Sheikh wa Mkoa wa Dar: Makonda kalikoroga mwenyewe, nisihusishwe

Hizi sio lugha za kiongozi wa Dini!.
Sheikh alipaswa kuishia kwenye kukanusha tuu, hakupaswa kumbeza na kumnanga Paul Makonda kwa maneno ya hovyo ya vijiweni na mipasho kwa kitendo cha Paul Makonda kuamua kuuacha ukuu wa mkoa na kwenda kugombea Ubunge wa Kigamboni, sio kulikoroga!.

Inaonyesha huyu Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam haijui CCM!. Yaani mema yote Paul Makonda aliowatendea Waislamu wa Dar es Salaam kwa kuwajengea makao makuu ya Bakwata yenye hadhi, leo amekuwa mtu wa kubezwa kwa maneno haya ya vichochoroni na vijiweni?.

Subiria matokeo ya vikao vya uteuzi, huyu Sheikh atatafuta pa kujificha na kuficha uso wake pale Makonda atakapoteuliwa kugombea Kigamboni, kisha kupewa Wizara ya Mambo ya Ndani na kugeuka ndio bosi wa taasisi zote za dini!.

Tunawategemea viongozi na haswa wa dini kuongea kwa unyenyekevu, humility na kutumia lugha ya staha wakati wote!.
Hii sio lugha ya kiongozi wa dini!.

Nazishangaa taasisi za dini zinazoheshimika kuongozwa na watu wa hovyo wa type hii!, kama hizi ndizo lugha anazotumia in public, you can just imagine in private si ni atakuwa worse?.

Bakwata inawaokotaga wapi watu wa namna hii?!, kuna siku huyu jamaa atakuja iaibisha Bakwata ndipo Bakwata itagundua it has a wrong man at the wrong place!

P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom