Shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao (Mke Wako). Kalale nao chumba kimoja

Mambo vp jamiiforums.

Ninaomba kuanza kwa kutangua kusema maneno haya machungu ambayo yatawauma wanaume wengi sana. Hata mimi nilikuwa hivi hivi. Mwanaume wengi sana huwa hawawapendi shemeji zao wa kiume siku za mwanzoni.

Just imagine, kwa akili ile ya kitoto unajua kabisa huyu ndio anataka kumchukua dada yangu aende naye kwake awe analala naye siku zote for the rest of their lives. Huwaga kunakuwa na hali fulani hivi ya wivu kwa siku za kwanza ile baadae unaona kawaida tu na maisha yanaendelea.

Kuna watu watakuwa wanajiuliza wivu huu unatokea wapi wakati huyu ni kaka na dada yake na kamwe hawawezi kuoana. Wakaka wengi wanakuwaga na wivu na dada zao na mara nyingi jaribu kuangali watoto wakubwa wa kiume wanavyowachapa wadogo zao wa kike.

Huwa wanawachapa pindi wakisikia wadogo zao wapo katika uhusiano na vijana fulani wa mtaani hapo ambao ni washkaji zao wanaokaa wote vijiweni au siku dada mdogo amechelewa kurudi nyumbani bila maelezo ya kutosha. Hiyo ni aina ya wivu wa asili ambao wanaume wengi huwa nao dhidi ya ndugu zao wa kike wakiwa katika uchumba na shemeji zao.

BACK TO THE TOPIC
=====
Ewe kijana ambaye bado haujaoa mpaka sasa, siku utakapooa, shemeji zako wa kiume wakija kukutembelea, siku hiyo usilale na dada yao. Kalale nao chumba kimoja mpige story mpaka asubuhi.

Kama wao ni watu wa tungi kama wewe, siku hiyo nunua beer, choma nyama, kunyweni mlewe, msikilize mziki. Kama ni watu wa mpira, wachukue uende nao sehemu wanayoonesha mpira tofauti na hapo kwako.

Nenda nao hata huukoooo city center Kariakoo/Posta, angalieni mpira kula nao nyama choma, inelata raha na heshima sana. Unajua, unapoona katika familia fulani, wewe unakuwa ni sehemu ya familia ile. Hivi wewe kijana unalijua hili?

Kama mama mkwe wako ana watoto 3 wa kiume, basi wewe kama shemeji wa familia ile unakuwa mtoto wake wa 4. Kwa hiyo wale shemeji zako wa kiume wanakuwa brothers to you.

Wanakuwa brothers alafu washkaji zako, tena kama umri unalingana ndio raha zaidi kwa maana hata stories pamoja na interests zinaweza kufanana kwa sehemu kubwa.
Siku hiyo ndio nawahi kulala na dada yao mapemaaa. Nawaachia remote na beers za kutosha wakeshe wanaangalia EPL mapa asubuhi wapunguze machungu ya kugongewa dada
 
Yaani aje mdogo ake wife wa kiume mmoja au kaka yake, unafika muda wa kulala namuaga wife leo nitalala na mdogo ako?? NEVER... ndo anakaa week kwangu week nzima nilale na shemeji yangu na mke wangu nimuache alale mwenyewe??? Nmekuelewa apo kwenye kutoka nao/nae sawa ila sio kulala mkuu
 
Mtoa ushauri ni MENDE mtukuka, unategemea anakushauri nini hapo
Yani aje mdogo ake wife wa kiume mmoja,au kaka ake, unafika muda wa kulala namuaga wife leo nitalala na mdogo ako?? NEVER... ndo anakaa week kwangu week nzima nilale na shemeji yangu na mke wangu nimuache alale mwenyewe??? Nmekuelewa apo kwenye kutoka nao/nae sawa ila sio kulala mkuu
 
Fikiria ndo wewe unaenda mji fulan kwa ishu zako,, unaona bora ulale kwa dada ako kwa kipindi hicho
Kama shemeji yako ni rafiki yako mnaweza ku-spend the whole night talking politics, sports, economics na mambo mengine kadha wa kadha. Siku moja tu na sio siku zooooote...
 
Fikiria ndo wewe unaenda mji fulan kwa ishu zako,, unaona bora ulale kwa dada ako kwa kipindi hicho, alafu mumewe unafika muda wa kulala anakwambia "Leo shemeji tutalala pamoja"😂😂😂
Sio shemeji, yule ni mwana (a brother)
 
kama ulikuwa hutaki majibu ya namna ile ni bora usingejiunga JF na haifichi ukweli kuwa ulichoandika ni rubbish utagunduaje?? angalia mawazo ya wachangiaji.
JF ina members zaidi ya 500,000 siwezi kuandika suala la kumfurahisha kila member mzee baba.
 
kama ulikuwa hutaki majibu ya namna ile ni bora usingejiunga JF na haifichi ukweli kuwa ulichoandika ni rubbish
Mkuu, kama ni rubbish si unaondoka tu mzee baba kabla sijakuweka ignore list. Kwani ugumu upo wapi?
 
Back
Top Bottom