Serikali yawaonya Walimu wanaoendelea na adhabu ya viboko shuleni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Serikali imeendelea kuzuia matumizi ya viboko katika ufundishaji wanafunzi na badala yake walimu wametakiwa kutafuta mbinu mbadala za ufundishaji ili wanafunzi wawaelewe.

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 16, katika mkutano wa mradi wa kuboresha mafunzo kwa walimu katika vyuo vya ualimu (TESP), Kamishna wa elimu nchini, Lyabwene Mutahabwa, amesema viboko sio suluhusho la uelewa kwa wanafunzi.

"Licha ya serikali kulikemea hili mara kwa mara bado kumekuwepo na baadhi ya walimu wanaondeleza ufundishaji wa matumizi ya kiboko kama sehemu ya kumuadhibisha mwanafunzi kuelewa na hii ni kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo.

"Utakuta mwanafunzi akikosa hesabu moja kiboko kimoja, akikosa hesabu mbili viboko viwili na wakati mwingine kutolewa lugha za vitisho, hii sio sahihi na ni moja ya mambo yanayozidi kuharibu elimu ya Tanzania," amesema Kamishna huyo.

Akizungumzia kuhusu mradi wa TESP, Mutahabwa amesema ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kwenda hadi mwaka 2025 ambapo katika.

Aidha katika mkutano huo wa leo, amesema wanaangalia walipotoka, walipo na kuweka mikakati kuendelea nao na hata pale utakapofika mwisho wa utekelezaji wake.

Amesema pamoja na mambo mengine, mradi umelenga kuwabadilisha walimu kifikra katika njia za ufundishaji ikiwemo matumizi ya teknolojia ili kuendana na wakati wa sasa.

"Maendeleo ya kweli katika nchi ni matokeo ya elimu bora na elimu bora na ni matokeo ya kuwa na walimu bora na mwalimu bora huwa na upendo kwa wanafunzi.

“Kupitia mradi huu tunaamini mwalimu atakuwa akikimbiliwa na wanafunzi kutaka awafundishe," amesema Kamishna huyo.

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo, Cosmas Mahenge, amesema katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya Canada kwa dola 53 milioni umefanya mambo mengi ikiwa pamoja na utoaji wa mafunzo.

Ametaja manufaa mengine ambayo ni pamoja na ujenzi wa maabara na maktaba, ugawaji wa vifaa vya Tehama katika vyuo vyote 35 vya ualimu zikiwemo projekta kompyita na mashine za kudurufu na utoaji wa mafunzo ambapo tayari wakufunzi 5,909 wameshafikiwa.

Naye Mwenyekiti wa vyuo vya walimu Tanzania Bara, Agustine Sahili amesema mafunzo hayo yamekuwa na faida kwao kwani yatasaidia katika kuboresha elimu ya Tanzania.

Pia amesema katika utekelezaji wa mradi huo wameweza kufundishwa mbinu mbalimbali za kiuongozi zikiwemo bodi za shule katika kutafuta fedha za kujiendesha.

MWANANCHI
 
Kamishna wa elimu mvivu wa kufikiri kwa kiwango hichi ataisogeza elimu kweli ? Anajua walimu wanapenda kuchapa voboko wanafunzi au wanalazimika kufanya ivo ili kujenga nidhamu ya hao watoto
 
Back
Top Bottom