Mkuu inaonekana nyumba za Ibada huendi wewe.
Kila kanisa au msikiti basi ukiwauliza wanajua nyumba za watoto yatima zilizo karibu.
Utaratibu ni kwamba uyatima una nama nyingi sana.Kuna waliofiwa na wazazi wote na kuna aliefiwa na mzazi mmoja.
Sasa aliefiwa na mzazi mmoja nahisi sio nzuri sana kumchukua,maana akianza kupata uelekeo kunakuwa na conflict kubwa saana kutoa upande wa mzazi wake.Tena inaweza kukufanya ukajuta kumlea,maana hadi huyo mtoto anaweza kuona hujafanya kitu,au akachukia upande mmoja,na inaweza pia akakuchukia wewe pia.Maana mama yake anaweza kuwa ameolewa na mwanaume mwingine kisha akalazimisha waje wamchukue,hapo inabidi umuache.
Nakushauri tafuta mtoto aliefiwa na wazazi wote,huyu atakuwa huru zaidi na atakuona kwamba nyie ndio wazazi wake in full,licha ya kwamba atajua wazazi wake wameishafariki,ila atajua nyie ndio wazazi wake wa pili mliompa dunia na kuijua na kumsaidia,
Na ndio maana kwa Sie waislam hata wakristo kama sikosei,ni kwamba kama ukimlea yatima kama mungu anavyotaka,basi kama na wewe utakuwa mtu wa mungu,nyumba yako na maisha yako yatakuwa na baraka sana.Na huto athirika na maisha ya dunia hadi mungu atakapoamua kukupa mtihani wake tu wa kukujaribu.Neema na thawabu kwa Mungu ni kubwa saana.Ila wengi sana wanafeli ikifika hatua fulani.
Wazo:- Ila sijajua uwezo wako na hali yako,ila ningekushauri uwachukua wawili,wa kiume mmoja na wakike mmoja.
Najua hakuna ulezi mwepesi ila fanya kama ni watoto wako,na usifikirie kwamba hao ni malaika,la, hao ni binaadam na watoto kama walivyo wengine,kuna manunda,wagomvi,wadokozi,kuna watoto wamepinda kupita maelezo,ila hayo yote uyajue.
Na isije siku ukajuta kwamba unajuta kumlea mtoto yatima,ni dhambi kubwa sana kwa mungu na hata kusamehe.
Hata kama huyo mtoto atakuwa kibaka au kama ni wa kike atakuwa Malaya,tambua huo ni mtihani mungu anakupa,maana hata mwanao wa kumzaa anaweza kuwa kama hivyo.Sasa mungu anakupa mtihani huo ili kuona uwezo wako wa kupambana nahali hiyo.
Jingine,nakushauri sana,chukua mwenye umri kati ya 3 - 5yrs.
Jinsi ya kuwapata:Kwanza uwe unatambulika na kazi yako kwa ujumla,baadhi ya vituo huweka ukaguzi wa kustukiza,maana huyu mtoto lazima kituo kiwe na ushirikiano wa karibu sana na wewe,na pia kama utakuwa muungwana basi siku moja moja unampeleka aende kwa wenzie akakumbuke alipotoka ili na yeye mungu akimpa huko ukubwani,basi afanye zaidi ya umevyofanya wewe kwake.
Ustawi wa jamii pia lazima wahusishwe kwa kushirikiana na serikali za mitaa na wajumbe wake.
Na muhim zaidi tafuta mwanasheria ambae atasimamia taratibu zako,hili ni muhim saana tena saana.
Ubarikiwe kwa lengo lako.