Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,621
- 46,267
Joseph Mungai
Chini ya uongozi wake huyu masomo ya biashara na kilimo yalifutwa kwa baadhi ya shule za sekondari, Physics na Chemistry ikafanywa kuwa kipindi kimoja halafu wizi au uvujishaji wa mitihani ya NECTA ulitamalaki sana.
Shukuru Kawambwa
Huyu chini ya uongozi wake mikopo ya vyuo vikuu ilianza kusuasua na kutolewa kwa vigezo vingi vya ajabu ajabu sana na pia viwango vyenye mkanganyiko mtupu, pia wakati wake ungeweza kukuta wanafunzi wengi tu wenye uhitaji wa mikopo wamekosa na wale ambao hata hawana uhitaji wa hiyo mikopo wamepata mikopo.
Joyce Ndalichako
Huyu akumbukwe zaidi kwa upande wa makato kupanda kutoka 8% hadi 15% kwa wanafunzi waliochukua mikopo ya vyuo vikuu.
Adolf Mkenda
Huyu wa sasa yeye legasi yake kubwa inaweza kuwa kuundwa kwa tahasusi rasmi za kidini katika elimu ya juu ya sekondari.