Sherehe za kumuaga Samweli Sitta zavurugika Dodoma

Sherehe za kumuaga Samweli Sitta zavurugika Dodoma

Hiyo ndo CCM ya wachovu wa mawazo aliyoyasema Nyerere kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania"

Yaani Sitta naye anakubali kufanyiwa sherehe ya kuagwa? Je hizo nazo ni fedha za walipa kodi au michango yao binafsi? Wamesahau kwamba watoto wanakaa chini hakuna madawati na walimu wanawadai, na wagonjwa wanalala wanne wanne kwa kila kitanda?
"ama kweli akili za kuambiwa changanya na zako!"
Kama kuagwa si angeagwa kitambo yaani miaka kibao imepita ndio wanamuaga, hapa maana yake 2015 asigombee tena ikiwa kama atakuwa bado yupo interested na siasa zetu (kama vile wamefanya hivyo ili aone noma kugombea)
 
ukiona former spika, mwanasiasa wa miaka karibia sabini, mtu mzito tena hata mkewe naye ni mwanasiasa na former waziri wanapewa TV ya 46" ujue either tuna kamati mbovu za maandalizi ya sherehe au tuna viongozi wasiojua maana ya zawadi
 
Jana kulikuwa na sherehe za kumuaga Samweli Sitta ,Spika za zamani wa Bunge zilivurigika baada ya Spika wa Bunge na Pinda kuamuru zipigwe nyimbo za Komba na mmojawapo uliopigwa ni ule wa ....wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe... Wimbo huu uliamsha hasira za wabunge wa CUF ambao waliamua kuondoka kwenye sherehe hizo bila kula chakula kilichokuwa kimeandaliwa.

Mbatia naye alitaka kuondoka ila akashikwa mkono na wabunge wa CCM naye bila aibu alirejea kwenye sherehe hizo , ila wabunge wa CUF waliamua kuondoka moja kwa moja pamoja na zawadi waliyokuwa wamemwandalia Sitta.

wabunge wa Chadema ,hawakuwepo hata mmoja.

----------------------------

IMG_0080.JPG


Aibu ilioje .... .... ...... zawadi ya television kutoka kwa pesa za walipa kodi? Halafu wanaitangaza kama vile ni kitu cha maana sana, hivi kweli katika karne ya 21 zawadi kama hii inatolewa na kuonyeshwa kwa mamillioni ya walipa kodi wakati huyu Mr. 6 alishindwa kutekeleza wajibu wake na kuiacha serikali kuendelea kutapanya pesa za walipa kodi! Je, alifanya kitu gani cha maana zaidi ya kusimamia kujiuzulu kwa richimonduli na kujirizisha kwa woga? Je, lile hekalu alilojengewa ni zawadi ya aina gani? This country has gone to the dogs.

Huku ndiko kukosa dira ya nini kifanyike kuwawezesha walipa kodi kuinua maisha yao, viongozi wanajipongeza wakati hakuna la maana wanalolifanya bali kujilimbikizia utajiri kutoka migongo ya walipa kodi.
 
Kwani CUF bado ni wapinzani au? maana sijaona huo upinzani wao labda kama ni wapinzai kwa Chadema. siku hizi afadhali hata ya NCCR unaweza kuwaita wapinzani.
 
Huyo Sitta nae ni wa hovyo tu kukubali eti kuangwa mwaka huu wa 2013, tena baada ya kudhalilishwa na mizengwe chungu mzima bado tu anaridhia...Sasa huko ni kuangwa au kusanifiwa tu.
 
akili ndogo, sasa sitta ni wa kumzawadia tv, blender au fridge...
 
binafsi hili tatizo nimeliona kwa mda mrefu wana ccm wanashindwa kutofautisha shughuli za kiserikali na kichama utakuta rais anaenda kuzindua mradi basi baadh ya viongozi wa watavaa mavazi ya chama na kuwaalika wanachama wa ccm kwa wing na mavazi ya kijani hii ni moja ya sababu ya wananch kuchukia serikali
 
Mbona hii sherehe imekuwa baada ya mlipuko. Haikuwa ni sherehe ya kitu kingine ila ikaunganishwa hapo baada ya hicho kitu kutokutokea. Anyway just a critical thinking.
 
Unajua n diyo maana JK,tangu zamani alikuwa anajikatalia kumteua Pinda kuwa waziri mkuu,alisha mjua mataitizo yake.Mara aamuru wauaji wa albino nao wauawe,mara aamuru polisi ipige watu,akiulzwa kisheria anaanza kulia.Sasa katika muktadha ule,wimbo wa upinzani ulikuwa unahusika nini?
 
Tatizo sio wimbo wa nani ila ni maudhui ya wimbo na hadhira kusudiwa, hivi unaendaje kuweka wimbo wa wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe , kwenye sherehe za kuaga spika aliyekuwa na wabunge wa upinzani na hao wa Ccm? Huu ni ujinga uliopindukia , sasa waliachiwa chakula chao walifurahia kula chote wenyewe?
Hawa watu wameiharibu kweli CCM! Unaweka wimbo wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe, huku mkielewa bado kuna utata juu ya wahusika wa mlipuko wa bomu huko Arusha lilowachanachana kiongozi wa chama hicho huko Arusha na watoto wadogo. Enzi za mwalimu aliyeamuru wimbo huo upigwe angesahaurika. Mnamuaga Sitta au mnampongeza mlipuaji wa bomu?. Siamini na wala sitaamini kuwa wabunge wote wa CCM hamna akili.
 
NJAA NI KITU KIBAYA SANA,HUYU MZEE ANAZEEKA VIBAYA,KAMA KWELI ANAWEZA KUJIDHALILISHA KUKUBALI TV NA SIJUI FENI KISA SHEREHE HAFAI ATA KUWA BALOZI WA NYUMBA KUMI,SASA ANA AGWA KWAN USPIKA ALISTAAFU AU?ALANIWE YEYE NA KIZAZI CHAKE KWA UNAFIKI WAKE MARA CCJ MARA KUNA KUNDI LA MAWAZIRI TUMEJIPANGA KUUNGANA KUGOMBEA URAIS

-----------------
IMG_0080.JPG
 
Njaa kitu kibaya sana,hasa ikifika kwenye akili
 
Hivi masisem yana akili kweli??eti zawadi ya tv na blander!!kwa lipi kwa huyu fisadi wa ccj mnafiki huyu...6 acha ukinaa mzee jua linazama!!!
 
Aibu ilioje .... .... ...... zawadi ya television kutoka kwa pesa za walipa kodi? Halafu wanaitangaza kama vile ni kitu cha maana sana, hivi kweli katika karne ya 21 zawadi kama hii inatolewa na kuonyeshwa kwa mamillioni ya walipa kodi wakati huyu Mr. 6 alishindwa kutekeleza wajibu wake na kuiacha serikali kuendelea kutapanya pesa za walipa kodi! Je, alifanya kitu gani cha maana zaidi ya kusimamia kujiuzulu kwa richimonduli na kujirizisha kwa woga? Je, lile hekalu alilojengewa ni zawadi ya aina gani? This country has gone to the dogs.

Huku ndiko kukosa dira ya nini kifanyike kuwawezesha walipa kodi kuinua maisha yao, viongozi wanajipongeza wakati hakuna la maana wanalolifanya bali kujilimbikizia utajiri kutoka migongo ya walipa kodi.

Kumbe baada ya kulazimishwa kuzima suala la Richmond bungeni wlienda kumjengea hekalu? Hapo sasa ndio inakuja kujulikana kuwa hakuwa makini na suala lenyewe bali njaa ilikuwa inamsumbua. Kwa hiyo naye aligeuka kuwa katika kundi lilelile la mafisadi. Aibu kwake na familia yake! Nilimwamini sana kumbe wapi, ni walewale. Ingawa alishafikia hatua ya kuanzisha CCJ akaambiwa tulia hapa hapa posho ipo!
 
Akili ndogo pindi inapotawala akili kubwa gues...what hapn

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwani Pinda anaumwa nini mweeeee........hata hivo na yeye kapinda kama jina lake.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Kuna mtu anaweza kusema ni kwanini CCM wanamuaga Spika (waliyemnyima' kuendelea kukalia kiti cha uspika - kwa sababu za kijinsia) miaka takribani mitatu?

Tangu mwaka 2011 walikuwa wapi? Na kama waliona anafanya kazi nzuri, kwanini walimuondoa?

FJM hii serikali ni ya mafisadi, kumbuka huu ni mwezi Juni, ni mwisho wa mwaka wa fedha, sherehe kufanyika sasa inamaanisha fungu la mgao wa bunge la mwaka wa fedha unaoisha wa 2012/2013 limebaki kubwa, wasipozitumia zitarudishwa hazina, UPO HAPO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kupeleka hospitali zikanunue dawa wanaona hasara maana wao na familia zao wanatibiwa India.
 
Back
Top Bottom