Heshima kwako mkuu@mshana jr, nakupunga mnamo mwaka 2004, kijijini kwetu kulikuja waganga wa kienyeji wakitokea maeneo ya kusini mwa Tz, kwa malengo ya kutoa na kuondoa uchawi, ktk kazi yao hio kuna nyumba moja ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na mwenye nyumba hiyo kusifika kuwa ni gwiji katika sanaa hiyo nakumbuka tulikaa hapo kuanzia mawio mpaka machewo ya jua lkn mwisho lengo la kutoa uchawi kwa gwiji huyo lilifikiwa lakini kwa shughuli pevu mno, waganga hao tuliwapa jina lao maarufu(rambaramba) na kweli walikuwa wanaramba wachawi, lakini nao waliipata shughuli nakumbuka walipoteza fahamu mara kwa mara walipokuwa wanataka kuingia ndani ya nyumba hio, kusukumwa nje kwa nguvu kwa vitu ambavyo sijavijua mpaka leo hii!! unaweza kunisaidia ni vitu gani hivyo vilivyokiwa vikiwasukuma kwa nguvu nje pindi wanapoukaribia mlango wake wa nyumba, na kwanini waganga hao walikuwa wakiingia kwa kusota sota, kubinjuka binjuka, kwa kachura kachura na kubebana zamu kwa zamu. Mwisho wa siku walifanikiwa kutoa vyungu viwili vikubwa vyeusi, tunguri nne(kubwa mbili zilikuwa na damu, ndogo moja mavumba na iliyosalia moja damu lakini ile ya wanawake) pamoja na nyoka mmoja mkubwa.
Swali langu ni kwanini walikuwa wakiingia kwa mtindo wa kubebana, kachura kachura n.k?
Hivyo vitu vilivyokutwa kwenye hizo tunguri walitueleza matumizi yake. Heshima kwako@mshana jr