Sheria na Katiba ya nchi sidhani kama inatambua kuna vitabu vitakatifu. Utakatifu wa vitabu unapimwa na nini?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,896
Kwema Wakuu!

Nimeona tujadili Jambo hapa kuhusu baadhi ya kauli za Watu hasa viongozi wa kisiasa wanaposema vitabu vitakatifu, sijajua wanazungumzia vitabu vipi.

Na hivyo vitabu vinavyozungumziwa je kisheria au Katiba ya nchi yetu inatambua kuna vitabu vitakatifu?
Nini vigezo vya kitabu Fulani kuitwa kitakatifu?
Je ni muandishi akiamua kukiita kitabu chake kitakatifu mfan Mimi ni Mtunzi alafu nikipe jina kitabu " Habisi Takatifu" je kitabu hicho kitageuka kitakatifu?

Au je Watu wakiamua kuamini na kukiita kitabu Fulani kitakatifu basi hapohapo kinageuka kitakatifu? Nazungumzia Imani.

Wataalamu wa mambo hasa ya kisheria mtupe muongozo wa kisheria, je ni upi uhalali wa Watu hasa viongozi wa kisiasa na nchi kuita vitabu Fulani vitakatifu? Je sheria au Katiba ya nchi kuna sehemu imevitaja vitabu hivyo.
Kama Vipo nitaomba nitajiwe ni vitabu gani vitakatifu kulingana na sheria za nchi yetu.

Kabla hatujajadili ishu ya utakatifu wenyewe.

Karibuni kwenye mjadala.

Mods msihamishe huu Uzi.
 
Back
Top Bottom