Sherehe za kumuaga Samweli Sitta zavurugika Dodoma

Sherehe za kumuaga Samweli Sitta zavurugika Dodoma

Jana kulikuwa na sherehe za kumuaga Samweli Sitta ,Spika za zamani wa Bunge zilivurigika baada ya Spika wa Bunge na Pinda kuamuru zipigwe nyimbo za Komba na mmojawapo uliopigwa ni ule wa ....wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe... Wimbo huu uliamsha hasira za wabunge wa CUF ambao waliamua kuondoka kwenye sherehe hizo bila kula chakula kilichokuwa kimeandaliwa.

Mbatia naye alitaka kuondoka ila akashikwa mkono na wabunge wa CCM naye bila aibu alirejea kwenye sherehe hizo , ila wabunge wa CUF waliamua kuondoka moja kwa moja pamoja na zawadi waliyokuwa wamemwandalia Sitta.

wabunge wa Chadema ,hawakuwepo hata mmoja .

Makubwa,walikuwa wanamuaga kwa lipi? Anaenda wapi?
 
Sita alikuwa macho kweli?? Hivi ile ofisi ya Bunge aliyojengea kijijini ikoje?
 
mimi bado naamini cuf ni chama imara cha upinzani. ieleweke kuwa kuunda serikali ya pamoja znz kulitokana na mpasuko mkubwa wa kisiasa na umoja uliyokua umeitawala znz. kutoshirikiana na chdm vizuri kumetokana na chdm kuwabagua ktk serikali ya upinzani. wamejikuta kwenye makutano lkn ni watu wenye hoja. kama chdm inahitaji kufanya vizuri na kuiarisha upinzani, lazima ishirikiane na cuf

You cant win both sides
 
Kumbe walikuwa wanawaambia hao cuf kwamba wakija kwenye sherehe wawa chane chane?
Tatizo sio wimbo wa nani ila ni maudhui ya wimbo na hadhira kusudiwa, hivi unaendaje kuweka wimbo wa wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe , kwenye sherehe za kuaga spika aliyekuwa na wabunge wa upinzani na hao wa Ccm? Huu ni ujinga uliopindukia , sasa waliachiwa chakula chao walifurahia kula chote wenyewe?
 
PM awe makini. Kama kweli alisalimia CCM oyeee katika sherehe inayojumuisha wabunge wa vyama vingine vya upinzani( cdm hawakuwepo) alifanya makosa makubwa sana, siyo uungwana hata kidogo! Kama ni kuagwa alikuwa anaagwa spika ambaye aliongoza bunge lenye wabunge wa vyama vingi na siyo CCM pekee. Aende kanisani akaungame .Siyo vizuri kufanya hivyo alivyofanya na kuendeleza manung'uniko ya watu juu yake. Kuna kitu hakipo sawa katika muono wake wa mambo.
 
Mbatia jamani!!!! au alidhani JK atamvua ubunge au uroho wa pilau na mapochopocho yaliyokuwepo. Nimetoa rai yangu humu majuzi kuwa CCM si ya kulaumiwa kwa wanayotenda kwa vile wapinzani wapo shaghla bagla. Nyerere aliposema upinzani wa dhati utatokea pindi CCM ikimeguka nionavyo ni kuwa kumeguka CCM ni ndoto bali CCM inahitaji front ambayo ni strong ya wapinzani ikiwa ni mbadala wa pande la CCM ambalo tunatarajia litameguka bila matumaini.

Kwa hali kama hii ya kina Mbatia ni ndoto kwa upinzani kutawala na Komba ataendelea kuimba "tuwachanechane"!!
 
Sita alikuwa macho kweli?? Hivi ile ofisi ya Bunge aliyojengea kijijini ikoje?
Hilo sijui, ila nafikiri kilimuuma kwani yeye wakati wake alifanya kazi na wapinzani bila kuwabagua sana na alikuwa akiwashirikisha sasa anaagwa na sherehe yake inaharibiwa makusudi ni dalili za wazi kuwa Spika Anna hakua anataka sherhe hizo zifane na zimalizike kwa furaha kwani wangepewa fursa ya kupongeza si ajabu wangemwagia sifa Six , so dawa ni kuwaudhi waondoke ili asije akapata credit kutoka kwa wapinzani ,
 
Inaonesha ni jinsi gani tuna viongozi wasio waelewa hata kidogo...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Sitta kumbe alifadhaishwa sana na kitendo hicho kwani inasemekana amelalamika kuwa haikuwa vyema wabunge aliofanya nao kazi kususia chakula cha kumuaga , sasa sijui kama kutakuwa na kuombana radhi jumatatu ama laa .......
 
Nkikua namuheshimu sana waziri pinda ila kwa haya mambo anayoyafanya sa iv nahic kama alivyoenda kule mtwara walimroga kidogo!!!!!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Jana kulikuwa na sherehe za kumuaga Samweli Sitta ,Spika za zamani wa Bunge zilivurigika baada ya Spika wa Bunge na Pinda kuamuru zipigwe nyimbo za Komba na mmojawapo uliopigwa ni ule wa ....wapinzani wakija tuwachanechane tuwatupe... Wimbo huu uliamsha hasira za wabunge wa CUF ambao waliamua kuondoka kwenye sherehe hizo bila kula chakula kilichokuwa kimeandaliwa.

Mbatia naye alitaka kuondoka ila akashikwa mkono na wabunge wa CCM naye bila aibu alirejea kwenye sherehe hizo , ila wabunge wa CUF waliamua kuondoka moja kwa moja pamoja na zawadi waliyokuwa wamemwandalia Sitta.

wabunge wa Chadema ,hawakuwepo hata mmoja .

CUF wanafiki jamani! Waseme sasa wazi nani anavuruga amani ya nchi!
 
Hamjambo jf hikh..!hivi viroba vya lumumba hikh...nimevinywa jana hadi najiskia hikh...hikh..ila mzee wenu kaharibu shereh..hikh..najiskia kutapika ila ngoja nimalize...hikh...wazazi muwe mnafikiria majina ya kuwapa watoto..hikh..,kasimama akaongea tu sherehe yote ikapindaa..natapikaa aargh hikh..najiskia tumbo langu limepindaa kwa viroba vya pindaa!
 
Back
Top Bottom