Sheikh Gologosi afariki katika ajali mbaya

Duh GT mkuu hata kama humpendi kiasi hicho haifai ndugu yangu.. Tunajua Bakwata ni sumu ya Waislaam lakini inapofikia kifo mkuu wangu basi hata sema - Bwana ndiye aliyetupa, Bwana ametwaa (Ina Lillah wa ina Ilaihi Rajiun) inatosha...

unaanza ku sound kama mgala mambo haya umeyaanza lini?

huyu gorogosi hana tofauti na Abuu lahabi

serves him right au unataka nikukumbushe ndugu yangu Muyaka anvyosema?

Muuyaka anasema:

YU WAPI FIRAUNI
YU WAPI KARUNI
NA SHADADI MALUUNI
WOTE WAMEANGAMIA


narudia,kama alivypsema marhum sheikh Hemed Bin Jumaa pale uwanja wa taifa Juliasi nyerer alipokufa, MWENYEZI MUNGU AMPELEKE ANAKOSTAHILI...

Atakaye sikitika sana kwenye hili ni swahiba wake bwana Reginald Mengi
 
Mungu aiweke roho ya Marehemu Sheikh Gorogosi mahali pema peponi.Amen. TBC 1 wametangaza katika habari kwa ufupi ya saa 10 kamili.

kwa waislam siku yake ya peponi bado kwa sababu itabidi kwanza afufuliwe siku ya kiama kisha asomewe mashtaka yake hapo ndio itaamuliwa ataenda FIN'AARI JAHANAM au vipi

the bottom line huyu huwezi kumfananisha na al Marhum sheikh NURDIN SHADHLY au HEMED BIN JUMAA BIN HEMED kwani pamoja na mambo mengine wao walikuwa wamebobea kwenye EI'LM tofauti na Gorogosi
 
Jamani Jamani...
Mungu ni lazima aogopwe kwa kweli. Kwa maana yeye ndiye mkuu na muweza wa vyote. Shekh Gologosi tulimpenda sana, ila ALLAH alimpenda zaidi. Tumwombee kwa Mungu ili aweze kufika kuzimu salama.

TUNAUNGANA NA NDUGU WA MAREHEMU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAJONZI
 
sote ni wa mwenyezi mungu na kwake ndio marejeo,

Mungu awape subira wafiwa,

pana mwenye habari zaidi kuhusu ajali? je alikuwa peke yake tu au pana majeruhi nk
 
i HOPE SERIKALI HAITOTUMIA KODI ZETU KUGHARAMIA MAZISHI YAKE MAANA HAKUAJIRIWA NA SERIKALI

WAPO AKINA MENGI AMBAO NAJUA WATAJITOLEA KWA KILA HALI INCLUDING KUONYESHA MAZISHI LIVE KWENYE ITV
 
Thread inahusu taarifa ya kifo..wengine badala yake wanafanya hii kuwa sehemu ya swearing kana kwamba wao hawataonja mauti.
 
Thread inahusu taarifa ya kifo..wengine badala yake wanafanya hii kuwa sehemu ya swearing kana kwamba wao hawataonja mauti.
bwana Muyaka anaendelea kusema hivi:
ZAO ZILIPOKWISHA
ZIRAILI KAWAFISHA
WAMEYAWACHA MAKASHA
NAMAMBO HAYA NA HAYA


haya hebu tuonyeshe wapi watu wameswear?
 
i HOPE SERIKALI HAITOTUMIA KODI ZETU KUGHARAMIA MAZISHI YAKE MAANA HAKUAJIRIWA NA SERIKALI

WAPO AKINA MENGI AMBAO NAJUA WATAJITOLEA KWA KILA HALI INCLUDING KUONYESHA MAZISHI LIVE KWENYE ITV
GT, surely unaweza kutafuta sehemu nyingine to settle the score, hpa ni kushoto kidogo mkuu
 
R.I.P. Gorogosi. Mungu akuhukumu kwa nafsi yako na siyo kwa maneno ya binadamu. Najua Mungu alikukujua zaidi. Nakutakia pumziko la milele.
 
kwa waislam siku yake ya peponi bado kwa sababu itabidi kwanza afufuliwe siku ya kiama kisha asomewe mashtaka yake hapo ndio itaamuliwa ataenda FIN'AARI JAHANAM au vipi

the bottom line huyu huwezi kumfananisha na al Marhum sheikh NURDIN SHADHLY au HEMED BIN JUMAA BIN HEMED kwani pamoja na mambo mengine wao walikuwa wamebobea kwenye EI'LM tofauti na Gorogosi
G.T,
Ungemsema unavyotaka pale wakati yupo hai,pengine angeweza kujitetea huo U Abu Lahabi wake,saivi ameshafariki tumuombee Mw'Mungu ampeleke anapostahiki(kama alivyosema Shk. Hemed bin Jumaa kwa Nyerere)
 
Halisi/Invi..rekebisha opening sentence, kifo kisomeke tangu mwanzo
Thanks mkuu, hii ungeituma kama report tungeifanyia kazi haraka kuliko kuandika kama post.

BTW: Ninafanya updates kwenye 1st post kila zinapotufikia...
 
unaanza ku sound kama mgala mambo haya umeyaanza lini?

Duh, yamekuwa hayo tena..sasa kama wewe unachohoji ni Wakristu kusema Bwana au kitu gani?..fikra zako ziko chini tu ktk maswala! yaani unaposikia neno Bwana basi unarudi ktk ubwana wa ngono..taabu kweli kweli..
Wagala ni sisi wote ikiwa ni pamoja na wewe mkuu soma vizuri Biblia..
 
_____________________________
Reported Earlier:

Kuna taarifa kuwa Sheikh Gologosi kapata ajali mbaya muda si mrefu. Hatuna uhakika wa maisha yake, tuombe Mungu. Tunafuatilia usahihi wa taarifa husika.
_____________________________

Update 1.


Confirmed:

Kaimu Mufti Mkuu, Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki katika ajali mbaya akiwa katika safari kusini mwa Tanzania. Aliondoka Dar leo kwa ndege kwenda Lindi kupitia Mtwara, akashuka na ndege mtwara kwenda Lindi gari ikapasuka tairi la mbele.

i470_gologosi.jpg


Mwenye miwani ndiye marehemu Sheikh Suleiman Gologosi akiwa kwenye mahafari ya shule ya Sekondari Jitegemee Oktoba 2007



mwinyi110309.jpg

Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye mkesha wa Maulid katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kulia ni kaimu Mufti Sheikh Suleiman Gologosi.


********************
Update 2.

Marehemu alikuwa akitokea Mtwara kwenda Lindi na kwenye gari walikuwa watatu, marehemu na abiria mwingine mmoja pamoja na derava wao aliyetambulika kwa jina la Maguo aliyewahi kuwa mfanyakazi wa Bandari (Mtwara).

Marehemu alifariki papo hapo na abiria mwingine na dereva walikimbizwa kwenda Hospitali.

Gari walilokuwa wanatumia ni T968ARC Toyota Land Cruiser Prado ambalo liliacha njia na kupinduka.

********************
Update 3.

Aliyekuwa anaendesha gari (dereva) ndiye mmiliki wa gari hilo na aliwahi kushiriki mchakato wa kugombea kiti cha ubunge Lindi kwa ticket ya CCM mwaka 2005 na akashindwa kwenye kura za maoni na mpaka sasa alikuwa anafanya kampeni za chinichini kujiimarisha ili agombee tena.

Majeruhi mwingine (abiria) ametambulika kwa jina la CPT Aboubakar Fundi lakini haijathibitishwa kama bado ni askari wa JWTZ au kishastaafu.

Bado haijathibitika majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Mission Nyangao au ile ya mkoa wa Lindi.

Mwili wa marehemu umeondolewa dakika chache zilizopita kwenye eneo la tukio na askari polisi na inaelekea wanaupeleka Hospitali ya mkoa wa Lindi.

Marehemu alikuwa pia ndiye Sheikh mkuu wa mkoa wa Lindi.

thanks a lot for the news!
 
Back
Top Bottom