Shabiby line tuoneeni huruma abiria....!!!

Shabiby line tuoneeni huruma abiria....!!!

Kuna siku niko kwenye dar express tukapelekwa pale mombo. Binafsi safarini nakula vyakula vikavu tu (nyama choma, chips au ndizi za kukaanga) nje ya hapo ni bites tu.

Nikawa na mzungu flani klwa rangi ya ngozi yake ) kwenye seat ya pembeni. Kufika pale jamaa akanunua wali maharage, wakamjazia na kisanvu mchuzi mwingi, akachukua na sharubati ya parachichi (imewekewa kwenye chupa ya maji) Akaja kula ndani ya gari daaah siku ile ndio niligundua kuna watu wana roho ngumu.
Alifika kweli?? Maana huo mchanganyiko kama sio ngozi ngumu yetu hautoboi...au mzungu pori huyo..
 
Dodoma umeondoka saa sita,amuda wa chakula cha mchana unafika upo morogoro, mbona rahisi tu? halafu, kama wewe huli, usifikiri na wenzako hawali, maisha yako sio ya wengine, unaposafiri sio kwamba unatakiwa ujiteseee, usileeee ili uonekane umesafiri, unaweza kuinjoy mambo mbalimbali kama vile misosi misafi pia. nyie watu mmekuja mjini juzi ninyi mnasumbua sana.
Niko mjini kabla huzaliwa pimbi wee. Njoo Ubungo Kibo utanikuta
 
Hana hela ya kutumia private jet muda wote. Hajui kuwa hata atcl,emirates na wenzie ni public transport.
Hahaha hapo itakuwa ndugu yetu alijisahau kidogo au labda safari zake ni barabarani tu hatuwezi jua, ila kwa mtu ambaye safari zake anamix na angani na majini wengi ni ngumu kukwepa public transport kwa miaka yote hiyo, wachache wanaomudu private mara kwa mara
 
wao kama ni madereva, wanakuwa na kamisheni kwanza ya chakula bure na pili ya pesa. sasa mwenye mabasi sijui kama analijua hilo. kiukweli inakera mno mno. unaweza kusafiri na mtoto mimi naweza nisile ila mtoto unatamani umnunulie kitu cha kutafuna hata kama kidogo, shida sasa unaogopa mtoto asije kuugua tumbo. watu wamejazana kama mtaa wa congo, choo haipo mbali, watu wote wanaotoka chooni na mimaji waliyokanyaga kule chooni wanapita na kukanyaga karibu na vyakula, watu wenyewe wa morogoro wanatawadhaga bila kunawa na sabuni hao.
Usimamizi nao mbovu, Hizi Hotel za njiani wanazouza vyakula karibu kabisa na vyoo vya abiria ni kwa sababu ya kutowajibika tu kwa idara za afya.
 
I think ndio wametuleta hapa Leo. Kwa nje si kuna kina mama kibao wanauza ndizi na machungwa? Imebidi ninunue tu ndizi kisukari za buku mbili na maji ya kunywa. Imagine ka robo kuku elfu sita, kuku mwenyewe si kuku sijui njiwa
Hapa Mahali magari mengi yanapapenda ila ni pabovu sana, nafikiri ni sehemu pia huwa wanapata abiria wengi wa kupakia na kusafiri
 
Hapo mahali pabovu Moro mabasi huwa yanapata abiria wa kupakia pia wakati nyie mnataseka huko kwa hizo dakika 15 wao wanaendelea kujaza mapengo katika bus.
hebu imagine, mabasi yanasimama pale morogoro msamvu sio chini ya 10 kwa wakati mmoja hadi watu huwa wanachanganya mabasi, yakiondoka mengine yamefika asubuhi hadi jioni, pako overcrowded mno, na pamebanana na vyoo hapohapo, vyakula havipo mbali na choo, nnzi akitoka chooni hata hahangaiki kwenda mbali kugusa msosi. afu mtu chakula cha buku mia tano anakuuzia 8000. soda pale ni 2000 na sidhani kama wanatoa kodi, manake huwa hawatoi risiti ya EFD unakula tu kwa coupon yao ile, kweli mtu aniuzie soda ya 1000 kwa 2000 na asinipe risidi ya efd? serikali ichunguze pale ama la na TRA nao wana mgao wao pale pamoja na madereva. TRA Mpo wapi? hela kiasi gani inaingizwa pale kichafuchafu tu au na yule mmemkadiria kama ni mama ntilie? analipa kodi? anatoa risiti manake ile biashara yake sio ndogo, ile inaingiza si chini ya 400m kwa mwaka anastahili atoe risiti kama kwenye migahawa mikubwa tu.

kuna siku nilienda Dodoma pale kati kuna mgahawa wa Chef Asil na Mwambao, pana jaa na pasafi sana, wanakuletea risiti ya EFD kabisa tena kwa chakula hata kama ni cha 6000 au 7000. hapo morogoro tunatozwa 8000 hadi 10,000 na hakuna EFD receipt.
 
Tatizo wabongo pia tunapenda sana kupoteza muda na kulakula hovyo. Safari ya Dodoma ilipaswa iwe kushusha tu abiria na kupakia na sio kusimama kula. Hata safari ya Arusha ilipaswa kuwa hivyo. Angalau Dar - Mwanza, Dar - Sumbawanga, Dar - Kigoma, Dar - Songea, Dar - Bukoba ndo kuna ulazima wa watu kusimama kula.
Unajua kwenye hizo safari kuna watoto, kuna watu wanatumia dawa na kuna wengine wameanza safari hata chai hawajanywa??
 
Back
Top Bottom