Chifu Sanze
JF-Expert Member
- Jul 20, 2021
- 3,103
- 6,295
Utakufa bure kwa sonona uliyekuwa ukimpenda ameshakufa na harudi tena(bila shaka ulimpendea roho mbaya yake) na usiyempenda ndiye yupo tena hadi 2030 sasa jiulize utaumia kiasi gani!Kama ibara ya kwanza ya katiba ya JMT inavyotanabaisha ni kuwa Tanzania ni dola huru ambayo ni jamhuri ya muungano.
Jamhuri ya muungano wa Tanzania ilizaliwa mwaka 1964 siku ya tarehe 26 mwezi wa nne.
Ibara ya 33 ya katiba ya JMT inatanabisha wazi kuwa rais ndie mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu.
Kusherehekea siku kuu ya kuzaliwa JMT huku mkuu wa nchi hayupo ni sawa kweli?
Hii inaleta picha gani?