheti cha kushindwa kusuluhisha, kwa faida ya watu wote iki cheti cha kushindwa kusuluhisha ni muhimu sana kwani huwezi kufungua kesi mahakama kuomba mahakama kuvunja ndoa bila kuonesha ulianzia kanisani na wakashindwa kuwasuruhisha.

Lakini mbali na zile sababu 3 nilizosema zinaweza peleka mahakama kuvunja ndoa, ili ndoa ivunjwe lazima mahakama ijiridhishe bila kutia shaka kuwa ndoa hiyo haiwezi kutengemaa kabisa.

Fafanua hizo nyekundu.
 
Back
Top Bottom