Share nasi matukio yako ya ukuaji

Dah hatari sana .
Mpende sana mama lakini nahisi sasa umebadilika maana hamkawii nyie watu wa hivi tukikutana bar mnatutegeshea tunaenda maliwato mnakojolea kwenye vinywaji vyetu [emoji848]

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Mama bahati mbaya alifariki, ila Vitu ambavyo namwomba Mungu mbegu zetu hizi zinazoonekana kupitia kwa Mke wangu zisinisumbue kama mimi nilivyokuwa msumbufu.... Hahahahah.. nakumbuka wakati tupo kwenye kuhangaika kwenye maisha kuna jamaa alivamia Pombe za bure kwenye sherehe aisee kalewa chakari, tukanunua mayai ukakoroga na unga wa ngano kidogo aisee tukammwagia jamaa kwenye suruali hahahahahaha. Mwamba alivyoaamka akasema hadi luisMkinga mwanangu hujanitetea.. aisee nilicheka kinoma kuamini tulimwonyesha video yake wakati tunafanya hivyo vituko.
 
Umetisha mkuu,hiyo story yako ya primary ni kama mimi tu,nilikuwa mpole sana hata wachapwe darasa Zima mi nlikuwa sichapwi,nilikuwa napangiwa tu kufanya usafi ofisi za walimu.
 
Kuna mtaa wa msisiri kinondoni pembeni kuna soko kubwa tu.
Soko lipo katikati ya mitaa mingi ila upande wa tulipo kuwa tunakaa kabla hujafik ndanindan unakutans na butcher safi tu kipind hiko.

Ilikuwa jioni tupo sokoni sijui tulifata nini kushangaa shangaa me nilikuwa nachezea zipu y kibukta changu cha jeans na zipu ya chuma si kigovinda changu kikanasa kwenye zipu

Nilitoa kilio sitokuj sahau soko lote likaja kwangu yule mwenye butcher alivyo kuja akasema kama ni govinda basi wanitahiri pale pale alooooo nilipiga yowe mpk wakanibeba kunipeleka home ndy kwenda kutolewa.

Nilitahiriwa week after hilo tukio mana walisema tushapata sababu nzuri ya kukukata.
 
Shuleni nilikua mkimya na mtulivu sana kiasi kwamba asilimia kubwa ya wanafunzi wenzangu walijua sisikii vizuri, kwasababu sikua na desturi ya kuongea hata kama ukiniuliza kitu labda tuwe tuna fahamiana

Basi bhana nikawa napendwa sana na mademu pamoja na walimu , nikawa natolewa mifano hadi pared kwa utulivu na kujipenda kwangu hususani na dalasan sikua vibaya Sana nikawa najipakualia minyama Tu.

Siku moja mwalimu wa fildi alikua anatoa somo class sasa mi nilikua nimekaa na manzi mmoja anaongea sauti ya chini huku pindi lina endelea , akaongea neno nika tabasamu ticha akaniona nakuniita mbele kwa ghadhabu huku akisema Mimi nafundisha wewe unanicheka shika chini hapo.

Hapo nika sita na kusema mwalimu mimi sija cheka umeniona nikitabasamu mwalimu akagoma na kuniforce niadhibiwe aloooh dalasa zima likainuka na kupinga Mimi kuazibiwa .
 

Uliona nini kule nyuma kaka[emoji3526][emoji3526]
 

Kweli we kikorofi[emoji23][emoji23]
 
Sasa nimeelewa kwanini unapenda matumizi ya fake ID, kumbe toka mtoto ulipenda kujificha πŸ˜‚
Yani izo ndo zangu za kujificha Sasa Kivumbi ule mchezo wa kuchezesha vikopo mara vichupa Tena sipend mtu aje niwe pekeyangu,moja had lilinikata mguuni Nina alama Hadi Leo nilishonwa mzee kagoma had akaona aache tuπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Kupika Sasa wee hunitoi, Mimi ndo mpishi mkuu sikumoja tukapika tukaenda kuiba malimao ya kachumbari mm ndo mpandaji juu acha nitobolewe na miba kwenye goti nililiavkimya kimya maana wenyew wangesikia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚nikapata kidonda kikubwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Haha pole mkuu[emoji28]
 

Manina wewe[emoji23][emoji23]
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Pole ulikuwa na heka heka nyingi kuliko umri umri wako. Hapo kwenye kupika itabidi ufanye namna nile pishi lako maana kwenye comment tu chakula n kitamu sijui uhalisia itakuwaje.
 
Umetisha mkuu,hiyo story yako ya primary ni kama mimi tu,nilikuwa mpole sana hata wachapwe darasa Zima mi nlikuwa sichapwi,nilikuwa napangiwa tu kufanya usafi ofisi za walimu.
Jina lako linasadifu uyasemayo na uhalisia wako, bado ni mpole au ndio ushafunguliwa dunia kuwa unachotaka?
 
Kipindi Cha utoto nilikuwa najiuliza jiko la mafuta linawashwa kwa juu ambazo ndo Kuna zile tambi zake Sasa kwanini tusiwashe kwa chini ambapo Kuna mafuta na tambi zilipoanzia labda Moto utapanda juu na kuendelea kuwaka Kama kawaida
Basi siku moja nikachukua kiberiti nikafungua lile bakuli lake ambako Kuna mafuta na tambi zake nikawasha kile kiberiti na kutumbukiza Kisha kufunika nikisubiri Moto uwake juu ya tambi lahaula tofauti na nilivyotegemea Moto ulishika Kasi jiko lote liliwaka na bado kidogo niunguze nyumba biLA ya msaada ya majirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…