Nimesikia Kiwete akiomboleza kama mtoto ati kwa kuwa kafa Mganga na Mtabiri wake!
Si mnakumbuka mwaka jana kwenye Kampeni pale Jangwani mtu mzima alipiga mweleka akapoteza Network!
Baadaye Mzee Kigagula Sheikh Yahya akasema angelimwekea ULINZI WA JINI USIOONEKANA. Na kweli jamaa baada ya hapo hakupoteza tena network!
Pia mtakumbuka kuna wakti wa mchakato wa kupata wagombea Urais ndani ya CCM na vyama vingine Sheikh akaibuka na MKWARA kuwa yeyote ATAKAYE MPINGA KIKWETE ATAKUFA KIFO CHA GHAFLA!Tukasikia watu kama Shibuda wakifyata mkia wa kugombea nafasi ya Urais ndani ya CCM baada ya mkwara wa mpiga ramli!
Jingine ni lile la Uchaguzi Mkuu wa 2005 ambapo Sheikh alisema Tanzania ingelipata Rais MWANAMKE! Baada ya uchaguzi na Kiwete akashinda kwa kishindo waandishi wa Habari walimfuata Sheikh na kumwuliza kuwa kwanini utabiri wake haukuwa sahihi! Unajua Sheikh Yahya alisema nini? Sikiliza. KWAMBA NI KWELI MSHINDI WA URAIS MWAKA 2005 ALIKUWA MWANAMKE NAYE NI RAHISI KIWETE! Kwamba Kiwete anasifa zote za kike,eti kwamba ni HANDSOMEMWENYE TABASAMU NA MPOLE na anapendwa na watu wengi ndiyo maana alishinda kwa kishindo!!!!!!!!!Tehe!tehe!tehe....! Ama kweli Wapiga ramli bwana!
Lakini baadaye imekuja kujidhihirisha kuwa kweli Kiwete ana TABIA ZA KIKE! Maana kweli ame-prove failure in leadership kwenye nafasi yake ya u-president. Mambo mengi yameenda shaghalabaghala kuanzia kwenye Chama,Serikali,Uchumi,Elimu n.k.
Kwanza baada ya kuapishwa tu mwaka 2005 aliji-suspect mwenyewe pale aliposema WAKTI WOTE NIMEVAA USO WENYE TABASAMU BUT I AM TOUGH ON ISSUES!
Test ya kwanza ilikuwa ni UFISADI WA EPA. Mzee mzima akaanza kuchemsha. Hakuna cha u-tough on issues!Tunajua kilichoendelea,tukasikia Mafisadi wanaombwa na kubembelezwa warudishe pesa walizokwapua na hawatafanywa chochote na ikawa hivyo!Kabla hajakaa sawa likaja hili la RICHMONDULI mzee AKAENDELEA KU-SMILE TU MBELE YA MAFISADI. Serikali yake ikaparaganyika baada ya swahiba wake EL kumwaga manyanga!
Kama vile alikuwa akijaribiwa na hiyo smiling-face yake likaja jingine la RADAR na mzee wa vijisenti, Andrew Chenge akatuhumiwa kuwa alikwa mwizi namba moja kwenye kesi hiyo. Baada ya kubanwa kuwa alikuwa na 2B Tshs kwenye off shore account jamaa akamwaga manyanga. Tukasubiri kuwa TAKUKURU wangeshughulikia kesi ya Rada mpaka mwisho na hatimaye kutiwa hatiani kwa AC. Wapi bwana TAKUKURU wakawa wa kwanza kumsafisha AC kuwa hahusiki na huku JKIWETE akiendelea kuangusha tabasamu KAMA MWANAMKE KABSAAAA!
Pole sana JKIWETE,sijui nani atakutabiria tena!