tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Nimeisikia híi katika mapitio ya magazeti, imeandikwa katika gazeti ya nipashe. Wamedai watakaondamana kudai kuongezewa mikopo watafutiwa mikopo waliyopewa.
Pia wamepiga marufuku siasa vyuoni na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mytake:
Hivi ni lini serikali iliruhusu maandamano ya kudai mikopo? Mi naona wanajaribu kuwasha moto utakaokosa mzimaji, kwani inaonekana ule mgomo wa 2008 haujawafunza lolote.
Pia wamepiga marufuku siasa vyuoni na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mytake:
Hivi ni lini serikali iliruhusu maandamano ya kudai mikopo? Mi naona wanajaribu kuwasha moto utakaokosa mzimaji, kwani inaonekana ule mgomo wa 2008 haujawafunza lolote.
SERIKALI imeonya kwamba haitavumilia na kutishia kufuta udhamini wa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini watakaoshiriki kwenye migomo na maandamano kwa sababu zisizo na msingi.
Msimamo huo ulitolewa juzi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa alipozungumza na jamii ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakati wa ziara ya kujifunza shughuli, utendaji na changamoto zinazozikabili vyuo vikuu nchini.
Alisema msimamo huo wa Serikali unatokana na dhamira ya kuboresha mfumo wa elimu ya juu nchini uliosababisha wizara yake kutengewa Sh 300 bilioni kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
"Katika bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2011/12, zaidi ya Sh80 bilioni zilinyofolewa kutoka mfuko wa kuendeleza elimu ya ufundi na kupelekwa bodi ya mikopo ili kuhakikisha wanafunzi zaidi wenye kutimiza masharti na vigezo wanakopeshwa. Hatutakubali fedha nyingi kiasi hicho zipotee bure kwa wanafunzi kuendekeza migomo na maandamano yasiyo na tija badala a kusoma," alisema Dk Kawambwa.
Katika bajeti ya mwaka huu, mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imetengewa Sh317 bilioni ambazo Dk Kawambwa alidai ni kubwa mara 20 kulinganisha na bajeti ya baadhi ya wizara akaitaja ile ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii iliyotengewa fedha isiyozidi Sh17 bilioni.
Kuhusu siasa vyuoni, waziri huyo aliwaagiza wakuu wa taasisi zote za elimu ya juu kuhakikisha hakuna shughuli wala harakati za kisiasa ndani ya maeneo na mazingira ya vyuo vyao ili kuepuka mitafaruku ndani ya jamii zao na kuleta utulivu kwa wahadhiri kufundisha na wanafunzi kujifunza.