Stories of Change - 2021 Competition

Rachel Nzengo

Member
Jul 29, 2021
13
17
Salaam!
Utenzi huu unabeba dhima ya neno "Ukatili" ambalo limekuwa likitajwa sana, lakini watu wengi wameshindwa hasa kuelewa neno hilo lina maana gani. Shairi hili lipo katika mtindo wa masimulizi kuhusu matukio ya ukatili yanayotokea ndani ya familia, ambapo mabinti yatima mapacha waliokuwa wakiishi na baba yao mdogo walifanyiwa ukatili na kaka yao, lakini walishindwa kuaminiwa walipozungumza ukweli wa yale yanayowasibu. Lakini pia, limemwonesha mtoto aliyefanyiwa ukatili kwa muda wa miaka mitatu, toka akiwa na umri wa miaka minne, na Mjomba aliyeaminiwa nyumbani. Nini hatima ya watoto hawa? Tafadhali fuatilia mkasa huu wa kusisimua.


1. Hili neno ukatili, majira haya masikioni li mashughuli,

Kichwani twalihariri, bila hisia wala huzuni dalili,

Ni nani atutabiri, madhara chafu juu ya huu ufedhuli,

Wa kingono ukatili, paso huruma majumbani wakithiri,

Waathirika wajikabili, kuwaficha uozo wale walowakatili,

Walimwengu nijibuni, alaumiwe nani juu ya huu ukatili?


2. Kwa wamama na watoto, na ukatili watafunwa,

Limekuwa janga msoto, majumbani limechimba kina,

Wafanyao ni wa ndoto, ndugu wawaaminio sana,

Wamegeuka kiroboto, ndani ya nyumba kung’atana,

Tamaa mwili msokoto, zaongeza kasi ya hii laana,

Ukatili wa kingono, mekuwa siri familia, waota mbawa.


3. Aishi Kariakoo aitwa Mama Shabani, familia’ke ni ya dini sana.

Waishi kenda nyumbani, wamejinadhiri kwa adhana,

Watoto wane wa tumboni, Shabani wa kwanza kijana,

aishi kaka wa Ma’shashani, aitwa Mjomba apendwa sana,

Wawili pacha bintize Hassani, marehemu kakake Baba Shabani,

Aisha binti pekee wa tumboni, mama Hassani ampenda sana.


4.Furaha litaradi kwa hii familia, wazazi nao walihimiza dua,

Siku kenda na kenda zilivyozidia, furaha 'lianza suasua,

Aisha miyaka saba lipokaribia, dadaze pacha kumi miyaka 'lifikia,

Aisha Mjomba hamkufurahia, nao pacha Kaka Shabani walimkimbia,

Mjomba alibaki Nyumbani kusimamia, Kumlinda na Aisha pia,

Pacha Kusoma walikukimbilia, kaka Shabani mwalimu wao nyumbani.


5. Kila kuchwapo Shabani 'liongeza nia, kuwahadaa dadaze kuwa si athari,

Siku mpito alitengeneza njia, pepo ngono akashinda baradhuri,

Zamu za siku 'liwatengezea, Kurwa na Dotto kuwafanyia ukatili,

Maskini! Yatima wale akahawadaa, kukidhi tamaa ya wake mwili,

Akili, afya zikawaelemea, wakawa wake wa Shabani kwa siri,

Kijana shabani Dadaze aliwapenda, sasa pepo gani kamwingia?


6. Kabla majuma kadha hayajapita, Dotto hasira ilimwaka sana,

Kusoma kwa kaka alisita, niyake ayaseme maovu kwa mama,

Akiliye ilijaa vita, mamkubwa maneno yangu ataona yaso mana,

Baada ya swala hakusita, kwa mamaye chumbani alikazana,

Mama! Kaka Shabani ni Sheta..., Miili yetu undugu kaukana,

Mama Shabani alibekwa sana, Alibwata Dotto akae kimya abadani.


7. Mtoto kwangu nyumbani umeleta shari, kijanangu Shabani si wa ngono,

Kurwa, Dotto walikanywa kwa ukali, maneno najisi nyumbani yawe kikomo,

Kwa ba’ Shabani walifanya siri, Kurwa, Dotto nani awape somo,

Afya zao, mwili pia akili, saikolojia hasi ikawashusha kimasomo,

Nyumbani waligeuzwa jabari, la mabaya matendo yaso komo,

Lahaula! Binti hawa yatima, ni nani awatetee na huu ukatili?


8. Malipo yapo duniani, hawakudanya walopita wahenga,

Aisha bintiye pekee wa tumboni, mjomba akamfanya mlengwa,

Akamkatili kingono nyumbani, kwa siku kadha Aisha akajitenga,

Kwa ugonjwa bila afueni, hadi lipoenda hosptali kwa walengwa,

Mtoto Aisha aingiliwa mwilini, 'lisema daktari bila chenga,

Alipobanwa Aisha mtoto, 'lifunguka mjomba anifanyia toka miaka mi'ne.


8. Ma'Shabani hakika 'liombeleza, likauma upya tumbo la uzazi,

Ni nani wa kumpoteza, Shabani mjomba, au kizazi?

Shabani mjomba alimfukuza, akapanga kumwangamiza kwa kisasi,

Ma’ Shabani mume hakumjuza, jinamizi ukatili alifanyie kazi,

Binti watatu walipooza, walipoambiwa dini hairuhusu maasi,

Wakaonywa wakae kimya, ni dhambi kuongelea tusi ngono.


9. Kurwa Kumbe ana mtoto tumboni, akiwa la saba mimba ya Shabani,

Lipojulikana lifukuzwa nyumbani, eti nenda kazae ewe hayawani,

Aliondoka Kurwa nyumbani, na mtoto wa Shabani tumboni,

Akawa kioja mitaani, akakosa hata tonge kuweka tumboni,

Siku ya uzazi yu jaani, Kurwa atafuta nini aweke tumboni,

Uchungu lipomzidia, 'likuwa na njaa akapoteza fahamu.


10. Lipopita Wasamaria, jicho liliona jaani kuna binadamu,

Limwokota kwa hisia, hospitali kumpeleka kwa watalamu,

Daktari 'liulizia, huyu binti nani wakowapi wanomfahamu,

Lipokosa wakumjibia, Kurwa 'lisahauliwa leba ka' sanamu,

Siku mbili ziliishia, kuna binti yu mochwari, 'lisema nesi wa zamu,

Masikini! Kurwa hatunaye tena, alaaumiwe nani na huu ukatili?


11. Walimwengu nauliza tena, nani wa kulaumiwa na huu unyama,

Taifa kesho nani alitafuna? Nijibuni basi, au swali langu halina mana?

Hayo tusemayo eti laana, ndiyo haya twafanya paso moyo huruma,

Twawapoteza taifa kesho teule, eti siri familia, waja wataniona sina mana,

Natamati kwa moyo bubujiko, nikisubiri kujibiwa swali neno 'ukatili,’

Mkinijibu ni nani alaaumiwe, dunia nzima tutasimama kuanza nae.


----------------------------------------------------------------------


Matukio haya yamekuwa yakijitokeza ndani ya familia, lakini wanafamilia hushindwa kuwa na utayari wa kuzungumzia ukweli wa janga hilo, mbali na kudhibiti pamoja na kutoa msaada kwa wahanga.
Tafadhali, NAOMBA KURA YAKO ili kwa pamoja tupaze sauti kukabiliana na janga hili, "Ukatili wa Kijinsia"
 
Makatili tupo..?
Makatili hoyeee..🤣🤣
Lazima tumjibu huyu..

UKatili twajivunia,kwa kweli tumeweka nia!
Abadani twafurahia,kama pepo katuingia!.
Katili hoyeee..

Jera twajijazia,Sera twazipandilia!
Maafisa twawahonga,sheria kuiponda!
Katili hoyeee..

Raha twajipa sie,kuzini kutamu nyie!
Wa mjomba anitaka,na nyuma anaparakacha
Naanzaje kukacha,na kibubu hakijachacha..??
Katili hoyeee...

Mimba twawajaza sie, viherehere kwanini mlie..?
Ukatili wangu mie,vigagula kwanini mlie..?
Shubiri yangu mie,tamu yangu acheni nijilie😂
Katili hoyeee..
 
Hili neno ukatili, maana zipo yakini
si moja wala si mbili, zaweza jaa kapuni
Unyanyasaji kimwili, mchana au gizani
Nao pia ukatili, afanyae firauni

Sio tu kwa kabali, au kwa visu shingoni
Ngumi mia au mbili, ama teke za mbavuni
Na zile mila batili, na ndoa za utotoni
Nao pia ukatili, afanyae firauni

Nilikuwa tu napasha, kujifanya mshairi
Nakusanya kabrasha, shaishiwa mistari
Ya mwisho nawakumbusha, ngono isiyo hiari,
Nao pia ukatili, afanyae firauni.
 
Back
Top Bottom