Sheikh Jongo asema ujenzi wa msikiti wa Kinondoni haukuombwa na Hayati Magufuli kama ilivyodaiwa

Mwenzenu naona aibu sana. Jinsi Magufuli alivyokuwa akijitapa mara atembelee Msikiti huku kavaa Kanzu, Mara amtume Makonda, mara aipige biti. Nimeona aibu sana kwa jinsi alivyokuwa akijitapa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Februari, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Mhe. Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016.

Akiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally, Mhe. Rais Magufuli amejionea kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la Msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa, na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa Msikiti huo.

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu Msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya Ibada.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa Msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.

Akiwa na viongozi wenzake wa BAKWATA, Sheikh Mkuu Aboubakar Zubeir bin Ally ameongoza Dua ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania dhidi ya maradhi ya homa ya virusi vya corona, kudumisha amani na utulivu na kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu ufanyike vizuri na kwa amani.
 
Mwenzenu naona aibu sana. Jinsi Magufuli alivyokuwa akijitapa mara atembelee Msikiti huku kavaa Kanzu, Mara amtume Makonda, mara aipige biti. Nimeona aibu sana kwa jinsi alivyokuwa akijitapa.
1711449163268.png
 
acheni unafiki huo huyo mzee kakosa la kusema kwanini hakusema wakati yupo na mpaka muft alisema mwenyewe kuwa magufuli ndiyo aliomba ujengwe inamaana huyu jamaa na mufti nani muongo?
Huyu jamaa ni "mtumiwa" wa genge linalopigana na "Makaburi".

Ndio maana tunaona wakijitahidi kuwapanga kwa zamu!

Leo ni huyu na wiki iliyopita alikuwa ni CDF Mabeyo!

Lakini watanzania sio wote ni wapumbazika!

Tunawaona na kuwapimia taraatiiibu!
 
Ila kama kuna binadamu anaishi kwa mateso hii dunia ni kikwete, seems like he has always something to prove, I mean, huyu jamaa amekuwa raisi kwa miaka 10 lkn bado anaona kama kuna pengo kwenye maisha yake, kuna watu wanahitaji therapist kwa maana unashindana hata mtu aliyekwisha kufa na hata rudi tena? Duh …
 
View attachment 2945052
Wakuu,

Mwenzenu naona aibu sana. Jinsi Magufuli alivyokuwa akijitapa mara atembelee Msikiti huku kavaa Kanzu, Mara amtume Makonda, mara aipige biti. Nimeona aibu sana kwa jinsi alivyokuwa akijitapa...

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Anyway tuacheni kupoteza muda kupambana na marhamu. Hizi siasa za kipuuzi tu wala hazina tija. Hata madaraja na barabara ya kimara Kibaha. Wanasema Magufuli wakati ni kazi ya Kikwete.
 
Back
Top Bottom