Muke ya muarabu
Member
- Apr 5, 2012
- 83
- 23
Hiyo ndio kawaida ya mafisadi. Fisadi yeyote huwa hampendi mpigania haki. unataka ujue shughuli zake ivi wewe unafanya kazi gani
Pengine wewe sii Muislaam lakini pamoja na hayo nitakufahamisha. Vita ya Bakwata imeanza siku nyingi sana na ndio sababu walimuua Sheikh Kassim Bin Jumaa enzi ya Mwinyi baada ya kuanzisha chombo cha kiislaam kisichokuwa na ushirika na serikali kikiitwa BALUKTA. Chombo hicho kilipigwa vita na viongozi wake wakakamatwa kutokana na kwamba walitaka kujua undani wa mabadiliko ya mfomo wa ELIMU na AFYA. Wakahoji kwa nini waislaam hawakuhusishwa ktk maamuzi ya mfumo mpya ikiwa chombo cha dini kimepewa jukumu la kuendesha elimu na Afya nchini..
Kwa hiyo, vita hii imeendelea hadi leo na kina Ponda ambao wanaamini kabisa kuna mfumo kristu ambao kazi yake ni kuhakikisha waislaam hawafanikiwi ktk elimu na Afya. Mimi binafsi najiuliza kama hakuna usir wowote kwa nini serikali inakataa kuwashirikisha. Kwa nini tunakuwa hatuna majibu wala kutazama malalamiko ya hawa watu na kuyatafutia Ufumbuzi kama navyojiuliza ktk maswali mengi ya Ufisadi..Itakuwaje watanzania waganyike ikiwa hakuna Usiri fulani maana tutaogopa hivyo tu ikiwa kuna siri fulani zitajitokeza. Kama hakuna siri wahusishwe pia kuunda hilo shirikisho la Elimu na Afya nchini chini ya CSSC ambako kuna wachungaji tu ndio viongozi na waingizwe NECTA kwani kuhna tatizo gani?..
Sasa tunapoendelea kuficha, kukataa na kupinga kuwashirikisha ndio maana tunajenga UDINI zaidi na kuwaaminisha Waislaam kuwa kuna siri kubwa inafanyika kama madai ya kina Jumbe na Malima maana hadi leo hii hatujapewa undani wa chombo hiki.. Ni hayo tu.
Tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni kuacha kutenda haki huku tukiacha hiisia zetu ndio zifanye kazi, angalia jinsi ambavyo watu kwa kipindi kirefu wameacha kutimiza wajibu wao ili kuogopa makundi mbalimbali ya kijamii. Kwa mimtirafu hii tumeibomoa nchi yetu kwa kuondoa hali ya kuaminiana miongoni mwa jamii zinazounganisha utanzania yetu. Ndani ya Tanzana kwa sasa sio ajabu watu wakijitambulisha kwa ukabila, udini na ukanda wao. Watanzania waleo si wamoja tena!!Nini kiliizuia serikali kuchukua hatua kubwa kwa radio Imani siku za nyuma? Bado naamni serikali adilifu ingekwisha shughulikia tatizo na chuki za kidini muda mrefu nyuma.
Kuhusu swala la kuhamasisha Waislaam wasihesabiwe sijasema sio makosa isipokuwa binafsi yangu namuunga mkono kama navyomuunga mkono DR.Slaa na Mbowe ktk kuhamasisha M4C. Je, ni makosa kisheria? itategemea wewe uko upande gani..
Siwezi kuelewa kwa nini ktk sensa kuna Kipengele cha wanawake na watu msione kama serikali inataka kutuchonganisha wanaume na wanawake lakini kipengele cha Dini kiwe ni uchoanishi mkiuliza ati ili ijewe?. Kwani kile cha wanawake wamekiweka ili iweje? kwa nini tusihesabiwe wote kama mbuzi zizini isipokuwa viwekwe vipengele vyote kasoro cha dini wakati waislaam wanalalamika miaka yote tusiwasikilize. Nitarudia kusema Bakwata ni sawa na Umoja wa wanawake (UWT ya CCM) huwezi kunambia chombo hicho kinasimamia maslahi ya wanawake wote nchini. UWT sio chombo cha wanawake nchini kivunjwe kama ni makosa nifungeni maana huu ni uongo wa mchana kweupe..
Wakati wa Nyerere na Ujmaaa tulijua sababu ya kutoweka kipengele cha Dini kwa sababu ni serikali ilokuwa ikitoa huduma zote kwa wananchi toka Elimu hadi Afya leo hii serikali inashirikiana na taasisi ya Kikristu kutoa huduma hizo. Leo hii Chadema wakizuiwa kuunda Umoja wa wanawake mtakubali? Je, Wanawake wasipokuwa katika serikali yetu ama kupata ushirika watakuwa wanafanya makosa kusema huu ni mfumo dume na kuuliza why?..
huyu bwana anaweza kuipeleka Tanzania kuwa kama Ruanda asipothibitiwa mapema
nashauri apewe karipio kali na na sio kumkamata kwa sasa mda wote walikuwa wapi
SHEKHE PONDA ISSA PONDA - KWA MANENO YAKE MWENYEWE NA WAANDISHI WA HABARI ANASEMAAAAA>
POLISI NDIYO WALIOSABABISHA MAKANISA KUVAMIWA MBAGALA KWANI WALIINGIA MAKANISANI NA KUANZA KURUSHA MABOMU MISIKITINI.
RAIS KIKWETE ALIPENDELEA KUANGALIA MAKANISA MBAGALA WAKATI IPO NA MISIKITI ILIFANYIWA HUJUMA.
ANASEMA UONGOZI WA NCHI HII UMEEGEMEA UPANDE MMOJA WA IMANI.
[FONT=lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif]hivi kuna msikiti uliohujumiwa? na nani?lini? na wapi?
shekhe ponda ni janga la kitaifa[/FONT]
teh teh..huyu alishaumbuka long time.Sasa hivi haoni tena haja ya kuficha malengo yake.Siku hiz haoni ten ahaja ya kuishauri CDM na ukristu.Kaamua fuguka tuu.Nahisi Mkandara anamaslai na shekhe Ponda...:ranger:
Huo ni uzushi !!!! Kama nchi akitawala Muislamu inakuwa haina amani , mimi sikubaliani na wewe, kikubwa ni kujua hawa Waislamu wanataka nini? Kuna mambo kama ya :-
1.Baraza la Mitihani (NECTA) pamekutwa madudu mengi yamefanywa(Sipendi kuyarudia)
2. Waislamu kutaka wao wajiunge na OIC (Wakristo mpaka leo hamtaki, ila Vatcan ina Ubalozi hapa na misaada mingi inapata toka huko kwa maendeleo ya kanisa)
3. Suala la kadhi mnapinga
4. kuna fungu kubwa la fedha linakwenda kusaidia makanisa na Taasisi zake, waislamu hata sh. 1,000/=
hawapewi
.Hivi kama wewe ungekuwa ni muislamu unaweza kustahamili hali hii? Hatupendi amani ivurugike ila sio kubeza unahitaji mjadala wa kitaifa , HAWA WAISLAMU WANATAKA NINI WAFANYIWE? HAUTASIKIA TENA MALALAMIKO
Mkandara tulimbana na Jmushi1 hadi akakosa pumzi kabisa na kuamua liwalo na liwe abandua cover.Siku hizi si mahuri tena wa CDM wala Ukristu.Ni uzao wa watu wanaookoteza thoeries fulani fulani na vyeti vya kishule kwa kiasi cha kuwajengea jina katika jamii, halafu wanajiachia tetea upotofu na kuhubiria watu huo uoptoshaji.Ndio maana nasema, ndugu zetu waislam linapofikia jambo la Muislam na dini nyingine hata akili sijui huwa zinaenda wapi. Huyu Mkandara ambaye anaheshimika kwa kutoa hoja nzito na leo sijui imekuwaje. Kwake yeye, kuongoza watu kugomea sensa ni sawa, kuhamasisha watu kuvunja amani ni sawa.....
Ukitaka kupima akili na busara ya mtu msikilize pindi maslahi yake yanapoguswa. Kwa kigezo hiki, waislam wa imani kali hawafai kuwa wanasheria. Hebu fikiria watu walioelimika mfano wa Mkandara umpelekee kesi ya Ponda ya kuhamasisha kugomea sensa, unategemea nini hapo? Kila anachofanya muislam ni haki!
Wengi wanatoa mfano wa Rwanda na Burundi, ilifika wakati watu wakataka kupendekeza kabila moja Wahutu/Watutsi waende Burundi wengine Rwanda. Nashukuru Mungu busara zilitumika sasa nchi hizi watu wake wanaishi kwa amani. Jinsi wakristu tunavyowapenda ndugu zetu waislam, shukrani kwao ni kuchoma makanisa. Kama isingekuwa upendo wa wakristu, hali ya waislam nchi hii ingekuwa mbaya sana. Fikiria hapo awali, wakristu ndio walikuwa wa kwanza kumiliki taasisi nyingi hususani mashule, kwa upendo wao na uongozi bora wa Baba wa taifa, Nyerere (apumzike kwa amani) watoto wote wakasoma.
Najua haya yote waislam wanayafahau lakini bado watabisha.
Anyways, Ukristo ni upendo. Mbali na mambo yanayotendeka, viongozi wa kikristo wakitoa matamko bado ni matamko ya upendo, redio zao zinatangaza upendo. Wenzetu wanatangaza ushindi, wanawapongeza vijana waliochoma makanisa na kuiba sadaka. Huu ndio msingi wa uislam, na hapa hakuna kosa!
Jioni njema wapendwa, ni muda wa kuongeza sala kwa ajili ya amani ya nchi.
yes kama ni kwel itakuwa kheri kwani jaman ni bonge la kirusi.kwani ukiacha usheke anafanya shughuli gani zingine?
Mkuu kama bakwata hamuitaki hakuna wa kuwazuia. Kwanza nashangaa kama hamuitaki kwanini mpaka leo bado ipo. Kuna kitu hakijakaa sawa kabisa kwenye umoja wenu ama sivyo BAKWATA ingekuwa ni history tu kwa sasa.