Sheria au Sera gani inayotuongoza katika kufungua uchumi kwa hisani ya wawekezaji?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Salamu!

Ni vyema tunaposema kuwa tunaenda kufungua uchumi kwa kualika wawekezaji wa nje tuwe na sera mahsusi na sheria dhibiti zinazotuongoza katika utekekezaji.

Iwapo Sera na Sheria zetu ni duni katika hili tutegemee kuanguaka kiuchumi.

Je, Sheria au Sera ya kufungua uchumi kwa hisani ya wawekezaji inagusia nini?

1-Ni nani mwekezaji mwenye mashiko?anatokea nchi zipi na kwa nini tunahisi tumlegezee masharti?

2-Ni kwa muda gani sasa tunaifungua nchi kwa wawekezaji hadi pale tutakaposimama na kuwapendlea wawekezaji wazawa?

3-Ni maeneo gani ya uwekezaji tunayoyafungua?wawekezaji duniani wapo wa sekta zote kuanzia kilimo, afya, madini, michezo, usafiri n.k sasa sisi kama Taifa tumefanya upembuzi wa kutosha na kujua ni maeneo gani na sekta zipi za kuwaachia wawekezaji wa nje na ndani kutusaidia?

4-Iko wapo ripoti ya kina kuwa tukiwalegezea wawekezaji wa nje tutafanikiwa??Tunatenda kwa ushahidi upi wa wazi?Bunge limeridhia ufunguaji au ufungaji wa fursa kwa wawekezeji wa nje? Yapo maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kukurupuka.

Msimamo wangu ni kuwa muongozo wa namna gani nchi iendeshwe mara baada ya uhuru upo ila viongozi wetu hawataki kuufuata.ushauri wangu ni kuwa muongozo huo ufuatwe kwa vitendo hata kama tutaonekana ni wakorofi,outdated au rigid.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Back
Top Bottom