Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hivi wewe mzee haunaga stori nyingine zaidi ya hizi ,kila siku waislamu na uhuru .....Waliofanya mapinduzi Zanzibar ni kina nani ? Mbona haijawahi kutokea Rais wa Zanzibar Mkristo ?

Yaani unavyo ongelea hili swala la Waislamu na uhuru utafikiria nchi hii haikuwa na watu wa dini nyingine walikuja baada ya kupata Uhuru sijui ulioletwa na Waislamu

Sijui kizazi chako utakuwa umewalisha sumu kiasi gani
Yamakagashi,
Mbona unaanza kwa lugha kali isiyo na adabu na kujawa na ghadhabu?

Ikiwa ushakiri kuwa mie ni mzee wajibu wako wewe ikiwa ni kijana ni
staha si matusi.

Nina stori nyingi sana mbali na mchango wa Waislam katika uhuru wa
Tanganyika.

Nimealikwa kwingi duniani kuzungumza historia hii ambayo wewe kwa
bahati mbaya inakuchoma.

Na hii kuchomwa na historia hii hauko peke yako.

Miaka 50 iliyopita palifanyika njama ya kuifuta kabisa historia hii isiwe
historia ya Tanganyika.

Hawa walikuwa wakichonotwa na historia hii kama wewe hii leo hapa
inavyokutaabisha.

Lakini huna sababu ya wewe kujiumiza nafsi yako.

Ikiwa wewe unakereka na historia hii pita usisome kwani hujalazimishwa
na mtu yoyote kunisoma.

Lakini ukweli utabakia kuwa historia hii inapendwa sana na wengi na ndiyo
pita utaona ikiwa sijatokea watauliza Mzee Mohamed mbona yuko kimya?
 
Sheikh anataka kama ilivyo NSSF jinsi yule Dr. Dau alivyofanya au? Maana pale wamejaa wa upande wa dini ile tu, kama ilivyokuwa TRA walijaa wa K'njaro tu. Zama hizo zimepitwa na wakati.
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.

FaizaFoxy unasemaje kuhusu hili swala
 
Sidhani kama Rais huteua watu kwa kuhoji dini zao. Pia kuna ukweli kuwa taasisi za elimu za Kikristo zimekuwa zikijitahidi sana kuendeleza watoto kielimu tofauti na taasisi nyingi za Kiislamu ambazo zimekuwa zikihimiza zaidi elimu ya Madrassa na lugha ya Kiarabu.
Muongo ww hya mambo yameisha toka enzi ya miaka ya 1980 ss hv kila mtu anagonga msuli tu
 
Yamakagashi,
Mbona unaanza kwa lugha kali isiyo na adabu na kujawa na ghadhabu?

Ikiwa ushakiri kuwa mie ni mzee wajibu wako wewe ikiwa ni kijana ni
staha si matusi.

Nina stori nyingi sana mbali na mchango wa Waislam katika uhuru wa
Tanganyika.

Nimealikwa kwingi duniani kuzungumza historia hii ambayo wewe kwa
bahati mbaya inakuchoma.

Na hii kuchomwa na historia hii hauko peke yako.

Miaka 50 iliyopita palifanyika njama ya kuifuta kabisa historia hii isiwe
historia ya Tanganyika.

Hawa walikuwa wakichonotwa na historia hii kama wewe hii leo hapa
inavyokutaabisha.

Lakini huna sababu ya wewe kujiumiza nafsi yako.

Ikiwa wewe unakereka na historia hii pita usisome kwani hujalazimishwa
na mtu yoyote kunisoma.

Lakini ukweli utabakia kuwa historia hii inapendwa sana na wengi na ndiyo
pita utaona ikiwa sijatokea watauliza Mzee Mohamed mbona yuko kimya?
Ulicho ulizwa sicho ulicho kijibu ,Waliofanya mapinduzi Zanzibar ni kina nani ? Mbona Zanzibar haijawahi kuwa na raisi mkristo ?

Kwa bahati nzuri mimi sio muumini wa hizi dini zenu mlizoletewa hivyo hakuna kinachoweza kunichoma kutoka kwenye mada zako za uislamu sijui na uhuru ,umealikwa duniani sijui kuelezea nini Pakistan ulifika ? umesikia kimetokea nini Msikitini? Kajilipua kijana kuwauwa waislamu wenzie

Pamoja na kwamba dini zenu hazinihusu ila jamii inayo nizunguka wanaamini katika dini hizo na anapotokea mtu kama wewe kila siku ni kupandikiza chuki tu nachelea kuona walichofanya Serikali juu ya wale Masheikh wa uhamsho ni sahihi kabisa

Sijui hata kwanini nilikuta mzee

Kuitwa mzee ni heshima sio umri ulioishi hapa duniani
Sikupaswa kukupa heshima hiyo
 
Kumbuka pia mlipewa bure chuo cha Tanesco pale Morogoro. Watu hamridhiki.
Vile vile kumbuka dhiki kubwa imewashika hasa jamaa zako wa kule kijiji sijakuambia wewe mwenyewe kodi ya pango hapo kinyerezi inavyokupeleka mbio.
 
Mtu anakaa anaanza kuhesabu watu wa dini yake wapo wangapi serikalini??

Ni mawazo ya kipumbavu..............

The Book,
Huenda Mwalimu Nyerere kasahau historia ya TANU na vipi yeye aliingia
katika siasa za Dar es Salaam mwaka 1953 alipochaguliwa kuwa rais wa
TAA tarehe 17 April 1953 alipomshinda Abdulwahid Sykes katika Ukumbi
wa Arnautoglo.

Historia ya uchaguzi huu haieleweki na wengi.
Mwalimu anasema suala la dini halikuwepo.

Ukweli ni kuwa lilikuwapo toka siku ya kwanza.

Abdulwahid Sykes na Ally Mwinyi Tambwe walikwenda kujadili suala la
uchaguzi wa 1953 Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu.

Hamza alimwomba Abdul ampishe Nyerere katika nafasi ya urais na amsaidie
achukue nafasi hiyo ili 1954 watakapounda TANU Nyerere awe ndiye kiongozi
wa kuongoza madai ya uhuru wa Tanganyika.

Mufti Sheikh Hassan bin Amir yeye aliongoza kampeni za kukubalika Nyerere
mara tu TANU ilipoundwa 1954.

Bahati mbaya historia hii leo haithaniwi na juhudi kubwa ilifanyika kuifuta.

Nimgeweza kuandika mengi kuhusu hili suala la dini lakini ikiwa msomaji anataka
kujua historia hii asome kitabu cha Abdul Sykes.

Mle nimeeleza kila kitu.
 
Usomi wa kubagua watu huo ni Usomi usomi ni kuondoa ujinga ukimbagua mtu maana yake huna elimu mnaelimu za kubagua watu kwa imani zao yaani nikiwa mkiristo mungu tayari keshanipa akili ya kusoma hapo hapo ni msomi huu ujanja ujanja haukubaliki kwa hiyo uongozi uwe wa Christian tupu sisi Islamic tuwe tunawapigia kura kuwaingiza mamlakani ukiangalia hizo takwimu zinatia hasira masisiemu 2020 mjitafakari mmelikoroga mapema
 
Sheikh anataka kama ilivyo NSSF jinsi yule Dr. Dau alivyofanya au? Maana pale wamejaa wa upande wa dini ile tu, kama ilivyokuwa TRA walijaa wa K'njaro tu. Zama hizo zimepitwa na wakati.
Usisahau na pale CRDB walivyojaa wana vigango na hasa kiukanda zaidi na mle Kigango cha Tanesco na ... na ...,

Kijana njoo taratibu utaumizwa na mengi, vyuo na shule zishafunguliwa.
 
Kuna kitu mm nimekigundua niko tayar kukosolewa, madereva wengi na makonda nchi hii ni muslims, wanamuziki wengi nchi hii n muslims, wachuuzi wengi na madalali nchi hii n muslims, wacheza mpira wengi nchi hii ni muslims, ofisi nyingi za serikali na taasisi zake zinaendeshwa na christians.......
 
Ulicho ulizwa sicho ulicho kijibu ,Waliofanya mapinduzi Zanzibar ni kina nani ? Mbona Zanzibar haijawahi kuwa na raisi mkristo ?

Kwa bahati nzuri mimi sio muumini wa hizi dini zenu mlizoletewa hivyo hakuna kinachoweza kunichoma kutoka kwenye mada zako za uislamu sijui na uhuru ,umealikwa duniani sijui kuelezea nini Pakistan ulifika ? umesikia kimetokea nini Msikitini? Kajilipua kijana kuwauwa waislamu wenzie

Pamoja na kwamba dini zenu hazinihusu ila jamii inayo nizunguka wanaamini katika dini hizo na anapotokea mtu kama wewe kila siku ni kupandikiza chuki tu nachelea kuona walichofanya Serikali juu ya wale Masheikh wa uhamsho ni sahihi kabisa

Sijui hata kwanini nilikuta mzee

Kuitwa mzee ni heshima sio umri ulioishi hapa duniani
Sikupaswa kukupa heshima hiyo
Yamagashi,
Umeghadhibika.
Naona lugha inazidi kujaa kejeli.

Hivi inakuwa tabu kufanya mjadala.

Nimeandika mengi hapa JF lakini inaelekea wewe ni mpya
humu.

Unaweza kusoma mengi niliyoandika na pia kuona video
kuhusu Zanzibar hapa: www.mohammedsaid.com
 
Nimeyapenda sana maneno haya katika bandiko la mleta mada...

....Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.
.......Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini.
Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?
 
The Book,
Huenda Mwalimu Nyerere kasahau historia ya TANU na vipi yeye aliingia
katika siasa za Dar es Salaam mwaka 1953 alipochaguliwa kuwa rais wa
TAA tarehe 17 April 1953 alipomshinda Abdulwahid Sykes katika Ukumbi
wa Arnautoglo.

Historia ya uchaguzi huu haieleweki na wengi.
Mwalimu anasema suala la dini halikuwepo.

Ukweli ni kuwa lilikuwapo toka siku ya kwanza.

Abdulwahid Sykes na Ally Mwinyi Tambwe walikwenda kujadili suala la
uchaguzi wa 1953 Nansio, Ukerewe nyumbani kwa Hamza Mwapachu.

Hamza alimwomba Abdul ampishe Nyerere katika nafasi ya urais na amsaidie
achukue nafasi hiyo ili 1954 watakapounda TANU Nyerere awe ndiye kiongozi
wa kuongoza madai ya uhuru wa Tanganyika.

Mufti Sheikh Hassan bin Amir yeye aliongoza kampeni za kukubalika Nyerere
mara tu TANU ilipoundwa 1954.

Bahati mbaya historia hii leo haithaniwi na juhudi kubwa ilifanyika kuifuta.

Nimgeweza kuandika mengi kuhusu hili suala la dini lakini ikiwa msomaji anataka
kujua historia hii asome kitabu cha Abdul Sykes.

Mle nimeeleza kila kitu.
Mbona sioni udini kwenye andiko lako mzee?

huyu Hamza alikuwa dini gani?
 
Nimeyapenda sana maneno haya katika bandiko la mleta mada...

....Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.
.......Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini.
Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?
Ingekuwa vyema kama wangeuliza,mbona wenzetu wenye diploma ni wachache kwenye awamu ya 5?
 
Yamagashi,
Umeghadhibika.
Naona lugha inazidi kujaa kejeli.

Hivi inakuwa tabu kufanya mjadala.

Nimeandika mengi hapa JF lakini inaelekea wewe ni mpya
humu.

Unaweza kusoma mengi niliyoandika na pia kuona video
kuhusu Zanzibar hapa: www.mohammedsaid.com
Ni bora nikasome hadithi za kina Tola na kula gizani au bulicheka na wengineo kuliko kupitia hiyo tovuti yako

Hakuna chochote cha manufaa nitakachopata humo zaidi ya sumu na chuki zako za kidini ambazo kwangu hazina maana yoyote

Una uhakika mimi ni mpya humu jamvini au kisa umeona ID ya juzi basi unajifariji

Wabilah Tawfiq

Aslaam Aleykum
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom