Shaka Hamdu Shaka: CCM haitavumilia wananchi kubambikwa kesi

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
983
1,000

Shaka : IGP Simon Siro tupia jicho lako kwa baadhi ya askari wako wilayani Kahama na kwingineko | Wanabambika watu kesi kubwa na nzito na baadae kuwatoza faini tena bila risiti kamwe CCM hatutavumilia hili |​

"Wananchi ninazo taarifa juu ya vitendo viovu vya kupambikwa kesi za kukamatwa na bangi na hata mauaji kwa vijana na wanawake vinavyofanywa na baadhi ya askari wetu wasio waaminifu wanaotaka kulitia doa jeshi letu la Polisi, hili halikubaliki"

"Kibaya zaidi wanapowafikisha watuhumiwa polisi, hawawapeleki hata mahakamani badala yake wanatozwa faini ambazo hazina hata stakabadhi yeyote, niwakikishie wananchi Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitavumilia jambo hili tunasimama upande wenu, kuweni na amani endeleni kutiii sheria bila shurti"

"Chama Cha Mapinduzi tutazungumza na IGP leo hii jicho lake liangalie wilaya ya Kahama haiwezekani wananchi wako kwenye nchi huru leo hii wakafanywa wanaishi kama wakimbizi kwa vitu vya kusingiziana na kubambikiziana kesi kubwa na nzito"

"Jumamosi tarehe 9 Oktoba, 2021 ili akashirikiane na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Wanaushetu mchaguenu Ndg Emmanuel Cherehani anatosha na amekidhi vigezo na viwango vya kuwa mbunge wenu wa 2021-2025"

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi

#Ushetu-Kahama Kampeni CCM

IMG-20210927-WA0058.jpg
IMG-20210917-WA0069.jpg

IMG-20210916-WA0078.jpg
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
6,332
2,000
Kwa hiyo wenye kuvaa mavazi ya kijani pekee ndio hawastahili kubambikiwa kesi na polisi chini ya huyo muheshimiwa sana sio, vipi wale wanaotamani wayapate hayo mavazi ya kijani lakini tozo zime wanyonga, pamoja na na ukosefu wa haki zao za msingi kutokana na Hawa wanaowabambikia, hawa kwa umoja wetu tujiweke katika kundi lipi, au sisi mmetutenga rasmi, tunaomba majibu ili tufahamu.
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,441
2,000
Wananchi msidanganywe na Shaka!!Mwambieni waliompiga Lisu Risasi wako wapi??Haki itendeke!!!
 
Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
983
1,000
Kwa hiyo wenye kuvaa mavazi ya kijani pekee ndio hawastahili kubambikiwa kesi na polisi chini ya huyo muheshimiwa sana sio, vipi wale wanaotamani wayapate hayo mavazi ya kijani lakini tozo zime wanyonga, pamoja na na ukosefu wa haki zao za msingi kutokana na Hawa wanaowabambikia, hawa kwa umoja wetu tujiweke katika kundi lipi, au sisi mmetutenga rasmi, tunaomba majibu ili tufahamu.
Mkuu mbona Shaka ametetea wananchi wote,
Niwapi amesema makada wa CCM?

Nibaadhi ya askari sio wote
 
Almighty

JF-Expert Member
May 27, 2020
602
500
Huyu Mwamba Shaka anatisha sana kwa uzalendo alionao,

Tunataka viongozi kama hawa Tanzania.

Viongozi wasimame na wananchi wakati wote.

Hongera sana Shaka hii ndio CCM ya Mwl Nyerere.
 
VUGU-VUGU

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
582
1,000
Huyu bwana naona atarudisha heshima ya CCM Tanzania

Asiishie hapo hao polisi wakamatwe maramoja,

Hawa wanamchonganisha Rais na wananchi wakamatwee na wafukwe kabisa
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,228
2,000
Kuna kazi ngumu sana kufanywa, mojawapo ni hii aliyojipa Shaka, anawalaumu washirika wao kwa mateso wanayowatendea watanzania kwa manufaa ya chama chake, Shaka aache usanii, anajua chama chake hakipendwi asijivike kilemba feki cha uzalendo wengi wanabambikiwa kesi kwa manufaa ya CCM.
 
ABC ZA 2020

JF-Expert Member
May 2, 2018
635
500

Shaka : IGP Simon Siro tupia jicho lako kwa baadhi ya askari wako wilayani Kahama na kwingineko | Wanabambika watu kesi kubwa na nzito na baadae kuwatoza faini tena bila risiti kamwe CCM hatutavumilia hili |​

Chagueni Mhe Cherehani akamsaidie Rais Samia Suluhu,​

"Wananchi ninazo taarifa juu ya vitendo viovu vya kupambikwa kesi za kukamatwa na bangi na hata mauaji kwa vijana na wanawake vinavyofanywa na baadhi ya askari wetu wasio waaminifu wanaotaka kulitia doa jeshi letu la Polisi, hili halikubaliki"

"Kibaya zaidi wanapowafikisha watuhumiwa polisi, hawawapeleki hata mahakamani badala yake wanatozwa faini ambazo hazina hata stakabadhi yeyote, niwakikishie wananchi Serikali ya CCM inayongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitavumilia jambo hili tunasimama upande wenu, kuweni na amani endeleni kutiii sheria bila shurti"

"Chama Cha Mapinduzi tutazungumza na IGP leo hii jicho lake liangalie wilaya ya Kahama haiwezekani wananchi wako kwenye nchi huru leo hii wakafanywa wanaishi kama wakimbizi kwa vitu vya kusingiziana na kubambikiziana kesi kubwa na nzito"

"Jumamosi tarehe 9 Oktoba, 2021 ili akashirikiane na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Wanaushetu mchaguenu Ndg Emmanuel Cherehani anatosha na amekidhi vigezo na viwango vya kuwa mbunge wenu wa 2021-2025"

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi

#Ushetu-Kahama Kampeni CCM

View attachment 1968218

View attachment 1968219

View attachment 1968220

View attachment 1968223

View attachment 1968233
Chagua Cherehani Ushetu,
Machadema hayana hela
CCM ndio Chama
 
ABC ZA 2020

JF-Expert Member
May 2, 2018
635
500
Kuna kazi ngumu sana kufanywa, mojawapo ni hii aliyojipa Shaka, anawalaumu washirika wao kwa mateso wanayowatendea watanzania kwa manufaa ya chama chake, Shaka aache usanii, anajua chama chake hakipendwi asijivike kilemba feki cha uzalendo wengi wanabambikiwa kesi kwa manufaa ya CCM.
Unamaanisha CCM haitakiwi kuwa na wazalendo,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom