Nakushukuru kwa swali lako. Kwanza kabisa ningependa kusema hivi.
Napenda kukuhakishia, uislamu na waislamu hawana chuki na ukristo na wakristo. Wala hatufundishwi kufanya hivyo. Napenda nikuahidi, mimi nataka kuanza mafunzo maalum kusisitizia kutokua na uhasama na wasio kua waislamu.
Baadhi ya viongozi wa makanisa, huwafundisha kwa siri sana waumini wao kuuchukia uislamu. Ndio maana vijana wengi wa kikristo hua na chuki kisirisiri dhidi ya uislamu.
Hufundishwa kuutakana na kuukashifu uislamu wakati sisi tunafundishwa kuto kumtakana nabii issa (yesu kristo), wala vitabu vya mwenyezi mungu zaburi, taurati na injili.
Uislamu unatufundisha kuishi na wasiokua waislamu kwa wema, kushirikiana katika mambo yanayo mpendeza mungu, na kuwalinda kwa mali zetu na nafsi wanapokua sisi ndio wenye dhamana ya kufanya hivyo.
Kwa hiyo waislamu wanaweza kupigana jihadi kuwalinda wasio kua waislamu ikibidi kufanya hivyo. Maana ni jukumu la waislamu kuhakisha kua kiumbe yoyote wa mungu hadhulumiwi haki yake.
Tatizo ni viongozi wachache wa kikristo ambao hutumia madhabau kujinufaisha na kupanda mbegu za chuki katia jamii hizi mbili.
Hua sisi tunasisitiza kuwaambia majirani zetu kua, yesu sio mungu, mungu sio watatu na wala yesu sio mwana wa mungu (ki-biolojia).
Hua tunalithibitisha hilo kwa maandiko yale yale yalioko ndani ya biblia.
Waislamu wote wanajua utukufu wa qur-an tukufu. Kwa hiyo yoyote atake ifanyia kitendo cha dharau, hata watoto wanaweza kumhukumu.