Serikali yatoa vipaumbele vyake kwa wananchi

evansGREATDeal

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
4,013
2,331
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kulipa deni hilo la taifa ambalo ni zaidi ya billion 30 USD=zaidi ya trillion 48 za Tshs.

Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.

Sasa wadau ktk trillion 48 tunazodaiwa je kwa kuanza na kias hicho cha billion 784.3,..
tutamaliza deni?

Maana ni kiasi kidogo sana cha fedha na pia deni linazidi kukua kila sekunde.

Naleta hoja...

==========================

Serikali imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016, kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa mishahara ya watumishi wa Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.

Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.

Aliongeza kuwa katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi nchini , Serikali imetoa Sh. Bilioni 130 kwa mwezi Januari mwaka 2016 ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 ilitoa Sh. Bilioni 193.

Kwa upande wa Mfuko wa Barabara, Katibu Likwelile alifafanua mradi huo umetengewa kiasi cha Sh. Bilioni 47.89 na kuongeza kuwa Benki kuu ina fungu la mfuko huo ambapo nayo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 76.3.

Dkt. Likwelile alisema kuwa Halmashauri zitapelekewa kiasi cha Sh. Bilioni 20.52 kwa ajili ya kuboresha barabara na jumla mfuko huo kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 274.71.

Akifafanua kuhusu miradi ya umeme, Dkt. Likwelile alisema kuwa mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ililipa deni la TANESCO kiasi cha Sh. Bilioni 80 za mradi wa Kinyerezi II na kwa mwezi Januari mwaka 2016 kiasi cha Sh. Bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.

Hali hii imefikisha kiasi cha Sh. Bilioni 120 kwa ajili ya kulipa madeni na kuendeleza uzalishaji wa umeme nchini.

Alisema kiasi cha Sh. Bilioni 21.959 kimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ina mfuko wa mradi huo ambao kwa sasa una kiasi cha Sh. Bilioni 21.9 na kuongeza kuwa huduma ya umeme kwa wananchi itaimarika.

Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mpaka sasa mfuko huo una jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 46.3.

Aidha, BoT imetoa Sh. Bilioni 12.5 kuendeleza miradi ya maji ambapo kwa Januari mwaka 2016 Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 7.7.

Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 82.2 kwa mwezi wa Januari ili kuweza kulipa pensheni za wastaafu, na kwa wale wastaafu walio katika daftari la kudumu ambapo wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 33.3 kwa ajili ya malipo yao.

Wabunge wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya mkopo wa magari ambapo kila mbunge atapata kiasi cha Sh. Milioni 90, kiasi cha Sh. Milioni. 45 ni ruzuku na Sh. Mil. 45 ni mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 5.

Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.

Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alibainisha kuwa hali ya makusanyo ya mapato nchini iko vizuri ambapo kwa mwezi Januari 2016, makadirio yalikuwa Sh. Trilioni 1 na Bilioni 45 na hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. Trilioni 1 na Bilioni 31 zimeshakusanywa.

Matarajio ya TRA ni kukamilisha kukusanya kiasi cha Sh. Billioni 14 zilizosalia.

Aidha, Kidata alibainisha kuwa uingizaji wa bidhaa kupitia bandarini bado uko vizuri licha ya minong’ono kuwa uzuiaji wa mianya ya ukwepaji kodi imepunguza uingizaji bidhaa ambapo kwa mwezi Januari Bilioni 111 zimekusanywa kutokana na ushuru wa forodha.

Kidata alitoa wito kwa kila mtanzania kulipa kodi na kutoa taarifa za wakwepa kodi ili kuweza kukuza mapato ya nchi.

Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu amepongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.

Alisema kuwa uchumi umekua na unazidi kuimarika licha ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo uchumi wa nchi umekua kwa asilimia 7 na unategemewa kukua miezi ijayo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.

Mfumuko wa bei unaendelea kubaki ndani ya kiwango cha tarakimu moja, licha ya ongezeko dogo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.

Alisema kuwa mfumuko wa bei ulikuwa asilimi 6.8 mwaka 2015, ukilinganishwa na asilimia 6.1 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2015.

Wakati huo huo mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati uliendelea kubaki katika viwango vya chini ya asilimia 2.5 kutokana na hatua mbalimbali za kisera zilizochukuliwa na BoT.

Prof. Ndulu alifafanua mapato ya fedha za kigeni yanaendelea vizuri ingawa bei ya dhahabu imeshuka kutoka Bilioni 2.5 hadi Bilioni1.3.
Sekta ya utalii imesaidia kuimarisha fedha za kigeni kwani mapato yameongezeka kutoka Bilioni 1.5 hadi Bilioni 2.2.

Sekta ya viwanda nayo imeshika nafasi ya pili katika kuongeza fedha za kigeni nchini ambapo mwaka 2015 mapato yalikuwa Bilioni 1 na kwa sasa yamefikia Bilioni1.5.

Aidha, Prof. Ndulu aliongeza kuwa sekta ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi imesaidia kuimarisha fedha za kigeni ambapo mapato yamefikia Dola Bilioni11 kwa mwaka.

Hadi kufikia sasa Tanzania imenufaika kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika uingizaji bidhaa hiyo kwa asilimia 44.

Serikali inatarajia kuendelea kuimarisha uchumi ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.

Imetolewa na Wizara ya Fedha na Mipango
Kitengo cha Mawasiliano
 
Inawezekana kabisa ndani ya miaka mitatu kwa kuongeza zaidi kubana matumizi.
Magufuli atafuta kabisa utegemezi wa wafadhili kwenye bajeti ndani ya mwaka mmoja

Hoja yako ina nguvu, ingawa siyo kwa miaka mitatu. Ni kweli kuwa katika miaka nane au kumi ijayo, Tanzania itakuwa tofauti kabisa ikiwa Magufuli atakuwa Rais hata baada ya 2020. Tanzania itakuwa superpower kiuchumi....
 
Kiuhalisia hilo deni ni magumashi tupu tulikopeshwa kwa masharti makali mno
-lazima lipitie bank zao
-lazima tutumie wataalam wao kwenye chochote
-lazima tutumie firm zenye link na wao kuanzia usafiri mpaka logistics za upangaji nyumba nk
Mwisho wa siku deni limewafaidisha wao, kwa kutoa ajira na biashara kwenye makampuni yao na jamaa zao
 
Walipe tu kidogo kidogo litaishaga, japo sina hakika kama madeni yanaishaga

Sasa kukopa kulipa madeni huo ni Uzuzu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kulipa deni hilo la taifa ambalo ni zaidi ya billion 30 USD=zaidi ya trillion 48 za Tshs,..
Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.
Sasa wadau ktk trillion 48 tunazodaiwa je kwa kuanza na kias hicho cha billion 784.3,..
tutamaliza deni???
maana ni kias kidogo sana cha fedha na pia deni linazidi kukua kila sekunde,...
hoja;


Badala ya kujivunia matumizi ya ovyo ya fedha zetu za kodi, walipaswa waone haya. Kwa binadamu makini alitakiwa afahamu hizo fedha tunazihitaji kufanya mendeleo ambayo yamekwama kwa miaka vizazi kwa visingizio vya serikali ya ccm kuwa haina uwezo wakti kila siku inakopa madeni.

Kabla ya kujifunika uso na kwingine kuko wazi, tunahitaji kwanza watupe mchanganuo wa deni lote lile na zile fedha zote zimetumika je.

Ukiona viongozi wanashangilia ulipaji madeni ya hovyo badala ya kusikitika, ujue taifa linaongozwa kwa laana.
 
Kiuhalisia hilo deni ni magumashi tupu tulikopeshwa kwa masharti makali mno
-lazima lipitie bank zao
-lazima tutumie wataalam wao kwenye chochote
-lazima tutumie firm zenye link na wao kuanzia usafiri mpaka logistics za upangaji nyumba nk
Mwisho wa siku deni limewafaidisha wao, kwa kutoa ajira na biashara kwenye makampuni yao na jamaa zao
Hii ni kweli. Kwa kuongezea ni kwamba kiasi kinachobaki kinatafunwa na wajanja wa humu ndani. Kwahiyo mnalipa deni ambalo halikuleta tija kwa taifa.
 
Badala ya kujivunia matumizi ya ovyo ya fedha zetu za kodi, walipaswa waone haya. Kwa binadamu makini alitakiwa afahamu hizo fedha tunazihitaji kufanya mendeleo ambayo yamekwama kwa miaka vizazi kwa visingizio vya serikali ya ccm kuwa haina uwezo wakti kila siku inakopa madeni.

Kabla ya kujifunika uso na kwingine kuko wazi, tunahitaji kwanza watupe mchanganuo wa deni lote lile na zile fedha zote zimetumika je.

Ukiona viongozi wanashangilia ulipaji madeni ya hovyo badala ya kusikitika, ujue taifa linaongozwa kwa laana.
aiseee ni sahihi kaka,..
hata mimi sijawahi kuskia mchanganuo wa hili deniiii,....
huwa lipo juujuu sana,explained
 
.....Tuchambue madeni ya kuyalipa yale muhimu tu!/ ambayo kweli kwa namna moja au nyingine fedha zake zilitumika kiufasaha !!
hayo mengine apelekewe tu nyumbani.........!?/
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kulipa deni hilo la taifa ambalo ni zaidi ya billion 30 USD=zaidi ya trillion 48 za Tshs,..
Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.
Sasa wadau ktk trillion 48 tunazodaiwa je kwa kuanza na kias hicho cha billion 784.3,..
tutamaliza deni???
maana ni kias kidogo sana cha fedha na pia deni linazidi kukua kila sekunde,...
hoja;
Kwani deni la taifa linakua kwa kiwango gani ili tujue kama kweli hicho kiwango cha ukipaji ni kidogo
 
mh.rais wetu jikite zaidi katika kutuletea maendeleo na nafuu watanzania!
...kama ni deni tuje kulilipa kifahari zaidi hapo baadae baada ya uchumi wetu kusimama imara!/
sioni umaana wowote katika kukimbilia kulipa! wakati viwanda vipo hoi,ajira hakuna,huduma za afya katika ngazi zote bado!,madawati,ubora wa kielimu n.k.
 
More like we are going to bail out these thieves who brought us in this mess in the first place. I say investigate all the loans on how they were spent by the previous administration before we pay them back.
Uhuni mwingi umefanyika mikataba mingi ujanjaujanja 10%watu wamepiga sana na usimamizi mbovu uliokuwepo na bado upo wa mianya ya wizi jitu linakaa katika ofisi ya umma kazi yake ni kubuni mipango ya kwiba tu.
Tuna resources nyingi zikisimamiwa ipasavyo nchi haitakuwa hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom