Sheikh Jongo asema ujenzi wa msikiti wa Kinondoni haukuombwa na Hayati Magufuli kama ilivyodaiwa

Dunia haina siri, waislamu wamefunguka kwamba ule msikiti ambao JPM alikuwa anatamba kuwaombea waislamu wajengewe kumbe ni kazi iliyoanza enzi ya JK mpaka Mufti akasafiri kwenda kwa nchi iliyofadhili ili wakajadiliane.

Iwe bhojo!
View attachment 2945023
Huo ni unafiki kwanini hakusema wakati magufuli yupo hatuwezi kusikiliza maneno ya upande mmoja tu kama kwenye kanga angesema na Magufuli yupo ili tusikie naye atasemaje hapo mzee umefeli pakubwa sanaaaaaaaaaa
 
Dunia haina siri, waislamu wamefunguka kwamba ule msikiti ambao JPM alikuwa anatamba kuwaombea waislamu wajengewe kumbe ni kazi iliyoanza enzi ya JK mpaka Mufti akasafiri kwenda kwa nchi iliyofadhili ili wakajadiliane.

Iwe bhojo!
1711447829153.png
 
Shehe aache uongo. mfalme wa 6 wa Morocco alitembelea Tanzania october mwaka 2016, je mwaka huo rais alikuwa Kikwete?

Ukweli ni kwamba ujenzi wa msikiti uliombwa kwa mfalme huyo baada ya kufika Tanzania.

Hata kama huyo mzee hampendi magufuli. teknolojia haidanganyi.. tazameni video wenyewe mumuone mfalme mwenyewe wa morocco anavyokubali kwa JPM



 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Februari, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Mhe. Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016.

Akiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally, Mhe. Rais Magufuli amejionea kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la Msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa, na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa Msikiti huo.

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu Msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya Ibada.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa Msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.

Akiwa na viongozi wenzake wa BAKWATA, Sheikh Mkuu Aboubakar Zubeir bin Ally ameongoza Dua ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania dhidi ya maradhi ya homa ya virusi vya corona, kudumisha amani na utulivu na kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu ufanyike vizuri na kwa amani.
 
Back
Top Bottom