cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 497
link ulotupa imesaidia japo maelezo hayakuwa ya kutosha
ukitaka ku adopt unatakiwa wende wapi? na lazima tayari uwe ushajua unataka kum adopt nani au ukifika kwa wahusika wanakutafutia wao?
Imekuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu ku-adopt mtoto yatima awe wangu kabisa nimlee,kumsomesha na kumfanyia yote anayostahili kufanyiwa mtoto!sasa naona nina uwezo na muda wa kuitimiza ndoto yangu!
hivyo naomba kujulishwa sheria na taratibu za kuasili/adopt mtoto hapa Tanzania!
Je niende wapi kwa ajili ya kufanikisha jambo hili!
natanguliza shukrani!
Nina wasiwasi na hizi fikra zako cheusi!
Sidhani kama ni sahii unless Cheusi wewe si muafrika.
Coz ninaamini uko na ndugu zako wengi masikini wengine hawana hata pakuishi, wanaumasikini mkubwa tuu wa kutosha kuwasaidia wanyanyuke.
Mbona haya mamboya kuadopt kids from other families in Africa bado sana, predicted may be in africa (Tanzania in particular) they can start for 200 years to come or more than that, of which I believe it is not in your generation.
Your clan net worth iko vipi cheusi, work it out a little bit and understand your responsibilities in a family and your clan before you go into other families business cheusi wee.
Acha kuigiza maisha yako.
"LIFE IS CHOICE LIVE IT" Tehe he heeeee....
Kweli huna ndugu huko Tanganyika wa kuweza kuchukua mtoto umlee? au mnataka misifa mbele za watu!
Cheusi mangala badili mwendo huo mangala eeh mangala eeh binti wa afrika. Tusimkatishe tamaa yawezekana yeye mwenyewe kashindwa kupata mtoto wa kumzaa kwa sababu yeyote ile. Kuchukua mtoto wa ndugu ni sahihi kabisa lakini ikumbukwe tu mtoto huyo atakuwa na wazazi wake na wazazi wake bado watakuwa na amri ya mwisho kwa mtoto wao jambo ambalo litamwathiri mlezi kwa kiasi kikubwa.NGUO YA KUAZIMA HAISITIRI ******. na tumuulize ni chepi kimemsibu hadi kufikia uamuzi huo
nakuombea kwa muumba akujalie wana wema wakufae na waifae jamii itakayowazunguka kikubwa wawe wacha MUNGU kama wewe japo kuna kipindi uliahidi kuiondoa AVAR yako maana ilisababisha mtaafaruku humu jamvini lakini bado umeikomalia.Mangala CHAKO NI CHAKO UKIKIONA CHA MWENZIO KITEME MATE.Ushauri wangu kwako zaa ulee damu yako kuliko kukimbilia mambo ya KIDHUUNGU. Na lau kama hupati bahati ya kuzaa si vibaya ukatekeleza uamuzi wakosina matatizo yeyote ya kuzaa na siku moja nitakuja kuzaa muda utakapofika!
hujatenda dhambi kuwa na wasiwasi na fikra zangu na yote uliyoongea ni kweli lkn nisamehe tu maana sitabadili msimamo wangu niombee nifanikiwe!
sina matatizo yeyote ya kuzaa na siku moja nitakuja kuzaa muda utakapofika!
asante na mungu akubariki sana na anisamehe kwa kutaka misifa mbele ya halaiki!