Sheikh Gologosi afariki katika ajali mbaya

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
_____________________________
Reported Earlier:

Kuna taarifa kuwa Sheikh Gologosi kapata ajali mbaya muda si mrefu. Hatuna uhakika wa maisha yake, tuombe Mungu. Tunafuatilia usahihi wa taarifa husika.
_____________________________

Update 1.

Confirmed:

Kaimu Mufti Mkuu, Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki katika ajali mbaya akiwa katika safari kusini mwa Tanzania. Aliondoka Dar leo kwa ndege kwenda Lindi kupitia Mtwara, akashuka na ndege mtwara kwenda Lindi gari ikapasuka tairi la mbele.

i470_gologosi.jpg

Mwenye miwani ndiye marehemu Sheikh Suleiman Gologosi akiwa kwenye mahafari ya shule ya Sekondari Jitegemee Oktoba 2007

mwinyi110309.jpg

Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye mkesha wa Maulid katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kulia ni kaimu Mufti Sheikh Suleiman Gologosi.

********************
Update 2.

Marehemu alikuwa akitokea Mtwara kwenda Lindi na kwenye gari walikuwa watatu, marehemu na abiria mwingine mmoja pamoja na derava wao aliyetambulika kwa jina la Maguo aliyewahi kuwa mfanyakazi wa Bandari (Mtwara).

Marehemu alifariki papo hapo na abiria mwingine na dereva walikimbizwa kwenda Hospitali.

Gari walilokuwa wanatumia ni T968ARC Toyota Land Cruiser Prado ambalo liliacha njia na kupinduka.

********************
Update 3.

Aliyekuwa anaendesha gari (dereva) ndiye mmiliki wa gari hilo na aliwahi kushiriki mchakato wa kugombea kiti cha ubunge Lindi kwa ticket ya CCM mwaka 2005 na akashindwa kwenye kura za maoni na mpaka sasa alikuwa anafanya kampeni za chinichini kujiimarisha ili agombee tena.

Majeruhi mwingine (abiria) ametambulika kwa jina la CPT Aboubakar Fundi lakini haijathibitishwa kama bado ni askari wa JWTZ au kishastaafu.

Bado haijathibitika majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Mission Nyangao au ile ya mkoa wa Lindi.

Mwili wa marehemu umeondolewa dakika chache zilizopita kwenye eneo la tukio na askari polisi na inaelekea wanaupeleka Hospitali ya mkoa wa Lindi.

Marehemu alikuwa pia ndiye Sheikh mkuu wa mkoa wa Lindi.

Last edited by a moderator:
Duh Tumuombee kwa Mungu ili apate afya na kuendelea na majukumu yake ya kazi ya Mungu, Pole wote
 
Amepata ajali eneo la Madango kati ya Mtwara na Lindi na polisi waliopo jirani na eneo la tukio wamesema, "kuhusu kufa sio swali tena ni kwamba amekufa"

Kama ni kweli, Ina Lilah wa Ina Ilaihi Rajiun
 
Duuh! Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana na lihimidiwe.

Ina Lilah wa Ina Ilaihi Rajiun
 
Last edited:
Kwenye chain of command, huyu ndiye aliyekuwa the brain behind Sheikh Mkuu.
Ina Lilah wa Ina Ilaihi Rajiun
 
Jamani wadau vipi mbona mnachanganya mambo, Amefariki au Amepata Ajali?? tunaomba tujue basi haraka
 
Confirmed..kafa, huyu si alikatwa mkono au sjui kidole..lakini its one of the two

lakini ndio ma sheikh wa BAKWATA hao, yule sheikh mkuu naye alikatwa mguu lakini waandishi wakapigwa marufuku kuripoti kuwa alikatwa mguu..kisa imani za shirikina haafu kila kukicha wanasema kuna conspiracy toka kwa wakristo na kanisa!

I wonder how much MENGI atakuwa kasikitishwa na kifo cha huyu bwana maana Gorogosi na sheikh mkuu ndio watu wake wa karibu sana hawa na kama mtu aliona ile dvd ya Mengi kupewa tuzo na BAKWATA you could see hawa wawili walikuwa ma swahiba wakubwa sana

MWENYEZI MUNGU AMFIKISHE GOROGOSI ANAPOSTAHILI
 
Kwenye chain of command, huyu ndiye aliyekuwa the brain behind Sheikh Mkuu.
Ina Lilah wa Ina Ilaihi Rajiun

hebu tupumzishe mjomba...mambo hayo tuulize sisi, hakuna cha brain wala nini Sheikh mkuu anaogopwa na kila mtu maanawanasema majini alonayo hayawezekaniki na ukiingia kwenye anga zake basi ukae mkao wa kula

hakuna brains zozote ..kungekuwa na brains basi wasingekubali lile dula liuze pombe pale nje ya ofisi za BAKWATA shule ya Kindondoni Muslim..mpaka waislam wakaja kuliondoa kinguvu

sasa kama angekuwa na hizo brains mbona hawakuzitumia wakati wa kusign contract na tenants?
 
Confirmed..kafa, huyu si alikatwa mkono au sjui kidole..lakini its one of the two

lakini ndio ma sheikh wa BAKWATA hao, yule sheikh mkuu naye alikatwa mguu lakini waandishi wakapigwa marufuku kuripoti kuwa alikatwa mguu..kisa imani za shirikina haafu kila kukicha wanasema kuna conspiracy toka kwa wakristo na kanisa!

I wonder how much MENGI atakuwa kasikitishwa na kifo cha huyu bwana maana Gorogosi na sheikh mkuu ndio watu wake wa karibu sana hawa na kama mtu aliona ile dvd ya Mengi kupewa tuzo na BAKWATA you could see hawa wawili walikuwa ma swahiba wakubwa sana

MWENYEZI MUNGU AMFIKISHE GOROGOSI ANAPOSTAHILI
Duh GT mkuu hata kama humpendi kiasi hicho haifai ndugu yangu.. Tunajua Bakwata ni sumu ya Waislaam lakini inapofikia kifo mkuu wangu basi hata sema - Bwana ndiye aliyetupa, Bwana ametwaa (Ina Lillah wa ina Ilaihi Rajiun) inatosha...
 
Mungu aiweke roho ya Marehemu Sheikh Gorogosi mahali pema peponi.Amen. TBC 1 wametangaza katika habari kwa ufupi ya saa 10 kamili.
 
I wonder how much MENGI atakuwa kasikitishwa na kifo cha huyu bwana maana Gorogosi na sheikh mkuu ndio watu wake wa karibu sana hawa na kama mtu aliona ile dvd ya Mengi kupewa tuzo na BAKWATA you could see hawa wawili walikuwa ma swahiba wakubwa sana
Huyu ndiye alikaimu Sheikh mkuu kipindi chote Sheikh Mkuu alipokuwa anaumwa. Hivyo sio suala la Mangi kuhuzunika. Ni msiba wa taifa.
Nijuavyo mimi, Mangi hana maswahiba wala permenent friends, anao aliances for his stragetic missions. Aliikumbatia Bwakata ili amchomee utambi Manji kwa kujifanya anawapenda sana Waislamu.
Hata sasa anavyowakumbatia kundi la kina Sendeka, Kimaro, Seleli na wengineo kwa kutembelea majimbo yao huku akimwaga senti, its not friendship, its a mission,
RIP Gorogosi.
 
Poleni wote na pia na kuna haja ya kuangalia kwa makini sana ajali hizi na kujua chanzo chake kama ni barabara ni kazi ya CCM kujenga barabara zote
 
Back
Top Bottom