Serikali yatoa vipaumbele vyake kwa wananchi

Serikali yatoa vipaumbele vyake kwa wananchi

Kiuhalisia hilo deni ni magumashi tupu tulikopeshwa kwa masharti makali mno
-lazima lipitie bank zao
-lazima tutumie wataalam wao kwenye chochote
-lazima tutumie firm zenye link na wao kuanzia usafiri mpaka logistics za upangaji nyumba nk
Mwisho wa siku deni limewafaidisha wao, kwa kutoa ajira na biashara kwenye makampuni yao na jamaa zao

Wacha uongo.
 
Inawezekana kabisa ndani ya miaka mitatu kwa kuongeza zaidi kubana matumizi.
Magufuli atafuta kabisa utegemezi wa wafadhili kwenye bajeti ndani ya mwaka mmoja


Kitu cha muhimu hapa ni kujua chanzo cha deni hili kubwa mno ambalo tunalipa; inawezekana kabisa tunalipa madeni kwa wahuni waloshirikiana na utawala dharimu kutuibia kwa mtindo wa kutupa madenia hewa!! Rais Magufuli ana kila sababu sio tu kuhakikisha kuwa nchi inakuwa sio tegemezi bali kujua hayo madeni tunayolipa yalitokana na nini na kama kuna justification ya kuyalipa!!

Kuna baadhi ya wananchi wazalendo ambao wanaamini kuwa Magufuli hana budi kufanya forensic audit ya madeni haya ili kubaini uhalali wake na pia kuhakikisha kuwa TREASURY inalipa madeni yale tu ambayo yanastahili kulipwa kwani katika ulipaji madeni ya nje kuna kilasababu za kuamini kuwa ubadhilifu mkubwa unaweza kufanyika kule!!
 
Wacha uongo

Usitegemee kawa huyu SHORI atachangia kitu cha maana hapa kwani anajua kuwa baba yao DHAIFU ana kesi ya kujibu kuhusiana na MIKOPO YA KIGUMASHI aliyoiingizia nchi na kulikuza deni a Taifa wakati wa utawala wake!! Tukianzia na lile deni la ATCL tunalomlipa mlebanoni kwa ndege ya AIRBUS ambayo haikufanya kazi lakini TREASURY kwa amri ya DHAIFU walikuwa wanamlipa!!
 
jf kuna vituko sana. Ni vidole kwenda mbele. Halaf mqwereh yeye aliona sifa sn kutangazia umma alienda kupimwa na kutibiwa TD waswahili bana. Yani alikuwa radhi kupimwa TD na mzungu kuliko madokta wakibongo.

Na sasa tunamlipia madeni matriolioni kwa ajili yake
Mkuu vipimo vya aina hio vipo vingi sana sio Tezi Dume tuu! Hujafa hujaumbika...... Hospitali kuna Plain X-ray nyingi tuu watu wanafanyiwa kwa njia hio, pia kuna Ultrasound za kuingiza transducer huko na kufanyiwa kipimo no matter ni mwanaume au mwanamke

Vipimo vya aina hio ni vya kawaida sana na wazungu huwa hawashangai sababu ni kawaida wao vinafanyika sana! Kutokana na tamaduni zetu tunaona kitu cha ajabu sanaaa ndo maana mkwere akaamua kwenda nje lakini kiuhalisia hospital ni kipimo cha kawaida sanaaa file la mgonjwa lisingekuwa ni confidential nadhani ungeona sana! So usimponde wala kumshangaa leo kwake kesho kwako
 
Tutamaliza tu taratibu...hata Marekani wanadaiwa sana na hawalipi kwa kishindo kama sisi.

Kufananisha athari za deni kubwa la Taifa la chi yetu na deni la chi kama marekani ni kuonesha kutoelewa madhara yanayoweza kuletwa na ukubwa wa deni hilo kwa nchi tegemezi!! Maraekani leo wakitaka kulipa deni lao la taifa wanaweza kufanya hivyo kwani watachapisha dollar zoo na kulipa ;lakini nchi kama Tanzania ni lazima iwe na fedha za kigeni ikiwa ni dollars au pounds ndio iweze kulipa!! Ikishindwa kulipa deni maana yake haitaweza kufanya biashara na mataifa mengine!!!

Matatizo ya nchi kushindwa kulipa deni lake ndio kama yale yaliyoyakumba nchi ya Greece kwa uchumi wake kuyumba kwani nchi inakuwa haina hadhi ya kukopesheka na kufanya biashara na nchi za nje ambacho ndio chanzo kikubwa cha forex!! Kulipa madeni ya nje yaliyolimbikizwa kunapunguza uwezo wa nchi kutumia rasilimali zake kukuza uchumi wake na hasa pale mikopo/madeni hayakutumika kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma katika uchumi wa nchi!!
 
More like we are going to bail out these thieves who brought us in this mess in the first place. I say investigate all the loans on how they were spent by the previous administration before we pay them back.
It's useless to investigate it simply because it's a loan already we have nothing to do with it.
 
Hizo barabara za lami unazokanyaga (utasema fake) hukulipa kodi ya kuzijenga, ndio madeni yenyewe. Na hayo mabilioni yaliyofichwa Uswiss na baba zako ni kati ya fedha za mikopo! Kopa ulipe, vumilia maumivu

Badala ya kujivunia matumizi ya ovyo ya fedha zetu za kodi, walipaswa waone haya. Kwa binadamu makini alitakiwa afahamu hizo fedha tunazihitaji kufanya mendeleo ambayo yamekwama kwa miaka vizazi kwa visingizio vya serikali ya ccm kuwa haina uwezo wakti kila siku inakopa madeni.

Kabla ya kujifunika uso na kwingine kuko wazi, tunahitaji kwanza watupe mchanganuo wa deni lote lile na zile fedha zote zimetumika je.

Ukiona viongozi wanashangilia ulipaji madeni ya hovyo badala ya kusikitika, ujue taifa linaongozwa kwa laana.
 
Ulitaka alipe sh ngapi, au ulitaka asilipe ili mwisho iwe nini?
true that
mimi huwa nahisi rahisi hana washauri,...
kulipa bil784 ni sawa na ngwenjela2
hiyo pesa angejaribu kuitia kwenye viwanda hata wkaanza na hiyo kwanza japo ndogo ili watu wakija kupata ajila deni litajilipa
ila magu hana washauri
 
It's useless to investigate it simply because it's a loan already we have nothing to do with it.

Perfect comment.....kutaka investigation ya deni la taifa ni kuleta siasa kwenye kazi na kupoteza muda na kusababisha kushindwa ku-focus kwenye matatizo ya wananchi
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kulipa deni hilo la taifa ambalo ni zaidi ya billion 30 USD=zaidi ya trillion 48 za Tshs.

Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.

Sasa wadau ktk trillion 48 tunazodaiwa je kwa kuanza na kias hicho cha billion 784.3,..
tutamaliza deni?

Maana ni kiasi kidogo sana cha fedha na pia deni linazidi kukua kila sekunde.

Naleta hoja...

==========================

Serikali imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016, kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa mishahara ya watumishi wa Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.

Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.

Aliongeza kuwa katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi nchini , Serikali imetoa Sh. Bilioni 130 kwa mwezi Januari mwaka 2016 ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 ilitoa Sh. Bilioni 193.

Kwa upande wa Mfuko wa Barabara, Katibu Likwelile alifafanua mradi huo umetengewa kiasi cha Sh. Bilioni 47.89 na kuongeza kuwa Benki kuu ina fungu la mfuko huo ambapo nayo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 76.3.

Dkt. Likwelile alisema kuwa Halmashauri zitapelekewa kiasi cha Sh. Bilioni 20.52 kwa ajili ya kuboresha barabara na jumla mfuko huo kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 274.71.

Akifafanua kuhusu miradi ya umeme, Dkt. Likwelile alisema kuwa mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ililipa deni la TANESCO kiasi cha Sh. Bilioni 80 za mradi wa Kinyerezi II na kwa mwezi Januari mwaka 2016 kiasi cha Sh. Bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.

Hali hii imefikisha kiasi cha Sh. Bilioni 120 kwa ajili ya kulipa madeni na kuendeleza uzalishaji wa umeme nchini.

Alisema kiasi cha Sh. Bilioni 21.959 kimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ina mfuko wa mradi huo ambao kwa sasa una kiasi cha Sh. Bilioni 21.9 na kuongeza kuwa huduma ya umeme kwa wananchi itaimarika.

Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mpaka sasa mfuko huo una jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 46.3.

Aidha, BoT imetoa Sh. Bilioni 12.5 kuendeleza miradi ya maji ambapo kwa Januari mwaka 2016 Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 7.7.

Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 82.2 kwa mwezi wa Januari ili kuweza kulipa pensheni za wastaafu, na kwa wale wastaafu walio katika daftari la kudumu ambapo wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 33.3 kwa ajili ya malipo yao.

Wabunge wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya mkopo wa magari ambapo kila mbunge atapata kiasi cha Sh. Milioni 90, kiasi cha Sh. Milioni. 45 ni ruzuku na Sh. Mil. 45 ni mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 5.

Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.

Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alibainisha kuwa hali ya makusanyo ya mapato nchini iko vizuri ambapo kwa mwezi Januari 2016, makadirio yalikuwa Sh. Trilioni 1 na Bilioni 45 na hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. Trilioni 1 na Bilioni 31 zimeshakusanywa.

Matarajio ya TRA ni kukamilisha kukusanya kiasi cha Sh. Billioni 14 zilizosalia.

Aidha, Kidata alibainisha kuwa uingizaji wa bidhaa kupitia bandarini bado uko vizuri licha ya minong’ono kuwa uzuiaji wa mianya ya ukwepaji kodi imepunguza uingizaji bidhaa ambapo kwa mwezi Januari Bilioni 111 zimekusanywa kutokana na ushuru wa forodha.

Kidata alitoa wito kwa kila mtanzania kulipa kodi na kutoa taarifa za wakwepa kodi ili kuweza kukuza mapato ya nchi.

Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu amepongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.

Alisema kuwa uchumi umekua na unazidi kuimarika licha ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo uchumi wa nchi umekua kwa asilimia 7 na unategemewa kukua miezi ijayo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.

Mfumuko wa bei unaendelea kubaki ndani ya kiwango cha tarakimu moja, licha ya ongezeko dogo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.

Alisema kuwa mfumuko wa bei ulikuwa asilimi 6.8 mwaka 2015, ukilinganishwa na asilimia 6.1 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2015.

Wakati huo huo mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati uliendelea kubaki katika viwango vya chini ya asilimia 2.5 kutokana na hatua mbalimbali za kisera zilizochukuliwa na BoT.

Prof. Ndulu alifafanua mapato ya fedha za kigeni yanaendelea vizuri ingawa bei ya dhahabu imeshuka kutoka Bilioni 2.5 hadi Bilioni1.3.
Sekta ya utalii imesaidia kuimarisha fedha za kigeni kwani mapato yameongezeka kutoka Bilioni 1.5 hadi Bilioni 2.2.

Sekta ya viwanda nayo imeshika nafasi ya pili katika kuongeza fedha za kigeni nchini ambapo mwaka 2015 mapato yalikuwa Bilioni 1 na kwa sasa yamefikia Bilioni1.5.

Aidha, Prof. Ndulu aliongeza kuwa sekta ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi imesaidia kuimarisha fedha za kigeni ambapo mapato yamefikia Dola Bilioni11 kwa mwaka.

Hadi kufikia sasa Tanzania imenufaika kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika uingizaji bidhaa hiyo kwa asilimia 44.

Serikali inatarajia kuendelea kuimarisha uchumi ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.

Imetolewa na Wizara ya Fedha na Mipango
Kitengo cha Mawasiliano
madai ya walimu vip da jasho la mnyonge huliwa na mwenye nguvi ualimu! ualimu!
 
Hizo barabara za lami unazokanyaga (utasema fake) hukulipa kodi ya kuzijenga, ndio madeni yenyewe. Na hayo mabilioni yaliyofichwa Uswiss na baba zako ni kati ya fedha za mikopo! Kopa ulipe, vumilia maumivu

What a rotten feces stuffed and stinking pumpkin on top of a neck!
 
Sasa ulitaka wafanyaje? Some few years/months back there was practically nothing set aside for serving the national debt. Waziri wa fedha SAADA MKUYA akiulizwa juu ya deni la Taifa jibu lake lilikuwa very political- kwamba deni hili stamilivu.... wakati kila siku deni lilikuwa linapanda. This is a big step ahead, kwanza kutambua kuwa unadaiwa na kuanza kutenga fedha kwa ajili ya kulipa. Hata watu binafsi au makampuni yanayokopa fedha hayalipi kwa wakati mmoja... kuna payment schedule
 
Sasa ulitaka wafanyaje? Some few years/months back there was practically nothing set aside for serving the national debt. Waziri wa fedha SAADA MKUYA akiulizwa juu ya deni la Taifa jibu lake lilikuwa very political- kwamba deni hili stamilivu.... wakati kila siku deni lilikuwa linapanda. This is a big step ahead, kwanza kutambua kuwa unadaiwa na kuanza kutenga fedha kwa ajili ya kulipa. Hata watu binafsi au makampuni yanayokopa fedha hayalipi kwa wakati mmoja... kuna payment schedule
 
Kumbuka deni lina schedule of payment na madeni ya serikali mengi ni muda mrefu sasa kiasi ukikilinganisha kiasi gani kilipaswa kulipwa kwa mwezi utakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuona uwezo wa serikali kulipa. Sema waandishi wetu ni makasuku wakiitwa ktk conference hawaulizi maswali ya maana na wakiuliza hawayapi headlines.
magazeti ya uhuru mkuu
 
Back
Top Bottom