Sheikh Ponda amezitoa wapi hizi takwimu?

Mfano wako wa Israel na Palestina sio sahihi, Israeli wangeachwa peke yao wangeshatandikwa siku nyingi na Wapiganaji wa Kipalestina, ila kwa vile Israel inasimamishwa na mataifa ya Magharibi, USA, UK nk
 
Mimi sioni tatizo kujua idadi ya dini na waumini wake hapa nchini mbona nchi zingine takwimu kama hizi zipo wazi kuna nini Tanzania?
 
Tumefikia hapa kutokana na watawala wetu kutumia dini kama mbinu ya kujiweka madarakani. Sasa wanaposhinda, baadhi ya hawa viongozi wa dini wanafikiri ushindi huo umepatikana na waumini wa dini waliyoipigia kampenni. Mfano mdogo huko Igunga, tumeshuhudia madhehebu ya dini yakifanya kampeni za wazi na kuwahasa waumini wao kuwa ni lazima wachague chama fulani. Sasa hizi ni athari chache tu, mengi na magumu zaidi yatakuja chini ya mwamvuli huu huu.
 
Hivi shetani ana akili kuliko mungu? Haujui shatani atakundanganya ili utekeleze maovu anayotaka?Jini hawezi kuwa above god hata siku moja! Ni mawazo finyu.
 
Hivi shetani ana akili kuliko mungu? Haujui shatani atakundanganya ili utekeleze maovu anayotaka?Jini hawezi kuwa above god hata siku moja! Ni mawazo finyu.
Ukitaka kupima akili na nguvu za Shetani, hebu angalia idadi ya waumini walioko kwenye nyumba za ibada (Makanisa, Misikiti nk) na muda wanaoutumia humo, kisha ulinganishe na idadi ya watu kwenye Mabaa, Madanguro nk na muda wanaoutumia humo! ("Wanaoitwa ni Wengi lakini Wateule ni Wachache!")
 
wakitaka wajue wako wangapi wahesabu watakaojitokeza kwenye maandamao yao ya amani halafu plus watakaoshiriki sensa..its very easy kwani majina ya kiislamu si yanajulikana na sensa huwa tunarekodi majina yote bwana
 
Jamaa wanataka nchi iendeshwe kiislam. Hovyo kweli kweli
 
Wacheni masuala yasiyo kichwa wala miguu


unataka kujua shekhe ponda kazitoa wapi hizo takwimu, mimi pia ningependa.


Ushauri


mwenye namba ya shekhe ponda au email yake aiweke hapa na wanajukwaa wamtafute atuambie


wakatabahu

 
Hivi cheo cha usheikh amepewa na nani? Sheikh ponda ameishia darasa la ngapi?

Hivi huyu ni sheikh au muuni?

SHEIKH ni mtu tajiri na maarufu katika mji fulani, Hakuna cheo cha kidini ktk uislam katika hili TZ bado tunajikongoja. Hawa wanzetu elimu ya kizungu hawaitaki wanapenda kubabaisha kwa rejea za hdithi zisizo za kitaalamu wa ubinadamu!!!
 

Nafikiri kiswahili kidogo kimekuchanganya hapo.

Mimi nilivyomwelewa ni kuwa zaidi ya 80% ya waislam hawatamsikiliza maagizo ya Mufti wa BAKWATA. na amesema kuwa Waiskam ni zaidi ya 50% ya population ya waTz.

Hivyo ndivo nilivyomwelewa mimi ambaye kiswahili ni lugha ya kigeni kwangu.

Lugha yangu ya asli ni ile inayoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto.

 
Ntamaholo habari za siku mkuu,MWZ vipi?hakika ulimjibu vema huyo mtu kuhusu mgawanyo wa hekari za ardhi.
ila mi napendekeza wendelee kugoma hivyo hivyo,maana nao wameanza kuamka,na wamechoka kudanganywa hovyo na magamba,kwangu mimi naona waislamu wameamua ku-revenge baada ya kudanganywa juu ya mahakama ya kadhi,so hii ni kutaka kulipiza kisasi.

Otherwise kufanya sensa kwa kigezo cha dini hakina mantiki hata kidogo,na hata hivyo wanaweza wakatammbuana wenyewe kupitia structure ya dini yao,kama ilivyo kwa wakatoliki mfumo wao wanatambuana kuanzia kwenye Jumuia,kigango,parokia na kisha Jimbo.kama vipi wakajifunze kwa wakatoliki sio dhambi.

Ndio maana mm naona ni kulipa kisasi kwa serikali iliyowadanganya kama watoto kuhusu mahakama ya Kadhi.
 
Akiendelea na upuuzi wake msitu wa pande utamhusu. Nashauri akae kimya au arudi Burundi la sivyo Tanzania ni ya muhimu mara 1,000,0000,000 kuliko yeye.
 
Sasa Sheikh Ponda kama anajua waislam ni 80% ya watanzania wote, hivi kuna sababu gani ya kutaka kipengere cha dini kiwepo kwenye hizo karatasi za sensa?

Mi binafsi ningependa Waislam wote wogemee hiyo sensa then serikali iendelee na utalatibu wake after that tutajua tu waislam wako wangapi even though hatutajua wakristo pia wako wangapi kwasababu nchi hii ina dini nyingi including wapagani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…