Calender
Senior Member
- Dec 28, 2015
- 112
- 84
Kwa hiyo Improve kuwa TUNALIPA KODI, Na wanaLIPA KODI na tutalipa KODI.... Hivyo kodi zote zinalipwa !!!Kukuza uchumi ni wajibu wa kila mwananchi wote tuseme Ameen
!Savimbi jr
Kwa hiyo Improve kuwa TUNALIPA KODI, Na wanaLIPA KODI na tutalipa KODI.... Hivyo kodi zote zinalipwa !!!Kukuza uchumi ni wajibu wa kila mwananchi wote tuseme Ameen
Kodi zote zinalipwa yes, serikali inapunguza matumizi ikiwemo na bungeni majipu yanatumbuliwa na wananchi kwa pamoja wanaamua kuwa wazalendoKwa hiyo Improve kuwa TUNALIPA KODI, Na wanaLIPA KODI na tutalipa KODI.... Hivyo kodi zote zinalipwa !!!
!Savimbi jr
Hivyo vyema.. sasa hakuna uhasama tena...Tuwe macho zisije bebwa na wajanja!!!Kodi zote zinalipwa yes, serikali inapunguza matumizi ikiwemo na bungeni majipu yanatumbuliwa na wananchi kwa pamoja wanaamua kuwa wazalendo
Hilo deni ni pamoja na deni la ndani? Katika wadau wanaopaswa kuangaliwa ni hawa wazabuni na wakandarasi wa ndani, wanafanya kazi kwa mikopo kutoka katika mabenki, serikali haiwalipi kwa wakati mwisho wa siku wanaingia katika migogoro mikubwa sana na taasisi za fedha na hata kufilisiwa mali zao
Namaanisha kua kutakua na udhibiti wa hali ya juuLabda GESI tu ndio bado haijaanza kuuzwa lkn Madini na Mali asili mbona iko miaka yote na bado hakieleweki au unamaanisha nini kusema hivyo
Mimi sio mchumi
ila kwa ujuz mdogo,,,..
kubadilisha mkataba ningumu sana kwasababu inabidi kuvunja mkataba
na kuvunja mkataba ni gharama sana tena kwa hasa kwa makampuni ya kimataifa ni inshu coz jamaa
wapo na pesa ndefu so wanaweza kudeal na shria effectively ukaja kulipa deni kubwa mnoo na nchi ikapata hasara kubwa sana
na kumbuka mikatba mibovu nchi hii ni kila sector mfano Sector ya madini,gas,Ticks ndani ya bandari, etc
so ishu ni kwenye kuvunja mkataba cost kubwa ndo ishu nchi kma nchi ijipange,..
nahii ndo sababu ya serikali mikataba ambayo ni haki ya wananchi kuijua serikali inafanya siri it means madini na resources
mi kwanza sipendi kwa mikopo at,..
nchi yetu inajiweza sana sector zote zikisimamiwa vizur ktk
kukusanya kodi
kaka ila ktk mikataba ya nchi hiko kipengele lazima kiwepoKwanini kwenye mikataba yao hawakuweka kipengele cha kuruhusu kuvunja mikataba pindi ikibainika ubadhilifu au kuna mapungufu ???
haha ila kma jpm yupo serious anaweza kutumia mikopo vizr kuanzisha viwanda vyetu akasaidia uchumi kukuaaaMkuu evansGREATDeal, Kukopa kupo na kunaruhusiwa na Sio Dhambi, Tatizo linakujaga ni wakati wa kulipa Deni.
"Kukopa Harusi, ila kulipa ni Matanga".
kaka ila ktk mikataba ya nchi hiko kipengele lazima kiwepo
kwa maslahi ya wananchi,...
ila kwetu sidhaniiii coz mikataba yetu ipo kisiasa zaidi yaani ni siri kati ya viongoz na wanaowekeana contracts mkuu,.
nahii ni kwasababu ya kulinda 10%
haha ila kma jpm yupo serious anaweza kutumia mikopo vizr kuanzisha viwanda vyetu akasaidia uchumi kukuaaa
ila sijaona kipya kuashiria uwepo wa viwandaMkuu evansGREATDeal, Viwanda ni Moja ya Ahadi zake (Rais Magufuli), So lets See and Hope and Pray for Good.
hapa misingi imejengwa na vasco msoga,...Mkuu evansGREATDeal Kuna Jipu la kutumbua hapo basi.
ila sijaona kipya kuashiria uwepo wa viwanda
hapa misingi imejengwa na vasco msoga,...
na unakuta mikataba yote iliyosainiwa wakat ye rais ana10%
uzur ndo kwanza mwanzoDuuuu, Basi ni Sheeedaaa, Tatizo letu SIASA kila mahali, SIASA mpaka kwa Watendaji.
Hapa basi inahitaji zaidi ya Ujasiri wa kutumbua Majipu, maana unamtumbua Mtu unayemjua.
Acha na Movie iendelee.
Siamini katika hilo ndg yangu labda kama tunataka kujifurahisha tuNamaanisha kua kutakua na udhibiti wa hali ya juu
uongoz system zilezileSiamini katika hilo ndg yangu labda kama tunataka kujifurahisha tu
Kumbuka deni lina schedule of payment na madeni ya serikali mengi ni muda mrefu sasa kiasi ukikilinganisha kiasi gani kilipaswa kulipwa kwa mwezi utakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuona uwezo wa serikali kulipa. Sema waandishi wetu ni makasuku wakiitwa ktk conference hawaulizi maswali ya maana na wakiuliza hawayapi headlines.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kulipa deni hilo la taifa ambalo ni zaidi ya billion 30 USD=zaidi ya trillion 48 za Tshs.
Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.
Sasa wadau ktk trillion 48 tunazodaiwa je kwa kuanza na kias hicho cha billion 784.3,..
tutamaliza deni?
Maana ni kiasi kidogo sana cha fedha na pia deni linazidi kukua kila sekunde.
Naleta hoja...
==========================
Serikali imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016, kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa mishahara ya watumishi wa Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.
Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.
Aliongeza kuwa katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi nchini , Serikali imetoa Sh. Bilioni 130 kwa mwezi Januari mwaka 2016 ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 ilitoa Sh. Bilioni 193.
Kwa upande wa Mfuko wa Barabara, Katibu Likwelile alifafanua mradi huo umetengewa kiasi cha Sh. Bilioni 47.89 na kuongeza kuwa Benki kuu ina fungu la mfuko huo ambapo nayo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 76.3.
Dkt. Likwelile alisema kuwa Halmashauri zitapelekewa kiasi cha Sh. Bilioni 20.52 kwa ajili ya kuboresha barabara na jumla mfuko huo kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 274.71.
Akifafanua kuhusu miradi ya umeme, Dkt. Likwelile alisema kuwa mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ililipa deni la TANESCO kiasi cha Sh. Bilioni 80 za mradi wa Kinyerezi II na kwa mwezi Januari mwaka 2016 kiasi cha Sh. Bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.
Hali hii imefikisha kiasi cha Sh. Bilioni 120 kwa ajili ya kulipa madeni na kuendeleza uzalishaji wa umeme nchini.
Alisema kiasi cha Sh. Bilioni 21.959 kimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ina mfuko wa mradi huo ambao kwa sasa una kiasi cha Sh. Bilioni 21.9 na kuongeza kuwa huduma ya umeme kwa wananchi itaimarika.
Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mpaka sasa mfuko huo una jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 46.3.
Aidha, BoT imetoa Sh. Bilioni 12.5 kuendeleza miradi ya maji ambapo kwa Januari mwaka 2016 Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 7.7.
Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 82.2 kwa mwezi wa Januari ili kuweza kulipa pensheni za wastaafu, na kwa wale wastaafu walio katika daftari la kudumu ambapo wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 33.3 kwa ajili ya malipo yao.
Wabunge wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya mkopo wa magari ambapo kila mbunge atapata kiasi cha Sh. Milioni 90, kiasi cha Sh. Milioni. 45 ni ruzuku na Sh. Mil. 45 ni mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 5.
Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.
Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alibainisha kuwa hali ya makusanyo ya mapato nchini iko vizuri ambapo kwa mwezi Januari 2016, makadirio yalikuwa Sh. Trilioni 1 na Bilioni 45 na hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. Trilioni 1 na Bilioni 31 zimeshakusanywa.
Matarajio ya TRA ni kukamilisha kukusanya kiasi cha Sh. Billioni 14 zilizosalia.
Aidha, Kidata alibainisha kuwa uingizaji wa bidhaa kupitia bandarini bado uko vizuri licha ya minong’ono kuwa uzuiaji wa mianya ya ukwepaji kodi imepunguza uingizaji bidhaa ambapo kwa mwezi Januari Bilioni 111 zimekusanywa kutokana na ushuru wa forodha.
Kidata alitoa wito kwa kila mtanzania kulipa kodi na kutoa taarifa za wakwepa kodi ili kuweza kukuza mapato ya nchi.
Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu amepongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.
Alisema kuwa uchumi umekua na unazidi kuimarika licha ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo uchumi wa nchi umekua kwa asilimia 7 na unategemewa kukua miezi ijayo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.
Mfumuko wa bei unaendelea kubaki ndani ya kiwango cha tarakimu moja, licha ya ongezeko dogo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.
Alisema kuwa mfumuko wa bei ulikuwa asilimi 6.8 mwaka 2015, ukilinganishwa na asilimia 6.1 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2015.
Wakati huo huo mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati uliendelea kubaki katika viwango vya chini ya asilimia 2.5 kutokana na hatua mbalimbali za kisera zilizochukuliwa na BoT.
Prof. Ndulu alifafanua mapato ya fedha za kigeni yanaendelea vizuri ingawa bei ya dhahabu imeshuka kutoka Bilioni 2.5 hadi Bilioni1.3.
Sekta ya utalii imesaidia kuimarisha fedha za kigeni kwani mapato yameongezeka kutoka Bilioni 1.5 hadi Bilioni 2.2.
Sekta ya viwanda nayo imeshika nafasi ya pili katika kuongeza fedha za kigeni nchini ambapo mwaka 2015 mapato yalikuwa Bilioni 1 na kwa sasa yamefikia Bilioni1.5.
Aidha, Prof. Ndulu aliongeza kuwa sekta ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi imesaidia kuimarisha fedha za kigeni ambapo mapato yamefikia Dola Bilioni11 kwa mwaka.
Hadi kufikia sasa Tanzania imenufaika kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika uingizaji bidhaa hiyo kwa asilimia 44.
Serikali inatarajia kuendelea kuimarisha uchumi ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.
Imetolewa na Wizara ya Fedha na Mipango
Kitengo cha Mawasiliano