Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,542
- 2,174
Shaka : IGP Simon Siro tupia jicho lako kwa baadhi ya askari wako wilayani Kahama na kwingineko | Wanabambika watu kesi kubwa na nzito na baadae kuwatoza faini tena bila risiti kamwe CCM hatutavumilia hili |
"Wananchi ninazo taarifa juu ya vitendo viovu vya kupambikwa kesi za kukamatwa na bangi na hata mauaji kwa vijana na wanawake vinavyofanywa na baadhi ya askari wetu wasio waaminifu wanaotaka kulitia doa jeshi letu la Polisi, hili halikubaliki"
"Kibaya zaidi wanapowafikisha watuhumiwa polisi, hawawapeleki hata mahakamani badala yake wanatozwa faini ambazo hazina hata stakabadhi yeyote, niwakikishie wananchi Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitavumilia jambo hili tunasimama upande wenu, kuweni na amani endeleni kutiii sheria bila shurti"
"Chama Cha Mapinduzi tutazungumza na IGP leo hii jicho lake liangalie wilaya ya Kahama haiwezekani wananchi wako kwenye nchi huru leo hii wakafanywa wanaishi kama wakimbizi kwa vitu vya kusingiziana na kubambikiziana kesi kubwa na nzito"
"Jumamosi tarehe 9 Oktoba, 2021 ili akashirikiane na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Wanaushetu mchaguenu Ndg Emmanuel Cherehani anatosha na amekidhi vigezo na viwango vya kuwa mbunge wenu wa 2021-2025"
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
#Ushetu-Kahama Kampeni CCM