Hongera sana Paul Makonda kwa kumsaidia Rais Samia

Nov 6, 2016
51
141
UKIPEWA MADARAKA FANYA KAZI, LETA UBUNIFU, TATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI, ACHA KUWASAGIA KUNGUNI VIONGOZI WENZAKO

Na Comrade Ally Maftah

Nitakuwa wa kwanza kuumgana na Ndugu Paul Makonda ( Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa ) katika kauli aliyoizungumza katika ziara zake kanda ya ziwa akiongea katika rafudhi ya kisukuma, watani zangu " SISI TUKIPEWA KAZI TUNAFANYA KAZI, HATUTAKI MAJUNGU MAJUNGU" inawezekana sijanukuu kila neno ila alimaanisha kwamba kuna aina ya watu wakishapewa kazi wanaanza kukimbilia kwa mabosi kuwadhibiti wenzao wanaojituma kutatua changamoto za wananchi

Suala hili halipo juu, hata huku ngazi za chini pia kuna watu wa namna hiyo hawataki kuona viongozi wenzao wakishughulika na matatizo ya wananchi, sijui wanawaza uchaguzi masikini ya Mungu hawa, au wanafikiri kila anayejituma na kutatua changamoto za wananchi basi anataka uteuzi,

Ndugu zangu viongozi tumeteuliwa kufanya kazi na kutatua changamoto za wananchi kwa kipindi cha miaka mitano, tosheka na nafasi uliyonayo na muda uliopewa kwenye hiyo nafasi muda ukiisha kama unafaa utachaguliwa tena, ACHA KUWASAGIA KUNGUNI WENZAKO, FANYA KAZI ZA WANANCHI, TUMRAHISISHIE KAZI DR SAMIA,

Binafsi ni shabiki sana wa Paul Makonda, nilifurahishwa na uteuzi wake na nilitabiri moto wake huu na nafikiri bado anaendeleza moto zaidi, viongozi wengi mmelala, mnawazarau wananchi kazi yetu ni UNOKO,

Ndimi
Comrade Ally Maftah
-Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
-Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
-Mtia Nia Machachali - Jimbo la Kawe 2020
IMG-20240208-WA0001.jpg
 
Ila hii nchi ina vichaa wengi Sana, trust me, sijasema mleta mada ni kichaa, hapana, nazungumzia nchi kama nchi.
 
Ujinga mtupu
 
Anayemsifia Makonda kumsaidia Samia ni mjinga tu kama wajinga wengine.

Tangu lini mwenye mamlaka akashindwa kutumia mamlaka yake kudhibiti wasiowajibika?? 🤣 🤣

Haya maigizo
 
CCM ingekuwa na kitengo cha Monitoring & Evaluation (ME)
Kisha wapime ufanisi wa makonda anakopita, naapa angetakiwa kurudisha fedha zote alizotumia na kusitisha ziara zote! anachofanya ni usanii!
 
UKIPEWA MADARAKA FANYA KAZI, LETA UBUNIFU, TATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI, ACHA KUWASAGIA KUNGUNI VIONGOZI WENZAKO

Na Comrade Ally Maftah

Nitakuwa wa kwanza kuumgana na Ndugu Paul Makonda ( Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa ) katika kauli aliyoizungumza katika ziara zake kanda ya ziwa akiongea katika rafudhi ya kisukuma, watani zangu " SISI TUKIPEWA KAZI TUNAFANYA KAZI, HATUTAKI MAJUNGU MAJUNGU" inawezekana sijanukuu kila neno ila alimaanisha kwamba kuna aina ya watu wakishapewa kazi wanaanza kukimbilia kwa mabosi kuwadhibiti wenzao wanaojituma kutatua changamoto za wananchi

Suala hili halipo juu, hata huku ngazi za chini pia kuna watu wa namna hiyo hawataki kuona viongozi wenzao wakishughulika na matatizo ya wananchi, sijui wanawaza uchaguzi masikini ya Mungu hawa, au wanafikiri kila anayejituma na kutatua changamoto za wananchi basi anataka uteuzi,

Ndugu zangu viongozi tumeteuliwa kufanya kazi na kutatua changamoto za wananchi kwa kipindi cha miaka mitano, tosheka na nafasi uliyonayo na muda uliopewa kwenye hiyo nafasi muda ukiisha kama unafaa utachaguliwa tena, ACHA KUWASAGIA KUNGUNI WENZAKO, FANYA KAZI ZA WANANCHI, TUMRAHISISHIE KAZI DR SAMIA,

Binafsi ni shabiki sana wa Paul Makonda, nilifurahishwa na uteuzi wake na nilitabiri moto wake huu na nafikiri bado anaendeleza moto zaidi, viongozi wengi mmelala, mnawazarau wananchi kazi yetu ni UNOKO,

Ndimi
Comrade Ally Maftah
-Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
-Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
-Mtia Nia Machachali - Jimbo la Kawe 2020View attachment 2897480
Huko CCM uchawa umerasimishwa kabisa. Pumbavu !!!
 
Back
Top Bottom