Serikali yatangaza kiama kwa wapenda migomo vyuoni

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,856
1,101
Nimeisikia híi katika mapitio ya magazeti, imeandikwa katika gazeti ya nipashe. Wamedai watakaondamana kudai kuongezewa mikopo watafutiwa mikopo waliyopewa.

Pia wamepiga marufuku siasa vyuoni na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mytake:

Hivi ni lini serikali iliruhusu maandamano ya kudai mikopo? Mi naona wanajaribu kuwasha moto utakaokosa mzimaji, kwani inaonekana ule mgomo wa 2008 haujawafunza lolote.
SERIKALI imeonya kwamba haitavumilia na kutishia kufuta udhamini wa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini watakaoshiriki kwenye migomo na maandamano kwa sababu zisizo na msingi.

Msimamo huo ulitolewa juzi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipozungumza na jamii ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakati wa ziara ya kujifunza shughuli, utendaji na changamoto zinazozikabili vyuo vikuu nchini.

Alisema msimamo huo wa Serikali unatokana na dhamira ya kuboresha mfumo wa elimu ya juu nchini uliosababisha wizara yake kutengewa Sh 300 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

"Katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2011/12, zaidi ya Sh80 bilioni zilinyofolewa kutoka mfuko wa kuendeleza elimu ya ufundi na kupelekwa bodi ya mikopo ili kuhakikisha wanafunzi zaidi wenye kutimiza masharti na vigezo wanakopeshwa. Hatutakubali fedha nyingi kiasi hicho zipotee bure kwa wanafunzi kuendekeza migomo na maandamano yasiyo na tija badala a kusoma," alisema Dk Kawambwa.

Katika bajeti ya mwaka huu, mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imetengewa Sh317 bilioni ambazo Dk Kawambwa alidai ni kubwa mara 20 kulinganisha na bajeti ya baadhi ya wizara akaitaja ile ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii iliyotengewa fedha isiyozidi Sh17 bilioni.

Kuhusu siasa vyuoni, waziri huyo aliwaagiza wakuu wa taasisi zote za elimu ya juu kuhakikisha hakuna shughuli wala harakati za kisiasa ndani ya maeneo na mazingira ya vyuo vyao ili kuepuka mitafaruku ndani ya jamii zao na kuleta utulivu kwa wahadhiri kufundisha na wanafunzi kujifunza.
 
Eshacky

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
962
243
Ndugu, sisi tuliokosa mkopo ambapo tuliahidiwa na wizara twende jana watupe majibu ya hatima yetu. Tulichofanyiwa jana ni ujinga na dharau zisizostahimilika, et toka tar.20 waliyotupa ahad mpaka jana tar.27 wanasema hawajafanyia kaz swala letu kbs.

Naibu waziri anasema hajui chochote kuhusu sisi. Ila tatizo nilogundua ni udhaifu wa viongozi kutokuwa na msimamo wa kukubaliana na katibu wa wizara ahad zisizo na time frame et tutawasiliana na wazir, how? Tutamtumia email.

So tumepanga leo kwenda kwa wazir mkuu, ila kiukweli hii nchi ni ya ajabu sana. yan wanachojua ni kutishia watu na maaskar wenye miveo ming mabegan na virungu. Jana tulikaa wizaran mpaka saa 1 usiku. Yaani hakuna matumaini ya sisi kupata hiyo mikopo.
 
pole sana mkuu, hawa wanabomoa nyumba waliyomo pasipo kujua. Mtu anaposhndwa kutumia akili huanza kutoa vitisho.
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
wanatakiwa kubadilisha kwanza utaratibu wao kwani ndo unaosababisha kutokuelewana kati ya wanafunza, bodi na chuo
 
tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,856
1,101
Akili za watu kama akina Kawambwa ni janga la taifa, sijui alifikiria nini? Hapa naona wanajaribu kushndana na wakati, ni wakati wa mabadiliko uliopo, ngoja tusubiri.
 
FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Huu ujasiri wa sasa ukilikuwa wapi wakati wa mgomo wa mafuta? Where were all these morons mpaka bunge lilingilie kati wakati watendaji (serikali) wapo? Huko Igunga serikali ya CCM inatuhumiwa kutoa chakula cha msaada kama hongo za kisiasa, sasa serikali hiyo hiyo inaingiza hongo kwenye elimu ya juu! Kusema kuwa mwanafunzi akishiriki maandamano utamnyima mkopo maanake nini kama sio hongo & intimidation at the same time?

Kwa mtindo huu kuna sababu gani kwa CCM kuendelea kuwa madarakani kama hawatambui haki za msingi za raia?
 
hapa wanajaribu kuwatisha wanyonge, mi naamini haya yote lazima yatokee katika kuelekea ukombozi wa kweli. Tena mwaka huu balaa wanalo, mpaka UDSM watu wamekosa mikopo?
 
Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,620
6,279
kwa taarifa yao udsm mgomo utatokea kabla ya mwezi wa 11. Na wataondamana sio wale waliokosa pekee bali ni wanafunz wote,kwa hiyo wafute mikopo yao udsm nzima.
 
Laurence

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
3,104
414
Hii ndio serikali ya CCM,watoto wa masikini wanalalamika kutopewa mkopo lakn Mke wake Riz1 some body Arapha Kikwete kapata 100% mkopo Udom hii si hatari ndugu zangu? ati watu wakiandamana wanatishwa wakati watoto wa wakubwa wanatesa tuu.
 
Eunda

Member
May 2, 2008
60
11
SERIKALI imeonya kwamba haitavumilia na kutishia kufuta udhamini wa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini watakaoshiriki kwenye migomo na maandamano kwa sababu zisizo na msingi.

Msimamo huo ulitolewa juzi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipozungumza na jamii ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakati wa ziara ya kujifunza shughuli, utendaji na changamoto zinazozikabili vyuo vikuu nchini.

Alisema msimamo huo wa Serikali unatokana na dhamira ya kuboresha mfumo wa elimu ya juu nchini uliosababisha wizara yake kutengewa Sh 300 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

"Katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2011/12, zaidi ya Sh80 bilioni zilinyofolewa kutoka mfuko wa kuendeleza elimu ya ufundi na kupelekwa bodi ya mikopo ili kuhakikisha wanafunzi zaidi wenye kutimiza masharti na vigezo wanakopeshwa. Hatutakubali fedha nyingi kiasi hicho zipotee bure kwa wanafunzi kuendekeza migomo na maandamano yasiyo na tija badala a kusoma," alisema Dk Kawambwa.

Katika bajeti ya mwaka huu, mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imetengewa Sh317 bilioni ambazo Dk Kawambwa alidai ni kubwa mara 20 kulinganisha na bajeti ya baadhi ya wizara akaitaja ile ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii iliyotengewa fedha isiyozidi Sh17 bilioni.

Kuhusu siasa vyuoni, waziri huyo aliwaagiza wakuu wa taasisi zote za elimu ya juu kuhakikisha hakuna shughuli wala harakati za kisiasa ndani ya maeneo na mazingira ya vyuo vyao ili kuepuka mitafaruku ndani ya jamii zao na kuleta utulivu kwa wahadhiri kufundisha na wanafunzi kujifunza.
 
Eunda

Member
May 2, 2008
60
11
SERIKALI imeonya kwamba haitavumilia na kutishia kufuta udhamini wa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini watakaoshiriki kwenye migomo na maandamano kwa sababu zisizo na msingi. Msimamo huo ulitolewa juzi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipozungumza na jamii ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakati wa ziara ya kujifunza shughuli, utendaji na changamoto zinazozikabili vyuo vikuu nchini.
Alisema msimamo huo wa Serikali unatokana na dhamira ya kuboresha mfumo wa elimu ya juu nchini uliosababisha wizara yake kutengewa Sh 300 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.“Katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2011/12, zaidi ya Sh80 bilioni zilinyofolewa kutoka mfuko wa kuendeleza elimu ya ufundi na kupelekwa bodi ya mikopo ili kuhakikisha wanafunzi zaidi wenye kutimiza masharti na vigezo wanakopeshwa. Hatutakubali fedha nyingi kiasi hicho zipotee bure kwa wanafunzi kuendekeza migomo na maandamano yasiyo na tija badala a kusoma,” alisema Dk Kawambwa. Katika bajeti ya mwaka huu, mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imetengewa Sh317 bilioni ambazo Dk Kawambwa alidai ni kubwa mara 20 kulinganisha na bajeti ya baadhi ya wizara akaitaja ile ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii iliyotengewa fedha isiyozidi Sh17 bilioni.
Kuhusu siasa vyuoni, waziri huyo aliwaagiza wakuu wa taasisi zote za elimu ya juu kuhakikisha hakuna shughuli wala harakati za kisiasa ndani ya maeneo na mazingira ya vyuo vyao ili kuepuka mitafaruku ndani ya jamii zao na kuleta utulivu kwa wahadhiri kufundisha na wanafunzi kujifunza.
 
Malboro

Member
Jun 24, 2011
23
11
Wanaofanya siasa vyuoni ni wana CCM. Chunguzeni mtaona. Wao ndio waache na wengine bila shaka wataacha tu.
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,538
5,646
Siku zote haki itadumu milele. Wanajaribu kupingana na ukweli. Tamko lao ni sawa na lile la Luhanjo kuwakataza wapinzani kualikwa shule. Huo ni upuuzi. Maandamano ndio njia pekee ya mlalahoi kupaza sauti.
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,161
4,434
Hata ningekuwa mimi ni waziri ningepiga marufuku harakati za Siasa Vyuoni katika kipindi hiki ambacho wasomi karibu woote wanaionyoshea kidole CCM baada ya kufumbuka macho kwamba nchi haina uongozi. Wee unategemea nini kutoka kwa mtu anayejua vizuri theoretically na practically:
1.Impact ya Inflation kwa maisha ya binaadamu
2.Impact ya kuwa na katiba mbovu
3.Impact ya Ufisadi
4.Impact ya utoroshaji nyara za serikali nakadhalika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom