Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,846
- 730,321
Kuna mfanano wa ajabu kati ya wachawi na dini ya mashetani, nao ni kutumia nyama ya binadamu na damu yake kwenye sherehe na makafara yao na sababu kubwa ni kupata ujasiri nguvu na kujiamini.
Tofauti yao ni moja tu kwamba wakati ya kishetani yakifanyika live ya kiuchawi hufanywa kimazingara, kwamba mtu ataumwa ghafla ugonjwa usioeleweka kisha atakufa, kwa mashetani mtu atatekwa na kwenda kuuliwa na huku haijalishi ni nani bali ni yeyote yule atakayepatikana.
Kitu kimoja kibaya sana kwenye sherehe za kichawi ni kwamba kama mko wachawi saba itabidi kwa miaka saba kila mmoja atoe nyama ya sherehe kwenye sherehe za mwaka na nyama hiyo ni ndugu yako yeyote unayempenda sana.
Ukikosa kutoa nyama kwa miaka miwili mfululizo jua mwaka wa tatu wewe ndio utakuwa nyama ya sherehe , na kila mwaka unaotoa nyama unapanda daraja au cheo.
Tunazo shuhuda nyingi sana humu zinahusu watu waliotolewa kafara la sherehe na ndugu zao ambao ni wachawi, hiki ni kipengele kimoja kibaya sana kinachoufanya uchawi uchukiwe na kupigwa vita kila mahali.
Kuna watu wengi sana wana hamu ya kujifunza uchawi na ushirikina lakini huko hakuna mkate na siagi, huko kuna maagano na viapo ambavyo vinawatesa wengi, si wachawi wote wanafurahia kuwepo huko wengi wanatamani kutoka lakini inakuwa ngumu, wengi wameteketeza ndugu si chini ya watano kwenye makafara na sherehe za kila mwaka, damu yao inawadai hawana amani hawana furaha na ni watu wa mashaka muda wote.
Je bado unatamani kuwa mchawi?
Tafakari mara mbili.